Demu anahisi kuwa Mama yangu Hampendi

Freddy81

Member
Feb 3, 2009
99
3
Hv jamani kama demu wako anhisi kuwa mama yako mzazi hampendi, na wewe unajua kuwa hakuna tatizo, ni njia ipi iliyo ya busara kuchukua ili uweke mambo sawa? mana mama anadai hana tatizo naye,,.....
 
Nasubiria mawazo yenu ndugu zangu

Pole Freddy
Kwanza unatakuwa kuuliza kwa undani ni kwa nini huyo dada anahisi mama hampendi ni dalili zipi alizoona zinazomfanya ahisi hivyo.

Pili akishakujibu basi chunguza vizuri uone kama kweli hizo dalili alizotaja zinaashiria chuki -usitegemee tu kwenye kumwuliza mama kwani hata kama ni kweli mama hawezikubali.

Tatu, ukigundua kuna walakini jaribu kuchunguza sababu halisi kwani inawezekana tu ni wivu wa mama kwa mtoto yaani mama wakwe wenguine huwa na wivu kwa watoto waao huamini kuwa hakuna mtu atakayeweza kumunza mwanaye kama alivyoweza yeye so outomatically huwa wanajiwekea vijitabia flani na wakwe zao sio chuki in such

All the best
 
Mtu hawezi kukurupuka akasema mama yako hampendi,
lazima kuna sababu mwambie akueleze heizo sababu, na pia ukae na mama yako umwulize ingawa hatasema ukweli atajikosha kwaako,
wewe unatakiwa ufanye uchunguzi wako mwenyewe either huyo msichana hampendi mama yako kwa hiyo anatafuta sababu,
au ni kweli mama hampendi binti cha muhimu hapo ni kuwatenganisha wakae mbali mbali wawe wanaonana mara moja moja.
au msichana ana tabia mbaya ndo mana mama hampendi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom