Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
MWISHONI mwa wiki iliyopita, Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo) Zitto Kabwe, kupitia mitandao ya kijamii, alitoa taarifa kwamba Deni la Taifa la Tanzania kwa sasa limefikia Dola 15 bilioni ambazo ni zaidi ya Shs. 30 trilioni.
Kutokana na ukubwa wa deni hilo, Zitto Kabwe anasema, Tanzania hulipa Huduma ya deni la taifa takriban Shs. 2.2 trilioni kila mwaka, fedha ambazo ni nyingi kuliko hata bajeti ya wizara yoyote nchini.
Lakini akasema kwamba, ndani ya madeni hayo kuna ambayo yamepatikana kwa rushwa na mengine yamechukuliwa kwa matumizi ya anasa tu, yaani ‘odious debts’.
Deni mojawapo la hovyo ni la Dola 600 milioni (Shs. 1.2 trilioni) ambalo Tanzania ilikopa kutoka Benki ya Standard ya Uingereza kupitia Hati Fungani (Bonds), mkopo ambao Taasisi ya Serious Fraud Office (SFO) ya Uingereza imebainisha kwamba umepatikana kwa rushwa huku taasisi nyingine ya Corruption Watch ya Uingereza pia ikisema kwamba Tanzania imepata hasara ya Dola 80 milioni (Shs. 160 bilioni) kwa kuchukua mkopo huo.
SOMA ZAIDI...