Deni la taifa lazidi kupaa sasa limefika US bil 52 kwa ongezeko la toka dola bil 49.2 la mwaka jana. Waziri adai wataendelea kukopa bado ni himilivu

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
#NipasheBUNGENI "Hadi kufikia Agosti mwaka huu deni la Taifa lilifikia Dola bilioni 52, ikilinganishwa na Dola bilioni 49.2 katika kipindi cha Agosti mwaka jana, hivyo deni bado ni himilivu" - Waziri wa fedha na Mipango, Dkt. Mpango.
 
Juzi tumeambiwa deni la Marekani limepaa kwa 100%

Sisi Tanzania ni Nani hadi tusidaiwe?

Bado hatuna viwanda vya kutosha
 
😂😂 Himilivu!!,siku litakapo kuwa si himilivu itakuwa ndo mwanzo wa maumivu.
 
Juzi tumeambiwa deni la Marekani limepaa kwa 100%

Sisi Tanzania ni Nani hadi tusidaiwe?

Bado hatuna viwanda vya kutosha

Na bado, mtanyoosha maelezo. Nchi tajiri huku deni linazidi kuongezeka huku mkiweka 10% kwenye miradi na hamtaki ukaguzi. Tutajuana tabia tu.
 
Mi natamani kabla ya kukopa Bunge lingekuwa linapitia na kujilizisha na sababu zinazopelekea tukope.

Hii nchi ni ya wananchi, Mungu akipenda huyo jamaa anaweza kufa akatuachia madeni yasiyolipika.
 
#NipasheBUNGENI "Hadi kufikia Agosti mwaka huu deni la Taifa lilifikia Dola bilioni 52, ikilinganishwa na Dola bilioni 49.2 katika kipindi cha Agosti mwaka jana, hivyo deni bado ni himilivu" - Waziri wa fedha na Mipango, Dkt. Mpango.
Waandishi wetu wa habari hawana uelewa mzuri wa takwimu ndogo za uchumi. Deni kweli lina shoot sana ila for now lipo around USD 24 Billion ambayo ni roughly TZS Trillioni 52.9

Issue ni kwamba shillingi yetu ipo kwenye mood ya kudhoofika of which deni la taifa litazidi kuongezeka in nominal terms.

So ni limepanda kutoka TZS Trillioni 49.2 hadi TZS 52.9 Trillioni na sio hiyo USD Billion 49.2 kama waandishi walivo report
 
Mi natamani kabla ya kukopa Bunge lingekuwa linapitia na kujilizisha na sababu zinazopelekea tukope.

Hii nchi ni ya wananchi, Mungu akipenda huyo jamaa anaweza kufa akatuachia madeni yasiyolipika.
Keshasema anakopa na hawaambii kakopa wapi,na anaekagua hela akiwa kidomodomo anatumbulia.

Wewe ukitaka ujue kwamba deni linakua kwa kasi fuatilia kila siku ukinunua kitu kodi unakatwa %ngapi.
Ukiona % zinapanda kila siku ujue ndio unapunguza deni hivyo mkuu.
 
Mi natamani kabla ya kukopa Bunge lingekuwa linapitia na kujilizisha na sababu zinazopelekea tukope.

Hii nchi ni ya wananchi, Mungu akipenda huyo jamaa anaweza kufa akatuachia madeni yasiyolipika.

Mkuu bunge hili hata likipelekewa ni kazi bure tu.
 
Back
Top Bottom