Deni la Taifa lazidi kupaa. Upinzani wataka CAG kufanya ukaguzi

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
CAG%2001%2033.jpg


DENI la taifa limeongezeka maradufu, hali ambayo imeifanya kambi Rasmi ya Upinzani kushtuka na kumtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalum.

Ongezeko hilo, kwa mujibu wa kambi ya upinzani, deni hilo limeongezeka kwa kiasi hivyo, kutoka mwaka 2010 hadi mwaka jana.

Akiwasilisha maoni ya Kambi ya Upinzani kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kwanza wa Maendeleo ya Taifa wa Mwaka 2011/12 hadi 2015/16 na mwelekeo wa Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa wa Mwaka 2015/16 hadi 2020/21, Naibu Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani, Wizara ya Fedha na Mipango, David Silinde, alisema hali ya deni la taifa inatisha na Bunge linapaswa kushituka.

Silinde alisema nchi itafilisika kama Ugiriki ikiwa Bunge halitachukua hatua madhubuti za kuisimamia serikali.

Alisema deni la taifa limekuwa na kufikia dola za Marekani bilioni 19.141 (Sh. trilioni 41.536). Alisema deni liliongezeka maradufu mwaka jana, baada ya serikali kukopa dola bilioni 3.846 (Sh. trilioni 8.347).

"Mwishoni mwa Juni, 2010, jumla ya deni la Tanzania lilifikia dola bilioni 9.9 (Sh. trilioni 13.6) kulingana na thamani ya dola kipindi hicho). Miaka mitano baadaye deni limefikia Sh. trilioni 41.5, lazima Bunge tushituke," alisema Silinde.

"Fedha zilizokopwa kuanzia 2010 hadi 2015 zilifanyia miradi ipi ya maendeleo? Mikopo hii ina riba kiasi gani, tumeweka nini kama dhamana ya kupatiwa mikopo au ile minong'ono mitaani ya vitalu vya gesi?

"Mkopo mkubwa wa mwaka 2010 ambao ni sawa na asilimia 5.9 ya deni lote ulitumika kufanyia jambo gani? Fedha hizi zimetumika kugharamia miradi gani au ndiyo EPA ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015?

"Majibu ya maswali haya yatapatikana tu kama itafanyika 'Special Audit' ya deni la taifa. Mkopo huu ni hatari zaidi kama hautalipwa kwa wakati kwani riba itaongezeka maradufu na kuifanya nchi ifilisike.

"Kwa sababu hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani inamtaka CAG kufanya ukaguzi maalum wa deni la taifa na kuleta taarifa ya ukaguzi huo bungeni kwa ajili ya kujadiliwa,” aliongeza.

Serikali yakubali

Akizunguma na Nipashe nje ya ukumbi wa Bunge jana mchana, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, alisema serikali iko tayari CAG afanye ukaguzi huo kwa kuwa fedha hizo zilitumika kwa miradi mbalimbali ya maendeleo.

"Wizara yangu haina kipingamizi, CAG aje atukague. Deni la taifa lipo tangu kipindi cha uongozi wa (Mwalimu Julius) Nyerere. Tunakopa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Tutamwonyesha CAG miradi iliyotekelezwa," alisema.

Awali, akieleza kuhusu Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa wa Mwaka 2015/16 hadi 2020/21, Silinde alilitaka Bunge kutunga sheria ya utekelezaji wa mpango huo kwa maelezo kuwa bila kufanya hivyo hautatekelezeka kama uliopita.

Mbunge huyo wa Mbozi Magharibi (CHADEMA), alisema mpango uliopita, ulikuwa na lengo la kujenga barabara kwa kiwango cha lami Km 5,204 (kila mwaka Km 1,040.8) ndani ya miaka mitano, lakini zilizojengwa ni Km 2,775 (kila mwaka Km 555), sawa na asilimia 53 ya lengo.

"Mwalimu Nyerere aliondoka (madarakani) mwaka 1985, aliliachia Shirika la Ndege (ATCL) ndege 11, lakini kwa sasa linamiliki ndege 'zero' (sifuri), ilhali likiwa na wafanyakazi wengi wanaolipwa kodi za wananchi," alisema.

Kuhusu reli, Silinde alisema serikali iliweka lengo la kukarabati Km 2,707 kwa kiwango cha 'standard gauge', lakini hadi sasa imekarabati Km 136 tu (wastani wa Km 27.2 kwa mwaka). Ili kutimiza malengo ya miaka mitano ya Km 2707, Silinde alisema serikali itatumia miaka 99.5.

Kweye kilimo, Silinde mpango uliopita ulikuwa na lengo la kukuza kilimo kwa asilimia sita kwa mwaka, lakini sekta hiyo imekuwa kwa asilimia 3.4 kwa kipindi chote cha miaka mitano, huku akidokeza kuwa mpango huo haukuleta matokeo chanya katika sekta ya elimu.

Kadhalika, katika mpango uliopita, Silinde alisema lengo lilikuwa kuzalisha Megawati 2,780 za umeme ndani ya miaka mitano, lakini katika kipindi chote zimeongezeka MW 496.24, hivyo Tanzania itahitaji miaka 13 kufikia malengo ya mpango wa kwanza.


Chanzo: Nipashe
 
Hao walioikopesha hela Tanzania sijui kama watakuja kulipwa na kama wakija kulipwa wakati wanabahati sana.
Kwasababu saizi nasikia wanataka waende wakakope zingine Na wamejiwekea malengo ndani ya miaka 5 wakope tena trion 48 nasijui hizo hela watazilipa vipi.
 
Hao walioikopesha hela Tanzania sijui kama watakuja kulipwa na kama wakija kulipwa wakati wanabahati sana.
Kwasababu saizi nasikia wanataka waende wakakope zingine Na wamejiwekea malengo ndani ya miaka 5 wakope tena trion 48 nasijui hizo hela watazilipa vipi.
Mkuu kudai deni kimataifa ni tofauti kabisa na kitaifa.

Hilo deni la kimataifa huwezi kulikwepa, utalipa tu.
 
Mkuu kudai deni kimataifa ni tofauti kabisa na kitaifa.

Hilo deni la kimataifa huwezi kulikwepa, utalipa tu.
Inamaana hilo Deni hakuna kikomo cha kulipa hata kama ni 300 ni sawa tu. kwamaana hilo Deni kila siku linaongezeka Na hatujui hatima yake nini.
 
Inamaana hilo Deni hakuna kikomo cha kulipa hata kama ni 300 ni sawa tu. kwamaana hilo Deni kila siku linaongezeka Na hatujui hatima yake nini.
Mataifa yanayokopesha kama China hufurahia kukopesha mataifa machanga maana pamoja na kukutoza riba lakini pia hawataki kulipwa cash.

Wanaweza kuja kuchukua dhahabu yenye thamani sawa na deni lao, na hapo ndipo tunapoumizwa sana.

Hii imefanyka nchi nyingi sana za SADC, Wanakupa mkopo wa kujenga miundombinu, unawapa kuchimba mafuta free kufidia deni.
 
Deni la taifa limeongezeka maradufu, hali ambayo imeifanya kambi Rasmi ya Upinzani kushtuka na kumtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalum.

Ongezeko hilo, kwa mujibu wa kambi ya upinzani, deni hilo limeongezeka kwa kiasi hivyo, kutoka mwaka 2010 hadi mwaka jana.

Akiwasilisha maoni ya Kambi ya Upinzani kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kwanza wa Maendeleo ya Taifa wa Mwaka 2011/12 hadi 2015/16 na mwelekeo wa Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa wa Mwaka 2015/16 hadi 2020/21, Naibu Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani, Wizara ya Fedha na Mipango, David Silinde, alisema hali ya deni la taifa inatisha na Bunge linapaswa kushituka.

Silinde alisema nchi itafilisika kama Ugiriki ikiwa Bunge halitachukua hatua madhubuti za kuisimamia serikali.Alisema deni la taifa limekuwa na kufikia dola za Marekani bilioni 19.141 (Sh. trilioni 41.536).

Alisema deni liliongezeka maradufu mwaka jana, baada ya serikali kukopa dola bilioni 3.846 (Sh. trilioni 8.347)."Mwishoni mwa Juni, 2010, jumla ya deni la Tanzania lilifikia dola bilioni 9.9 (Sh. trilioni 13.6) kulingana na thamani ya dola kipindi hicho).

Miaka mitano baadaye deni limefikia Sh. trilioni 41.5, lazima Bunge tushituke," alisema Silinde.
 
Mataifa yanayokopesha kama China hufurahia kukopesha mataifa machanga maana pamoja na kukutoza riba lakini pia hawataki kulipwa cash.

Wanaweza kuja kuchukua dhahabu yenye thamani sawa na deni lao, na hapo ndipo tunapoumizwa sana.

Hii imefanyka nchi nyingi sana za SADC, Wanakupa mkopo wa kujenga miundombinu, unawapa kuchimba mafuta free kufidia deni.
Hapo nimekupata.
 
Mheshimiwa Raisi anapaswa kuchukua hatua haraka,tuangalie ni jinsi gani tunaweza kupunguza deni ndani ya miaka hii mitano
 
DENI LA TAIFA LA MAREKANI LIMEPAA SANA
HUU ULIKUWA NI MPANGO WA TRUMP KUHUSU DENI HILO.
=============================
==========================
In a recent interview, presidential candidate Donald Trump said he would pay off the nation’s $19 trillion debt “over a period of eight years.”

He can’t. The numbers don’t add up. In fact, our estimates of Mr. Trump’s plan so far show debt will instead double to above $38 trillion.1

Setting aside whether paying down the debt makes economic sense, achieving this goal would be virtually impossible – particularly for a candidate who has proposed large tax cuts and ruled out significant entitlement reforms. Paying off the debt would require unprecedented tax increases, spending cuts, and economic growth.

Spending Cuts or Economic Growth Wouldn’t Do It

Gross debt (currently $19 trillion) will reach nearly $28 trillion by the end of 2025.2 To save that much money would require cutting all spending by two-thirds or achieving 16 percent real annual economic growth; growth is currently projected to average 2.1 percent.

Excluding Social Security – which Mr. Trump has said he would not significantly change – the rest of government would need to be cut by 93 percent.

Donald Trump has also proposed over $10 trillion of tax cuts and spending increases through 2025. Incorporating these, spending would have to be cut about 90 percent and the economy would have to grow more than 20 percent per year.

Asset Sales Won’t Do It

Selling federal assets couldn’t cover this $28 trillion to $38 trillion of costs. According to the Financial Statement of the United State Government, the government holds only $3.1 trillion of assets (excluding stewardship assets and natural resources) – and much of that couldn’t or shouldn’t be sold, at least not for a significant profit.

Trade Can’t Do It

Nor would Mr. Trump’s suggestion of “renegotiating all of our deals…the big trade deals that we’re doing so badly on” help to pay down the debt. The trade deficit has only an indirect economic relationship with the budget deficit, and outside of some small amount of tariff revenue and modest GDP effects, better trade deals would not significantly impact the national debt. In all likelihood, Trump’s changes to trade policy would reduce rather than enhance growth, according to several economists.

Donald Trump’s Policies Won’t Do It – They Will Increase the Debt

Ultimately, no plausible set of policies could pay off the debt in eight years; this would require deficit reduction 13 to 18 times as large as what the President has put forward and 4 to 6 times what House Republicans have called for. And neither of these proposals cut net taxes nor take Medicare and Social Security off the table.

Rather than pay off the debt, Donald Trump’s policies – as proposed so far – would increase it.



Our Rating: False

1 $38 trillion represents the almost $28 trillion that the gross debt will reach under CBO’s current law projections, plus our “low” estimate of the total cost of the policies on Mr. Trump’s website. We projected those policies would add at least $11.7 trillion to the debt by 2026. Here, we’re using a figure of $10 trillion by 2025, to account for the fact that Trump’s claim is over eight years.

2 These numbers refer to the gross federal debt, which as a technical matter would be quite difficult to pay off because it includes debt the government owes itself in various trust funds. Instead, we assume Mr. Trump is aiming to generate an amount of savings equal to the gross federal debt. For purposes of this analysis, we assume his goal is to do so by the end of the 8th full fiscal year starting from the next President’s first day in office. This allows for 8 years and 8 months in total.

Source:Donald Trump Can Pay Off the National Debt in 8 Years
 
Wanauchumi wanasema mkopaji/mdeni wako ni asset yako. Kwa hiyo Tanzania sasa ipo kwenye assets books ya mataifa mengi Duniani.

Ni ujinga kusema kuwa Tanzania inapoteza uhuru wake kwa kupewa misaada, na kudhani kuwa tuna uhuru wetu kwa kuwa mdeni sugu.

Mwenye deni/mdeni wako sugu ni mnyonge wako. Hakuna cha uhuru hapo lazima umheshimu aliyekukopesha wakati wote, hasa unapokuwa huna uwezo wa kulipa. Leo Ugiriki kwenye mikutano ya Jumuiya ya Ulaya imekuwa kama mgonjwa asiye na tumaini la kupona. Mataifa yanayoisaidia Ugiriki huwa yanakaa kama jopo la madaktari bingwa wanapojadili hali ya mgonjwa asiyeleta matumaini hata baada ya kupewa matibabu ya kila aina.

Hali hiyo ya Ugiriki wala siyo tofauti na Tanzania na mataifa mengi ya Afrika.
 
Maadam maisha yanazidi kuwa ghali na watu kuongezeka deni halikwepeki.

Tunapunguza deni na riba inaongezeka kila mwaka yaani ukikopa na hujafanya kitu unatwanga maji tu
 
Ipo siku tuambiwa tuhame nchini hapa kwa jinsi hali ya uchumi na deni inavyozorota na kuongezeka respectively. Mwaka 2015 january, deni la taifa ilikuwa usd 18,748.4 milioni wakati exchange rate ilikuwa ni tzs 1745.6/1usd.

Mwaka huu 2016 january,deni la taifa limefikia usd 19,521.8 milioni wakat exchange rate ni 2150.8.Na katka deni hili,la nje ni usd 15,475.4 milioni na la ndani ni usd 4046.4 milioni.kwa namna hii,tutaendelea kutawaliwa kiuchumi na mabepari.tunaishia kupga kelele zisizo na msingi kila uchwao.

Ngoja niishie hapa kwa sasa.
 
Kwa mujibu wa hotuba ya bajeti ya mwaka huu nchini Tanzania, deni la taifa limeongezeka na kufikia zaidi ya shilingi trilioni 40.

Je unafahamu kuwa kila mtanzania anadeni ya zaidi shilingi milioni moja ?

Na leo tunahoji;

Je taifa linawezaje kuwa na jitihada mpya na za ziada za kupunguza au kuondoa kabisa deni lake ?

Chanzo: BBC
 
Deni la Taifa limeshafikia Trilioni 45 ukiweka na mkopo wa Trilioni 7 kwenye hii bajeti hewa ya 2016/2017 mwakani litafikia Trilioni 52 kama siyo zaidi hasa ukitilia maanani makusanyo ya kodi ya kila mwezi yaliyofikia Trilioni na ushee sasa yameshuka na kufikia kati ya bilion 600 na bilioni 700.
 
Kwa mujibu wa hotuba ya bajeti ya mwaka huu nchini Tanzania, deni la taifa limeongezeka na kufikia zaidi ya shilingi trilioni 40.

Je unafahamu kuwa kila mtanzania anadeni ya zaidi shilingi milioni moja ?

Na leo tunahoji;

Je taifa linawezaje kuwa na jitihada mpya na za ziada za kupunguza au kuondoa kabisa deni lake ?

Chanzo: BBC
Naweza kwenda kulipa million moja yangu nikawa huru au kupunguza deni?
 
Back
Top Bottom