Deni la Trilioni 17. 1 TANZANIA imesingiziwa ? au Ni Ukweli ?

jnuswe

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,270
549
Kwa watanzania wote wenye mapenzi mema suala hili pengine linahtaji mjadala wa kitaifa juu ya Deni la Taifa ambalo sasa linafikia takribani trilion 17.1, nimeangalia jinsi linavyoendelea kupanda kila kukicha, mwaka 2008 lilikuwa trilion 7.6 mwaka 2009 Trilion 10.5 na sasa trilion 17.1

Yaani hii inamanisha kwamba wanaolidai taifa wakisema ndani ya mwaka 2011/2012 tulipe deni lote. Deni hilo litakomba bajeti yote ya Mkullo na tutafungwa maana haitatosha.

Ndiyo maana nikatangulia kusema hapa mjadala wa kitaifa ni muhimu , uchumi wa nchi hii uko ICU, sijui wadau mnasemaje juu ya hili
 
Wao wanasema uchumi unapaa kila mwaka.Hawa jamaa majuha kweli.Inakuwa vp uchumi unapaa wakati den linazidi kuongezeka? Kama lingekuwa deni la kijasilia mali (strategic debt) isingekuwa taab manake lingeweza kuisha hata kesho.Lkn la kwetu ni la kijinga hata mpangilio wa kulipa ni wa kijinga vile vile
 
Nashukuru sana mkuu nawe kwa kuliona hilo, yaani huyu jamaa inaonyesha baada ya kumaliza akiba iliyokuwa imeachwa na Beni, yeye akaanza kukopa tu na kutuongezea mzingo usiokuwa na maana, eti unakopa alafu huoni manufaa ya mkopo haya maajabu !
 
Baada ya trillioni kuna nini?....maana tulitoka deni la milioni...kisha billioni...sasa trilioni
 
hapo na fikiri ni mwisho, kitakachofuatwa sasa ni watanzania kuuzwa ili kulipa deni, maana wanyama ambao ni maaliasili ya Taifa wameanza kusafirishwa kwa ndege si jajua kama ni sehemu ya kulipa deni au laa, nchi hii uozo mtupu
 
WABUNGWE WALIPWE POSHO ZAIDI.

Serikalini Posho ziongezwe maana zitasababisha ufanisi uongezeke na kipato cha taifa kupanda....

Msiwe na wasiwasi, uchumi wetu unaendelea vizuri sana. Hata USA wana madeni na ni matajiri wa dunia.
 
rais yupo ulaya kazi yake kulalamika tuuuu kila siku eti vyombo vya habari vya africa kazi yao kuzungumza mabaya tuuu...najisikia aibu kuwa mtanzania...sosi habari tbc sijui hata kaenda eti mkutano wa ILO...sijui hakuna wzr au hamuamini, eti alikuwa anaongea na mabalozi.

Na bado tutakoma kwani nini tutakao lipa ni sisi wtz hasa ungizingatia hata budget haitoshi yote matumizi wataendelea kukopa mpaka wamalize kipindi chao lazima deni liwe trilion 40
 
Bajeti yetu ni Tshs. 13. Trillion.
Deni letu ni Tshs. 17.1 Trillion!

Hivi kuna hata wanaodhubutu kutukopesha kweli?
 
Bajeti yetu ni Tshs. 13. Trillion. Deni letu ni Tshs. 17.1 Trillion!Hivi kuna hata wanaodhubutu kutukopesha kweli?
Lazima waendelee kutukopesha ili deni lidumu milele na hatimaye watu-dictate milele!
 
Hahahahahaaaa... Trillioni Kumi na saba??????

Tumekwisha............
 
Wakati huo huo tunaambiwa uchumi wa nchi umepaa kwa 7% lakini umasikini umebaki pale pale!shame upon us.
 
Wakati huo huo tunaambiwa uchumi wa nchi umepaa kwa 7% lakini umasikini umebaki pale pale!
 
sasa hofu nyingine ni kwamba hao wanao tudai na hivi wameanza kusikia Bahi kuna uranium watasema tulifidie Deni kwa njia hiyo maana dhahabu ni kama imekwisha sijui kama imebaki na kama bado ipo ya kutosha nayo watawapa
 
hi kama unajifunza darasa la kwanza ukimaliza kujifunza herifi ya mwisho (za ze zi zo zu)....inafata harufi gani
au nda ..nde..ndi ...ndo....
 
Back
Top Bottom