DEMU ALINITOSA LEO,ANANILILIA ,nisaidien wakuu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DEMU ALINITOSA LEO,ANANILILIA ,nisaidien wakuu.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ndiyomkuusana, Oct 5, 2012.

 1. ndiyomkuusana

  ndiyomkuusana JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 627
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Wakuu mimi nilikuwa nimemaliza shule ya msingi mwaka 1997,mapambano primary School, mjini Dsm. Nilikuwa nasoma na Mtoto mmoja mkali sana yaani mzuri wa sura. lakini kipindi hicho alikuwa rafiki yangu tu wa kawaida. Baada ya Darasa la saba me nilifaru kwenda AZANIA Sec. School. yule binti alikuwaalichaguliwa kwenda kisutu Sec. School.

  Lakini me wazee wakamua niende Maua Seminary, Na yule binti akaenda kifungiro. wakati huo tulikuwa tuna wasiliana kama marafiki tu wakati wa likizo. baada ya kumaliza o"level yule binti akapelekwa Loleza, me nilipangiwa Songea boys High school but nikaamua kwenda Sangu high school Mbeya. Nikakutana na yule binti Mbeya ,

  Basi tukaanza mahusiano ya kimapenzi mwaka huo. tulikuwa wote tunarudi likizo pamoja na wote tunaenda shule pamoja tukifika mbeya kila mtu anaelekea shuleni kwake.Tuliendelea na mahusiano na kila mtu akijitahidi kwenye masomo. Me nilikuwa nasoma PCM na yeye CBG.
  Matokeo ya advance Tukafauru na kajiunga na Chuo Udsm. B.Eng Computer Engineering and IT yeye alipata kuajiliwa na PEA COCK Hotel kabla ya chuo kuanza.(kumbuka miaka hiyo tulikuwa tunakaa mwaka mmoja kabla ya kujiunga na chuo tofauti na sasa watu wanaunganisha.)

  Me niko shule yeye yupo kazin ,akaanza kuniletea mapozi kila kimtafuta alikuwa yupo bize sana, nilikuwa najikaza ikafika kipindi nikimpigia mpaka simu hapokei. Basi nikachukulia easy.

  na mimi mwaka ule ule nikapata Schoraship ,ya kwenda kusoma Urusi nikaacha udsm nikaenda urusi kusoma kozi ileile Computer Science Engineering. kozi yanguilikuwa ya miaka mitano.nilipomaliza mwaka wa kwanza urusi, nikaja Dsm kutembea likizo nikamtafuta yule binti kwa bidiii zote nikaenda kwao nikawakuta wazazi wake nikamuulizi bcoz walikuwa wananijua walinikalibisha wakaniambia mwenzako amehama amehamia kimara amepanga. wakanipa namba yake.

  Baada ya kunipa namba yake nikampigia ,nikajitamburisha kwa kweli alinikumbuka akasema yupo bize kidogo nimpigie baadaye.

  Baadaye nikampigia tena ,akaniambia yupo ndani ya gari akishuka atanipigia ,nikasubiri nikaona apigi. Baadaye niakamua nimpigie ikapokelewa ile simu lakini ni sauti ya mwanamke mwingine ikisema " we ni nani mwenye simu hayupo" nikajitamburisha ,akaendelea kusema " wewe ndiye unataka kuharibu ndoa ya wifi yangu na kaka yangu" nikawa pazzled , sijakaa sawa nikapigiwa mimi ikasikika sauti ya mwanaume " wewe ndiye unamsumbua mke wangu" nika changanyikiwa zaidi. Nikaanza kujiuliza hivi huyu binti ameshaolewa mbona nimeenda kwao hawajanipa hiz taarifa,nilisikitika sana coz nilimpenda sana huyu mdada.

  likizo ilikuwa imeisha nikarudi zangu Urusi, nikaa kule mpaka nimemaliza Chuo, miezi mitatu kabla sijamaliza chuo nilikuwa nachati kwenye Marafiki.com . Bahati nzuri nika mkuta yule bint online kwa jina lake lile lile ,me nilikuwa natumia nickname . Nikamuuliza wewe ndiye X akanijibu kama ifutav
  nimelitoa jina mutanisamehe.nimeliita (X).  Nikamuuliza umeshawahi kuishi Mbeya?
  akajibu:[TABLE="align: center"]
  [TR]
  [TD="colspan: 2"][TABLE="align: center"]
  [TR]
  [TD]mmmh nilishawahi kuwa Mbeya ila ni mda mrefu sasa, wewe je uko wapi?
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [HR][/HR]
  Nikamwabia me nipo Urussi ,kwa kweli alikuwa anajua kama mimi bado niliendelea Udsm,hakujua kama niliacha pale

  nikamwambia wewe ni (X),akanijibu:
  [TABLE="align: center"]
  [TR]
  [TD]"its me ma dia, sasa waweza nambia wewe ni nani?"  Nikamwambia unamjua (Y)?,yaani mimi
  akajibu:

  [TABLE="align: center"]
  [TR]
  [TD]"ndio namfahamu wewe ni nani?"


  Nikamwambia mimi ndiye (Y) .

  akanijibu:"naomba nikupe email yangu ili tuwasiliane m___X@yahoo.com nakukumbuka sana ma dia"


  [TABLE="align: center"]
  [TR]
  [TD]nafurahi kuchat na wewe tena.
  nikamwambia sehemu nilipo na kitu gani nakifanya
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  "mmmh sawa nafurahi kusikia hivyo mimi nipo bado dar maisha yamenipiga ile mbaya mpaka natamani nitorokee vijijini. Ni lini unakuja bongo ama umeshahamishia life yako huko kwa warusi?

  akaanaza kuniomba msamaha kwa yote yaliotokea ,nikanuuliza mumeo hajambo akasema hajaolewa bado kumbe ile ilikuwa nini hakunipa jibu lakini inaonekana kama alipigwa kibuti na huyo jamaa ambaye alikuwa anaishi naye.ananibembeleza turudiane ,alinuliza siku ya kurudi dar nikamwambia ,
  narudi tu Air port nikamkuta naye anakuja kunipokea ,ni muda imepita miaka miwili sasa bado ananibembeleza kwa sasa ameshaanza chuo yupo Mzumbe anasoma Degree ya Busness administration.

  lakini siku hiz havutii kama alivyokuwa anavutia zamani.


  Wazee mnasemaje naombeni ushauri.

  UPDATES:


  Mimi nilishaoa na nina mtoto mmoja, na Yeye alishaolewa na ana mtoto mmoja lakini kila siku ananisumbua kwenye simu,fb ,wasapp eti anataka kuonana na mimi, Ananiambia eti hafurahii ndoa yake kabisa, na mimi na familia yangu tumeokoka , tunamtegemea Mungu kwa kila kitu. Sitaweza Chepuka hata siku moja.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 2"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Sina mengi ya kukuambia ,ila ushauri wangu ni kwamba achana nae
   
 3. A

  Africa_Spring JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu kama unampenda usihofu unaweza kujaribu tena kumpa nafasi coz kajifunza sasa na nakuhakikishia atakua mke mwema. Ila kwa upande mwingine nikuwa alionyesha hali ya tamaa. Aliona wewe utachukua muda mrefu kufikia hatua ya huyo jamaa yake. Wanawake wengi sana wanatabia hiyo especially anapo pewa ahadi ya kuolewa na jamaa.
  PIMA MAJI KAKA NA UMAWEZA OGEREA
   
 4. k

  komamgo JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 14, 2012
  Messages: 819
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 80
  usihangaike na huyo....wako hivyo . Ni Mungu kawaumba vile.Kachanua maua mazuri na safi , kwa sasa yamekauka. Hakuwa na nia ya kujenga mji na sasa anataka mji kwako .Kijana foundation ni jambo la msingi.kaanza kwingine atamalizia hukohuko haijarishi anawaza nini.
  Utusamehe makosa yetu....safi sana.Lakini asikutie kishawishini.
  Mwombe Mungu akuokoe katika maovu ambayo anaweza kuwa amebeba.
   
 5. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  At times we men, acustom women to do sex perpetually b4 marriage, and at the end of the day we are the first to subject the complaints.
   
 6. adakiss23

  adakiss23 JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 3,346
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Mkuu achana nae. Umenikumbusha story flani. Kuna demu m1 mkikuyu tulisoma pamoja high school shule flani (nje ya tanzania). Alinivutia sana. Mzuri Mpole nk. Baada ya muda nilihamishiwa campus nyingine ya shule hiyohiyo na yeye alibaki palepale so kuonana ikawa ngumu kidogo. Mpaka siku namaliza high schoo pale sikuwa na mawasiliano nae. Kila mtu akarudi kwao. Mi tanzania yule demu kenya. Baada kama ya miaka 4,5 hivi.. Jamaa flani walianzisha group ya ile shule facebook. Wengi tulijiunga. Its was rly fun.. Sharin experience bak then wit ua OB's n OG's. Hamadiii! Yule binti nikamtuka ktk lile grp akanikumbuka. tunaanza kuwasiliana fresh. kuna tym nlkw likizo. Nkaamua kwenda nairobi. Mbali ya mengineyo yaliyonipeleka mojawapo alikuwa yule binti. Alikuwa anamalizia chuo Jomo Kenyatta Univ Of Scince n Tech. Nilifika hadi kwake maeneo ya Juja thika road uko cz alikuwa anakaa off campus. Alipokea vizuri sana. Yaani nilienjoy sana kuwa kwake pale. Had a gr8 tym yaan. W'end alinipeleka kumuona mama yake. Bi mkubwa wake alifurahi sana. Alinipenda inshort. Basi mi nikarudi zangu tz. Tukawa tunawasiliana daily via simu, fb, texts. Baada kama ya miezi 6, akabadilika. Nikimpigia simu hapokei. Mara akipokea tone inakuwa tofauti na ilivyo as if amelazimishwa kuongea na mimi. Nakumbuka kuna week flani nilimpigia siku hakupokea kabisa. Nkajiuliza kuna nn? Sikupata jibu. Nkauchuna. Zikapita week kadhaa. Siku moja niko online fb. Sina hili wala lile. Naona ktk profile yangu pale ktk category ya friends u might knw jina lake n prof pic yake. Eeh! Nilishtuka sana. Fasta nikachek Kumbe ameni-unfriend aisee.. Mmmh! Sikuwa na jibu la moja kwa moja. Nkapiga moyo konde nkampigia simu. Akapokea. Straight nkamuuliza mbona umeniunfriend fb? Akanijbu am sry its a long story. Nkakata simu nkaachana nae cz mwanamke akisema its a long story basi ujue kuna mengi hapo katikati. Nkamtoa kichwani. Nkaendelea na life yangu. Baada kama ya miezi kadhaa. Nkakuta missed cal yake cz nlkw mbali na simu. Nkamflash. Akapiga. Akasema ananisalimia tukaongea kidogo. Akawa anasema sry kwa kuniunfriend. Mi nkataka kujua sababu. If its worthy it ama la?? Akaniambia niende online fb ataniambia wit 1 condition aniadd tena then baada ya kuniambia ani unfrnd tena. Nkaona sio issue ngoja nijue sababu. Nkaingia online tukachat. Ila sababu hakutoa akawa anajikanyaga kanyaga 2. Tukaachana. Akaniunfriend. Mambo yakaisha. Ukapita mwaka m1 mara siku ntaona request yake. Nkaipotezea. Akarequest tena na akaniibox pls kubali request yangu. Cz she insisted nkakubali. Akaanza Am sry nyingii sijui kilipanda sijui kilishuka mambo mengi. Too bad nilikuwa nshamsahau. Ikabidi tuwe marafiki wa kawaida 2. N stl frnds mpaka sasa.

  So mkuu achana nae.. Kutakuwa kuna jamaa nyuma ya pazia. Baada ya kuumizwa uko anataka kuja kwa ili uwe crying shoulder. Hana mapenzi ya kweli kabisa.

  Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,265
  Trophy Points: 280
  Umeshasema havutii tena, unamtaka wa nini tena?
   
 8. Tigga Mumba

  Tigga Mumba JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 747
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Dah! Ngoja nitafakari sana leo, mida ya mchana nitakuja na ushauri.
   
 9. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mkuu hawa viumbe huwa wanarudia hizo tabia akishakuwa na uhakika lakini uwezekano wa kutulia upo. Anyway, my worry ni jinsi wewe unavyojisikia kuhusu yeye. Kama unampenda, nenda naye taratibu huku ukijaribu kumuelewa taratibu. Sometimes these people are complicated!!
   
 10. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,231
  Trophy Points: 280
  sasa kama hakuvutii tena ushauri wa nini?
   
 11. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,351
  Likes Received: 2,693
  Trophy Points: 280
  Fuata ushauri huu...sikiliza moyo wako vile wakuambia
   
 12. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,105
  Likes Received: 11,257
  Trophy Points: 280
  kumbe ulisoma Maua Seminary? Hata mimi pia.
   
 13. Mgibeon

  Mgibeon JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 7,443
  Likes Received: 9,092
  Trophy Points: 280
  Pumbavu sana..! Kuna mwanangu mmoja alikuaga ktk mahusiano na mdada mmoja tangu wapo O'level, ikifika kipindi mtoto akachange akamwambia eti yeye anaangalia future ka' vipi wa' break up...! Basi jamaa akampotezea even though he real loved the dada..! Sasa tukiwa chuo ile last year(mdada aliishia form 4) mdada akaanza kujileta, eti anasema yule jamaa hataki tena kumuoa, akaleta story nyingi mradi awe na mshikaji wangu! Nikamshauri mshikaji nikamwambia kua she is looking for greenpastures, so tukitoka hapa chuo then ukaingia katika life maisha yakakupiga tena bila kua na regular income atakutenda tena... Jamaa akampotezea, saivi nasikia kazalishwa watoto wawili kila mmoja ana baba yake..!! NOW; Temana naye tu huyo mtoto, ulieyeokota naye kuni ndo huyo anaefaa kuota naye moto, she is after something.... Fanya mambo yako, mjinga tu huyo mdada.
   
 14. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,947
  Trophy Points: 280
  kuna thread sijui nani aliileta ila inasema kuwa ukiona unapendwa sanaa jua kuna mtu kaumizwa ama kaachwa huko
   
 15. Mpangamji

  Mpangamji JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2012
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 536
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkuu piga chini fasta, keep distance. Epuka kutumiwa na hawa mabinti ma-oportunistic. Utajuta, kimbia
   
 16. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,407
  Trophy Points: 280
  Kama mbwai mbwai alivyokua kigori katumia na njemba nyingine leo amekua mzee anataka akushushie zigo mtoto wa watu...Achana naye hana issue atakuja kukusumbua tena!!!
   
 17. K

  Kipimbwe JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  We mzee wa Makk niaje,Temana nae huyo kwanza hata wewe ni ngumu kuwa haukuchovya kwingine kutokana na ulaku wako wa awali.Unajua Brk ulishindwa utawa ukapiga mashine vibaya haikuridhika ikakutema,chakufanya tafuta kitu mpya chali yangu,msamehe na umsaidie mambo zingine kama mtz mwingine.
   
 18. A

  Absine Member

  #18
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Temana nae hakufai hata kidogo.
   
 19. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #19
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  hayo ndo matatizo ya long distance relatnshp, mwanamke kwa asil anahitaj smbody 2lean on cyo mtu wa kuchat kwenye cm ama facebk.wewe ukiwa mbal na blahblah zako kwenye cmu akatokea mwenzio kuwa available physicaly lazima uwekwe kando.kwann ajipe ma2main ya uwongo wakat mwanaume especialy wengi wa kitz hawaaminik? Ni wachache wanaohimil lmg distanc relatnshp binafc camin ktk kwayo
   
 20. V

  Von Mo JF-Expert Member

  #20
  Oct 5, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 1,830
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Kimsingi kuna KITU nimegundua:
  HUMPENDI TENA HUYU DADA KWANI TAYARI UMEONA MAPUNGUFU YAKE., KWAMBA HAVUTII TENA, HII INAMANISHA WAPO WAKUVUTIAO ZAIDI, BASI USIMCHELEWESHE MWAMBIE UKWELI ITS TOO LATE..........KWISHA HABARI YAKE.

  NDIYO MANA MIMI MPAKA KESHO NIKIONA MWANAMKE KATENDWA SILAUMU KWANI WANAUME WENYE NIA TUKIONESHA KUWAJALI WANATUONA MABOGASI, ACHAPE LAPA..............
   
Loading...