Deni la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii: Serikali yadaiwa jumla ya shilingi 6 trilioni

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,668
149,839
Kamati ya Bajeti imesema moja ya eneo ambalo Serikali ina changamoto kubwa ya kutatua madeni yake ni katika mifuko ya jamii yanayofikia zaidi ya Sh6 trilioni.

Akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo makamu mwenyekiti Josephat Kandege amesema licha ya Serikali kuonyesha nia njema ya kulipa madeni hayo likiwamo la Mfuko wa Pensheni wa PSPF bado utekelezaji wake umekuwa wa kusuasua.

“Mfano kwa mwaka wa fedha 2015/16, Serikali iliahidi kutoa kiasi cha Sh150 bilioni pamoja na kutoa Non Cash Bond ya Sh2.6 trilioni ili kulipa deni la PSPF lakini hadi sasa ni Sh83 bilioni tu zilizotolewa na hakuna Non Cash Bond yoyote iliyotolewa,”amesema Kandege.

Amesema kuwa kamati inaona madeni hayo ni tishio kubwa linaloathiri utekelezaji wa majukumu ya mifuko husika hasa ulipaji wa pensheni ya wastaafu wanaongezeka kila mwaka.

Chanzo:Mwananchi online
 
Jamaa wanatumia fedha za wastaafu na afya kujengea maghorofa.Uwiii
 
Nchi ya ajabu, mtu mmemhifadhia pesa zake na tena mnafanya nazo biashara ambapo ktk hizo biashara yeye hanufaiki chochote. Mwisho wa siku anataka hata ule mtaji wake, tena inakuwa ni taabu, shida. Hata aibu hamna!
 
Yaani hii nchi ni ya ajabu sana. Wanachama wenyewe wa PSPF wanapostaafu huwachukua miaka miwili hadi mitatu kupata mafao yao, wengine hufa kabla ya kupewa pension zao ilhali walishastaafu. Kumbe hizi pesa wanazochangia zinatumika kuwaingiza madikteta madarakani then wanakuja kuwahujumu wale wale waliowadhulumu pesa zao. Naomba Mungu awalaani wote wanaosababisha mateso kwa wastaafu, hasa wanachama wa PSPF.
 
Kama kuna mahali hii nchi imeoza basi ni kwenye hii mifuko ya jamii na deni la taifa.
Hapa ukiangalia kuna mazingaumbwe makubwa.
Mifuko yote inapaswa kuwa optional ili kila mtu afe na chake, wabaki wale wanaoogopa kukaa na hela.
 
Unakata Mwezi wa 6 sasa wastaafu wa PSPF wa kuanzia January mpaka May hawajapata chao kila wakienda wanaambiwa Serikali haijapeleka hela na wakati Serikali hii hii Mwezi March ilitoa ahadi ya kulipa deni la PSPF kabla Mwezi June haujaisha. Na bora hawa wastaafu wangekuwa wanapewa kile kiinua mgongo chao cha kila Mwezi japo kingewapunguzia ukali wa maisha hawapewi wanaambiwa mpaka wapate kile kiinua mgongo chao cha jumla ambacho haifahamiki kitapatikana lini.
 
Mbaya zaidi, usishangae utakapotambua kwamba sehemu kubwa ya fedha hiyo ilitumika katika uchaguzi wa 2015

kumuwezesha Jecha kufanya vitu vyake...
 
Serikali hii dhalimu inayojinasibu kuwa inamtetea mnyonge huku wanyonge wa Taifa hili waliolitumikia Taifa kwa uzalendo uliotukuka wakiendelea kusotea viinua mgongo vyao inatufanya tuamini kauli za kumtetea mnyonge ni kauli za kinafiki,kipuuzi na kipumbavu zaidi.

Haiwezekani uuhadae Umma wa Watanzania kuwa unawatumikia wanyonge huku serikali hiyohiyo ikiyafumbia macho mateso wayapatayo wazee wetu.Kutowapa mafao yao kwa wakati ni kuwaweka kwenye mashinikizo ya kimaisha jambo linaloweza kuzifupisha siku zao za kuishi.

Kwa nini serikali iamue kuwa "agent" wa kifo kwa Raia wake?Mzee aliyetumia nguvu zake zote na sehemu kubwa ya maisha yake kulitumikia Taifa,kisha akatelekezwa bila msaada wowote huku akiendelea kuyasotea mafao yake kumfanya mzee huyo aishi kwa mashaka ndani ya nchi yake.
 
Yaani Mkuu nina Shangazi yangu ambaye amestaafu January mwaka huu alikuwa ni Mwalimu wa Secondary last week alipoenda PSPF Makao Makuu Posta kufuatilia mafao yake alichojibiwa eti aende tena kuulizia Mwezi August mwanzoni,huwezi amini yule Mama wa watu pressure ikapanda akalazwa Hospital siku mbili tulichoamua ni kumpiga marufuku asifuatilie tena apumzike tuu nyumbani wenzake kama wakipata watampa taarifa. Hii ni mbaya sana kwa wanyonge ambao wamelitumikia Taifa kwa nguvu na kwa uzalendo mkubwa kwa mishahara midogo bila posho yoyote leo anastaafu hata kile kidogo walichomnyonya wanashindwa kumpatia kwa wakati muafaka.
 
Yaan hawa wat wamelaaniwa. Ukiondoa lile den la trillion 50+ tunalodaiwa na hili tena. Mijitu ni kama michwa kutafuna tuu na ukiwasikia kabla ya hotuba zao tunamrudishia mwenyez mungu shukran mwingi wa rehema
 
Kuna jamaa mtoa huduma amefirisika baada ya kutolipwa hela zake na NHIF kwa kipindi kirefu .
 
Yaani Mkuu nina Shangazi yangu ambaye amestaafu January mwaka huu alikuwa ni Mwalimu wa Secondary last week alipoenda PSPF Makao Makuu Posta kufuatilia mafao yake alichojibiwa eti aende tena kuulizia Mwezi August mwanzoni,huwezi amini yule Mama wa watu pressure ikapanda akalazwa Hospital siku mbili tulichoamua ni kumpiga marufuku asifuatilie tena apumzike tuu nyumbani wenzake kama wakipata watampa taarifa. Hii ni mbaya sana kwa wanyonge ambao wamelitumikia Taifa kwa nguvu na kwa uzalendo mkubwa kwa mishahara midogo bila posho yoyote leo anastaafu hata kile kidogo walichomnyonya wanashindwa kumpatia kwa wakati muafaka.

Inasikitisha sana,hayo ndiyo mateso wayapatayo wazee wetu.
 
Nchi ya ajabu, mtu mmemhifadhia pesa zake na tena mnafanya nazo biashara ambapo ktk hizo biashara yeye hanufaiki chochote. Mwisho wa siku anataka hata ule mtaji wake, tena inakuwa ni taabu, shida. Hata aibu hamna!
What is the way forward! Haisaidii kitu kulalamika tu!
 
Back
Top Bottom