Deni la SUKITA ladhaminiwa na serikali.. la THI je?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,498
40,047
Habari Leo

Serikali hadi sasa imekwisha kutoa udhamini kwa mashirika mbalimbali wenye thamani wa zaidi ya Sh bilioni 350, imeelezwa.Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Jeremiah Sumari alikuwa akimjibu Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbrod Slaa (Chadema), aliyeuliza athari za udhamini huo kwa serikali ambao umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka.

Mashirika hayo na fedha ambazo serikali imeyadhamini katika mabano ni Shirika la Umeme Tanznaia (Tanesco) Sh 139,314,978,184, ATC Ltd (Sh bilioni 72) na Shirika la magari la Taifa (SMC) (Sh 2,898,840,716).Mengine ni Mamlaka ya Mkonge Tanzania (TSA) Sh 1,024,933,969, Shirika la Uchumi la CCM SUKITA ambalo limekwisha kufilisika na liko chini ya mfilisi (Sh 10,139,494,513) na Chama cha Ushirika Mara (Sh 8,502,977,181).

Naibu Waziri aliyataja mashirika mengine kuwa Kiwanda cha Nguo Urafiki (Sh 25,781,394,288.75), Kampuni ya General Tyre East Africa (Sh 12,530,800,000) na Chama cha Ushirika Nyanza (Sh 1,370,509,071.27).Alisema serikali inayo Kamati ya taifa ya Madeni kwa mujibu wa Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada ya Serikali ya mwaka 1974 iliyorekebishwa mwaka 2004.

Wajumbe wa kamati hiyo ni makatibu wakuu wa wizara mbalimbali, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Mhasibu Mkuu wa Serikali.“Kazi kubwa ya kamati hii ni kutathmini kwa kina shirika au kampuni inayoomba udhamini wa serikali na hatimaye kumshauri Waziri wa Fedha na Uchumi ipasavyo,” alisema.

Alisema athari za udhamini ni wakati shirika au kampuni inaposhindwa kulipa deni lililotokana na dhamama iliyotolewa ni kwa serikali kutakiwa kulilipa deni husika. Akijibu swali la nyongeza la Dk. Slaa, alisema ufutaji wa deni lililodhaminiwa na serikali una utaratibu na hufanywa inapoonekana ni busara.

Alitoa maelezo hayo baada ya Mbunge huyo kutaka deni la Tanesco lililodhaminiwa na serikali la zaidi ya Sh bilioni 139 lifutwe ili kusaidia shirika hilo lipunguze gharama za umeme kwa watumiaji.Dk. Slaa pia alitaka watu wanaohusika na deni la Sukita lililotokana na ununuzi wa pombe kali na matairi katika miaka ya 1985 hadi 1990 na ambao alisema wanajulikana washitakiwe.

My Take:

Mimi nilidhani kuwa serikali inadhamini mashirika ambayo ina hisa TU. Kama wameweza kutoa udhamini wa bilioni 10 kwa Sukita kweli wameshindwa kutoa udhamini kiduchu kwa THI ili iweze kupata misaada inayohitaji na kuweza kujikita na kuwa taasisi?
 
Naomba kuuliza:

Shirika la Magari la Taifa (SMC) (Sh 2,898,840,716). Hili shirika linashughulika na nini?
 
Dr. Slaa, hili swali umeliuliza ndani yake kuna mambo mengi na ya kushangaza kweli. Je hawa wanaokaa na kuamua kuhusu haya madeni na udhamini ni kina nani? wanaingia kutokana na nyadhifa zao au wanachaguliwa tu?
 
Dr. Slaa, hili swali umeliuliza ndani yake kuna mambo mengi na ya kushangaza kweli. Je hawa wanaokaa na kuamua kuhusu haya madeni na udhamini ni kina nani? wanaingia kutokana na nyadhifa zao au wanachaguliwa tu?


Jibu lake halitakuwa mbali na Gavana wa Benki kuu akishirikiana na Waziri wa Fedha...!!
 MKJJ

Lol usifanye utani..mimi ninatafuta kujua kweli. Wanashughulika vipi magari wakati kila kitu kinaagizwa nje na kutengezezwa kwenye gereji za magomeni, tabata n.k

I know.. nilikuta natania maana kama yale mafumbo ya zamani yanayosema "Baba John alikuwa na mtoto mmoja, mtoto wake alikuwa anaitwa nani"?

Ila hilo shirika la magari kwa kweli tunahitaji kujua kwani kuna Nyumbu ambalo linahusiana na magari ya kijeshii ambayo yanatengenezwa hapo TZ. Hili la TMC linatengeneza magari gani? au labda wanamaana magari ya serikali ndiko yanakotengenezwa au kununuliwa?
 
SUKITA si ina majengo mengi sana tuu? kweli kuna mpango wa kulipa au kwa sababu ni CCM ndio watu wasahau? Au mpaka kije chama kingine madarakani ndio litaanza kulipwa? na vitu walivyonunua ni pombe!!?
 
Dk. Slaa pia alitaka watu wanaohusika na deni la Sukita lililotokana na ununuzi wa pombe kali na matairi katika miaka ya 1985 hadi 1990 na ambao alisema wanajulikana washitakiwe.

Hili ndilo lile shirika la CCM, ambalo lilianzishwa na kupewa Bwana Kapinga, aliyeliuwa shirika la Umma la Dabco, lakini akapewa hili shirika hewa anyways,

Ukweli wa kisiasa ninaoujua ni kwamba hili shirika lilianzishwa kwa ajili ya cover tu, kwa sababu wafadhili walikuwa wameanza kuibana serikali yetu kutaka kujua CCM walikuwa wanatoa wapi hela za mikutano ya Chimwanga na kujenga majengo makubwa ya makao makuu ya CCM mikoani? Kwa hiyo walillianzisha hili shirika na kujifanya kuwa hela zao zinatokea huku Sukita, huku wakilipa hela kila mwaka kutoka Hazina ambazo zilikuwa un-accountable kwa anybody kwa ajili ya kuendesha chama, ndipo kina Msuya walipotajirikia hapa!

Ninaamini ni RIP Kolimba, ndiye aliyekuja na hii idea ya Sukita, yaani wafanya kazi wa kawaida tu wa hili shirika hakuna ambaye hakujenga nyumba ya kisasa kwa mikopo toka Sukita, ambayo mpaka leo haijalipwa na hakuna anayeidai, baada ya kuliua hili shirika Kapinga alipewa mlo mwingine tena serikalini, ifike mahali hawa viongozi waliohusika watinge kwenye mikono ya sheria maana wapi wananchi tuta-draw the line na kusema kuwa enough is enough?
 
I know.. nilikuta natania maana kama yale mafumbo ya zamani yanayosema "Baba John alikuwa na mtoto mmoja, mtoto wake alikuwa anaitwa nani"?

Ila hilo shirika la magari kwa kweli tunahitaji kujua kwani kuna Nyumbu ambalo linahusiana na magari ya kijeshii ambayo yanatengenezwa hapo TZ. Hili la TMC linatengeneza magari gani? au labda wanamaana magari ya serikali ndiko yanakotengenezwa au kununuliwa?


Dr Slaa hakuweka swali la nyongeza, kwa nini Sukita idhaminiwe na serikali na labda hili shirima la magari linatengeneza magari gani. Au sisi ndio mambumbu peke yetu...
 
Dr. Slaa, hili swali umeliuliza ndani yake kuna mambo mengi na ya kushangaza kweli. Je hawa wanaokaa na kuamua kuhusu haya madeni na udhamini ni kina nani? wanaingia kutokana na nyadhifa zao au wanachaguliwa tu?
MKJJ
Ni kweli inashangaza.Kamati yenyewe inaitwa Kamti ya Taifa ya Madeni(NDMC) imeundwa chini ya Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaasa ya Serikali (Government Loans, Guarantees and Grants Act,1974 as Revised 2004. Wajumbe ni Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali, Benki Kuu na Mhasibu Mkuu wa Serikali. Hivyo wako wanaoingia kwa Kofia yao (ex-officio na wako wanaoteuliwa. Inaonekana hakuna check and balance kabisa. Waziri hakujibu Swali katika ukamilifu wake wote. Mfano japo amejibu kama SUKITA ilifilisika hakusema chochote kwa mfano kuhusu State Motor Corporation ambayo sina hakika kama liko hai tena. Tusipoangalia mpango huu wa udhamini utawaingiza Watanzania katika tatizo kubwa huko tunakoenda. Kiwango hiki kinasemekana kimeongezeka zaidi katika mwaka wa Fedha wa 2007/2008, na idadi inaongezeka kwa kadiri midhamana hii inavyoiva. Tunahitaji kuwa makini sana.
 
Habari Leo

My Take:[/B]
Mimi nilidhani kuwa serikali inadhamini mashirika ambayo ina hisa TU. Kama wameweza kutoa udhamini wa bilioni 10 kwa Sukita kweli wameshindwa kutoa udhamini kiduchu kwa THI ili iweze kupata misaada inayohitaji na kuweza kujikita na kuwa taasisi?

THI waliomba Sukita Wakanyimwa?...Pia Kwasasa Sukita ina-exist?
 
Back
Top Bottom