Deni la Taifa in and out, kinachoumiza sio kukopa ni matumizi ya kinachokopwa

Mkuu swali zuri.. actually madhara ya kushindwa kulipa deni yatachofanya ni kwamba, nchi itakuwa down graded na wakopeshaji.

Na ukiwa downgraded maana yake huwezi kukopesheka tena.

Lakini impact kubwa huwa inakuwa ni trickle down effect ya kitachotokea baada ya kushindwa kulipa madeni.

1. Wawekezeji watakimbia maana macro fundamentals zita deteriorate.

2. Mfumuko wa bei

3. Pesa itashuka thamani kwa kasi..

4. Nchi inaweza kushindwa kumudu baadhi ya matumizi ya muhimu kabisa..

Yaani ikitokea, impact yake itakuwa ni mambo mengi magumu yatatuandama sana kwenye uchumi

Hizo hapo juu ndio athari zinazozipata nchi zinazoshindwa kulipa madeni yake [ INSOLVENT; NOT CREDIT WORTHY} Na nchi ikifikia hatua hizo ndio utasikia nchi ina machafuko, haitawaliki kwa sababu ya vurugu, yakiwemo maandamano yasiyokwisha na hatimaye JESHI huingilia kati na kupindua serikali!!!!
 
Hii dhana ya deni la taifa huwa inawapa shida sana watu wengi.

Shida kubwa inakuja kwenye usahihi wa upimaji wa deni la taifa.

Kuna njia mbili za kuangalia deni la taifa.

1. Absolute term - hii ni kama Ndugai alichofanya leo. Kuangalia deni la taifa kama namba mfano ni kusema deni limefika Trillioni 70. Madhara ya kuangalia deni in absolute term ni kwamba haitoi picha halisi na haisemi maana yake ni nini?.. Wala haiwezi kukuambia kama deni ni kubwa au dogo. Hichi ndo kafanya Ndugai leo.. anasema deni linakuwa kwa kasi limefika Trillioni 70.. So, what does it mean? Je ni kubwa au ni dogo? Na kwanini?

Ukiangalia absolutely huwezi kamwe kujijibu hayo maswali hapo juu.

Njia ya pili ya kuangalia deni la taifa ni

2. Relative terms - hapa ni unafananisha deni la taifa na pato la taifa (GDP). Kwa mfano, ikiwa deni la Taifa ni Trillioni 70 na pato la taifa ni Trillioni 145 maana yake in relative terms deni la taifa litakuwa 70/145 au 48% ambayo ki masuala ya mikopo hiyo bado ni stahimilivu ki nadharia, ukichukulia mfano kama una mshahara wa Sh. 145k na unadeni la Sh. 70k maana yake ni kwamba unaweza wa kulipa unachodaiwa na bado ukabakiwa na salio la karibu nusu.

Idea hapa ni kwamba kasi ya ukuaji wa GDP kama ni kubwa itafuta kabisa impact za deni kwa nchi, ila vice versa is true, GDP ikidondoka deni lazima litakuua.

Kwa maana hiyo, ukiwa unamulika in relative terms, ni kweli deni la taifa linaweza kukua in absolute terms mfano kutoka 70 Trillioni to 80 Trillioni to 90 Trillioni.. So hapo Ukitumia jicho la Ndugai maana yake deni linapaa, lakini ukiangalia in relative terms, kama GDP yaani pato la taifa nalo linakuwa kwa kasi kubwa kuliko ukuaji wa deni la taifa maana yake ile ratio ya deni la taifa to GDP itakuwa inashuka hata kama deni la taifa linakuwa in absolute terms.

Hivo basi, swali kubwa la kuulizwa siku zote ni' ..... Je, uchumi wetu unakuwa kwa kasi kuzidi deni la taifa?

Hilo ndilo swali ambalo Ndugai na watanzania wote tunapaswa kuuliza.. Maana yake kama uchumi haukui kwa kasi kuzidi ukuaji wa deni la taifa, then ni kweli kwamba tunaelekea kwenye debt crisis kama hofu ya Ndugai na watanzania wengine. Yaani debt crisis itakuwa ni kwamba pato la nchi halitaweza kuhimili madeni yanayokopwa na impact ya hichi kitu huwa ni mpasuko wa kiuchumi wa nchi husika, madhara yake huwa hayapimiki.

Kwa maana hiyo basi, kama tumeelewana kwenye hoja namba moja kuhusu tafsiri haswa ya deni la taifa, nataka kugusia hoja yangu namba mbili, ambayo ndiyo haswa shida kubwa mimi binafsi nnayoiona kwenye deni la taifa la Tanzania.

"Matumizi ya kinachokopwa"

Matumizi ya deni ndo mchawi mkubwa wa deni la taifa la Tanzania.

Kwa sababu ni aina ya matumizi ya mkopo ambayo itakuambia kwamba, mikopo unayokopa itakuza uchumi (GDP) au la. Angalia mfano hapa chini tuelewane vema

Mfano. mwalimu mwenye mshahara wa laki 7 anaweza kukopa Milioni 10 benki kwa mkopo wa makato ya laki 3 kwa mwezi.

Kuna utofauti mkubwa wa kati ya haya matumizi ya mkopo ambayo ni possible kwa mwalimu

1. Kununua gari la kutembelea - Hii haitakuza uchumi wa mwalimu kwasababu gari ambalo amenunua mwalimu halitaweza kutengeneza kipato kwa sababu lenyewe litakuwa linataka kuhudumiwa kila mwezi. Mafuta, service etc, ukichanganya hizi gharama na marejesho ya mkopo, unaona kabisa kwamba mkopo aliokopa mwalimu utakuwa ni chanzo cha kurudisha maendeleo yake nyuma. Maana mshahara ukitoka, akitoa laki 3 ya kulipa mkopo, pesa ya service, pesa ya mafuta, kodi ya nyumba... Tayari habakiwi na chochote... anaendelea kuwa masikini mwenye misururu ya madeni.

2. Lakini vipi kama mwalimu akitumia mkopo wake wa milioni 10 kununua uba au taxi au daladala? maana yake ni kwamba amewekeza mkopo wake kwenye wealth generating mashine ambayo kwanza itatoa ajira, itampa kipato yeye mwenyewe na atafanya maendeleo yake mwenyewe.. Yes in relative term deni au mkopo aliokopa mwalimu utakuwa umezaa utajiri kwa mwalimu na madhara ya hilo deni wala hayawezi kamwe kumuumiza mwalimu.

Tafasiri
Mfano wa kwanza. Mwalimu kachukua mkopo ambao matumizi yake hayana economic benefit.

At national level, haina tofauti na Magufuli kukopa na kujenga uwanja chato..no economic benefit.. kuna project chungu mbovu za dizaini hiyo katika nchi yetu tunazishughudia kila siku...

Most of these loans, huwa inaishia kwenye Operating expenses na white elephant projects ambazo huwa hazina mchango kwenye kukuza uchumi wa nchi directly.. Kama kununua mindege ile.. return yake uki compare na projects cost unaona kabisa ni mimba kwenye uchumi...

Ili kukuza uchumi wa nchi inatakiwa mikopo ielekezwe kwenye capital expenditure na tena kuwe na feasibility study za kutosha na wananchi tupewe mda wa kuchambua na kutoa maoni juu ya matumizi ya mikopo ili tuone kama itakuza uchumi au la.

Hayo ni kwa ufupi tu hili suala jinsi lilivo.

Ukiingia deep sana, utaanza kujiuliza, Je, wabunge ambao ndio wanapitisha hizi matumizi ya mikopo, wanaelewa kiasi gani?

Je, demokrasia ya kuwapata ipoje?

Kuna mlolongo mrefu sana, na kwa mfumo uliopo Tanzania kwa sasa, ni kweli kabisa hatutakwepa a debt crisis.. ni suala la muda tu.

Umeelimisha vizuri ukaharibu ulipoanza kumshambulia Hayati JPM. Hili zimwi la kuhangaika na marehemu sijui litaisha lini akili mwa baadhi ya Watanzania.

Yuko mwengine akasema kwa miaka mitano JPM amekopa zaidi ya miaka 10 Mkapa na miaka 10 Jakaya.

Mzee Mwinyi aliongea vizuri wakati flani akasema kwa miaka 5 JPM mambo aliyo yafanya yametufunika sisi tuliomtangulia wote.

So tumpogeze Rais SSH alivyo mjibu Spika Ndugai kuhusu hoja yake ya deni la Taifa. Tumpongeze Ndugai kwa uthubutu wake. Haya mengine ya kumshambulia Spika ni kufilisika kisiasa. Nyerere JK alishafafanua vizuri juu ya muflisi wa kisiasa. Pengine former CAG atapata pakutokea safari hii. Huyu hawezi msahau Ndugai kwa ile TKO.
 
Kukopa sio kubaya mkuu.. sema inatakiwa uhakikishe mkopo unaelekezwa kwenye viable projects.

Kukopa sio kubaya lakini ukope kwa akili sio kwa kufuata hisia; Kumbuka kuwa mkopeshaji anafanya biashara hivyo kama utakopa na kurudisha mkopo na riba basi hatasita kukukopesha zaidi. In fact kukopa kunaweza kukuletea sifa kama unakopa na kuweza kurudisha mikopo!!

Hakuna uwekezaji wa kijinga umewahi kufanyika nchini kama ule wa kwenda kununua ndege za ATCL zaidi ili hali zilizopo hazitumiki at full capacity!!! Hawasemi lakini fedha nyingine walizokopa walizitumia kununua hiyo mindege. Hasara ya shirika ni mzigo mzito sana wanabebeshwa wananchi bila kuonewa huruma na watawala kwani wanazidi kuongeza TOZO tu ili kupata mapato zaidi!!!
 
Back
Top Bottom