Wimbo wa demu mcharaza solo wa Werrason !

Kimuziki hilo ni zao la Mzee Simaro Lutumba wa Bana OK . Anaitwa Sarah Solo.
 
Kwa hiyo ni usajili kabisa au ilikuwa kunogesha?

Naona pengo la Flam Kapaya na Kimbangu limezibwa sasa.
 
Ni swala la muda I believe kuna mengi yanakuja kwa huyu bidada maana anajua na kuimba na amepitia kwenye mikono ya gwiji la rhumba DRC Congo Simaro Lutumba.

Ni kipaji halisi kabisa. Siyo mchezo dada anacharaza solo anaichezesha minjemba ndombolo uliona wapi?.

Kwa Werrason ni kupata platform nzuri ya kutoka na ametoa wengi.

Na hii ndiyo namna nzuri na murua ya kukuza na kulea vipaji vya kudumu.

Ama sivyo tutakuwa tunazalisha wasanii "BIG G".
 
Back
Top Bottom