DEMU ALINITOSA LEO,ANANILILIA ,nisaidien wakuu.

Umeshasema havutii tena, unamtaka wa nini tena?

hahah, king'asti hapa kutokuvutia ni mabadiliko ya kiuchumi tu, chezea shopping, mambo ya shear illusion, mariedo etc. lara1 atanirekebsha kama nimekosea hayo majina.. mimi sina cha kushauri wanawake ndivyo mlivyo sijui labda ndio necha yenu.
 
hayo ndo matatizo ya long distanc relatnshp,mabinti wengi wanakuwa hawana uhakika na huo uhusiano wa cmu na kuchat ukizingatia men wengi wakt hawaaminik mabint kwa asil wanahitaj uhalisia na uwepo wa mhusika cyo blahblah za kwenye phone.so akitoke smone physicaly kwa nn asipewe nafac? Fairytale ni kwa wanaume wa mbele2 bongo michosho2
 
mkuu achana na vyuma chakavu,tafuta mwanamke mwingine huyo kashobokea mpunga tu
akitoka tena anakudelete,so you better watch ur steps dude,asije kukupa na vitu vingine...let me off here!
 
wee umesema havutii kama zamani sasa tabu ipo wapi au unataka nawe upate revenge? kama hivyo sawa kamatia piga mzigo huo na sepa zako
 
Wakuu mimi nilikuwa nimemaliza shule ya msingi mwaka 1997,mapambano primary School, mjini Dsm. Nilikuwa nasoma na Mtoto mmoja mkali sana yaani mzuri wa sura. lakini kipindi hicho alikuwa rafiki yangu tu wa kawaida. Baada ya Darasa la saba me nilifaru kwenda AZANIA Sec. School. yule binti alikuwaalichaguliwa kwenda kisutu Sec. School.

Lakini me wazee wakamua niende Maua Seminary, Na yule binti akaenda kifungiro. wakati huo tulikuwa tuna wasiliana kama marafiki tu wakati wa likizo. baada ya kumaliza o"level yule binti akapelekwa Loleza, me nilipangiwa Songea boys High school but nikaamua kwenda Sangu high school Mbeya. Nikakutana na yule binti Mbeya ,

Basi tukaanza mahusiano ya kimapenzi mwaka huo. tulikuwa wote tunarudi likizo pamoja na wote tunaenda shule pamoja tukifika mbeya kila mtu anaelekea shuleni kwake.Tuliendelea na mahusiano na kila mtu akijitahidi kwenye masomo. Me nilikuwa nasoma PCM na yeye CBG.
Matokeo ya advance Tukafauru na kajiunga na Chuo Udsm. B.Eng Computer Engineering and IT yeye alipata kuajiliwa na PEA COCK Hotel kabla ya chuo kuanza.(kumbuka miaka hiyo tulikuwa tunakaa mwaka mmoja kabla ya kujiunga na chuo tofauti na sasa watu wanaunganisha.)

Me niko shule yeye yupo kazin ,akaanza kuniletea mapozi kila kimtafuta alikuwa yupo bize sana, nilikuwa najikaza ikafika kipindi nikimpigia mpaka simu hapokei. Basi nikachukulia easy.

na mimi mwaka ule ule nikapata Schoraship ,ya kwenda kusoma Urusi nikaacha udsm nikaenda urusi kusoma kozi ileile Computer Science Engineering. kozi yanguilikuwa ya miaka mitano.nilipomaliza mwaka wa kwanza urusi, nikaja Dsm kutembea likizo nikamtafuta yule binti kwa bidiii zote nikaenda kwao nikawakuta wazazi wake nikamuulizi bcoz walikuwa wananijua walinikalibisha wakaniambia mwenzako amehama amehamia kimara amepanga. wakanipa namba yake.

Baada ya kunipa namba yake nikampigia ,nikajitamburisha kwa kweli alinikumbuka akasema yupo bize kidogo nimpigie baadaye.

Baadaye nikampigia tena ,akaniambia yupo ndani ya gari akishuka atanipigia ,nikasubiri nikaona apigi. Baadaye niakamua nimpigie ikapokelewa ile simu lakini ni sauti ya mwanamke mwingine ikisema " we ni nani mwenye simu hayupo" nikajitamburisha ,akaendelea kusema " wewe ndiye unataka kuharibu ndoa ya wifi yangu na kaka yangu" nikawa pazzled , sijakaa sawa nikapigiwa mimi ikasikika sauti ya mwanaume " wewe ndiye unamsumbua mke wangu" nika changanyikiwa zaidi. Nikaanza kujiuliza hivi huyu binti ameshaolewa mbona nimeenda kwao hawajanipa hiz taarifa,nilisikitika sana coz nilimpenda sana huyu mdada.

likizo ilikuwa imeisha nikarudi zangu Urusi, nikaa kule mpaka nimemaliza Chuo, miezi mitatu kabla sijamaliza chuo nilikuwa nachati kwenye Marafiki.com . Bahati nzuri nika mkuta yule bint online kwa jina lake lile lile ,me nilikuwa natumia nickname . Nikamuuliza wewe ndiye X akanijibu kama ifutav
nimelitoa jina mutanisamehe.nimeliita (X).



Nikamuuliza umeshawahi kuishi Mbeya?
akajibu:

mmmh nilishawahi kuwa Mbeya ila ni mda mrefu sasa, wewe je uko wapi?

Nikamwabia me nipo Urussi ,kwa kweli alikuwa anajua kama mimi bado niliendelea Udsm,hakujua kama niliacha pale

nikamwambia wewe ni (X),akanijibu:

"its me ma dia, sasa waweza nambia wewe ni nani?"



Nikamwambia unamjua (Y)?,yaani mimi
akajibu:

"ndio namfahamu wewe ni nani?"


Nikamwambia mimi ndiye (Y) .

akanijibu:"naomba nikupe email yangu ili tuwasiliane m___X@yahoo.com nakukumbuka sana ma dia"

nafurahi kuchat na wewe tena.
nikamwambia sehemu nilipo na kitu gani nakifanya
"mmmh sawa nafurahi kusikia hivyo mimi nipo bado dar maisha yamenipiga ile mbaya mpaka natamani nitorokee vijijini. Ni lini unakuja bongo ama umeshahamishia life yako huko kwa warusi?

akaanaza kuniomba msamaha kwa yote yaliotokea ,nikanuuliza mumeo hajambo akasema hajaolewa bado kumbe ile ilikuwa nini hakunipa jibu lakini inaonekana kama alipigwa kibuti na huyo jamaa ambaye alikuwa anaishi naye.ananibembeleza turudiane ,alinuliza siku ya kurudi dar nikamwambia ,
narudi tu Air port nikamkuta naye anakuja kunipokea ,ni muda imepita miaka miwili sasa bado ananibembeleza kwa sasa ameshaanza chuo yupo Mzumbe anasoma Degree ya Busness administration.

lakini siku hiz havutii kama alivyokuwa anavutia zamani.


Wazee mnasemaje naombeni ushauri.


Najua wewe unahamu ya kumlipizia.... sasa fanya hivi vuta, piga halafu mtose..
 
lara 1, njoo umwokoe zombie mmoja anayetaka kuwa upgraded to 'the one and only one'

Ni kawaida hayo kutokea baada ya kuachana na umpendaye, unaamua kujikabidhishwa kwa zombie aliye kairbu yako.

Definition ya zombie, utaipata kwa Lara 1
 
Last edited by a moderator:
Wanawake wengi bwana tafuta mwingine.awachelewa kukuita ZOMBIII miaka zaid ya 7 unamfukuzia demu unakuwa kama asenal kuhusaka ubigwa
 
Ndiomkuusana,sikiliza moyo wako na utakupa jibu.Nilichofurahia kwenye stori hii ni kuwa tulimaliza Shule mwaka mmoja(1997),O-Level tukachaguliwa Seminari (Maua 1998)moja na Advance tukapangwa Shule Moja(Songea Boys 2002).Na chuo Tulichaguliwa Chuo Kikuu Kimoja baada ya Matriculation ya Mwisho UD(2005). Nimefarijika sana...
 
Shetani akiondoka achana nae maana akirudi huwa wanarudi 'WAWILI'
 
ndiyomkuusana kiukweli sina jinsi ya kukueleza kiuhalisia uachane na huyo binti kifupi hakufai. Wanawake wa aina hiyo ni hatari sana na wa kuwaupuka kama ukoma.

Ni wazi keshagundua jioni inaingia sasa anaanza kutafuta pa kulala.
 
Last edited by a moderator:
Piga chini wala usiwaze tena Ningekuwa Mimi ningemwambia majini yako naona yamenigeukia mimi.
 
Piga chini hiyo mtu. Ulipomhitaji hakuona umuhimu wako! Leo amesikia Urusi anaona unafaa. Wana wa eva bana.
 
Just leave her...coz hata ukiwa nae u wont feel comfortable bcz utakua ukikumbuka hayo aliyokufanyia and even unaweza kuhisi anaweza kuyafanya tena! but she is your friend remember, kubaki marafiki wa kawaida si mbaya
 
Kwa kifupi huyo demu ni opoturnist anaangalia uwezo wa kifedha huyo hakufai tafuta mtu wa maisha yako hapo bila bila.
 
Binafsi huwa sirudi nyuma aisee yaani kesha pigwaaaaa weeee leo ndio anakuona wa maaana duh am nt ready for that shit

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
kaka kwani huko urusi ukubahtika kumpata mzungu?plz wadada wa bongo pasua kichwa kaka ona alivokubadilikia wakati mumesoma toka msingi duuu kweli kua uyaone na si ******
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom