Demokrasia yazidi kuadimika CHADEMA; Mbunge Zenji asakamwa kila kona!

Maramla

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
581
642
BREAKING NEWS!!!!!!

DEMOKRASIA YAZIDI KUADIMIKA CHADEMA; MBUNGE ZENJI ASAKAMWA KILA KONA!

Kama ilivyotabiriwa, siku chache tu baada ya kurejea madarakani, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ameendelea na utawala wa kiimla ndani ya chama hicho.

Kama mnavyojua leo Mbunge wa Chama hicho Mariam Msabaha (Viti Maalum) amechangia mbele ya Rais Magufuli Visiwani Zanzibar akiwa mmoja wa viongozi waliohamasika kuwatunza vijana walioimba na kuhamasisha uzalendo.

Rais alikuwa akifanya uzinduzi wa hoteli ya kisasa ya kitalii ya Verde inayomilikiwa na Said Bakhresa.

"Tukisema hiki chama ni genge la wahuni ndio wanachama wajue; Dada Mariamu leo hana raha. Amesakamwa sana mitandaoni na kwa kupigiwa simu na viongozi ndani ya chama," amesema mmoja wa wanachama wa Chadema.

Hata baadhi ya viongozi wa juu na wabunge wa Chama wameshiriki waziwazi kumzodoa. "Yani ndani ya CHADEMA hakuna uhuru wa kufanyakazi, hakuna uhuru wa maoni, hakuna uhuru wa kufanya siasa, ili uwe mwema ufuate kauli za Mbowe na genge lake la kina Heche, Lema, Boniface na wengine wanaoamua mambo na ususe hata jambo la kitaifa au la maana likifanyika katika eneo lako," aliongeza.

Mariam licha ya kuchangia aliitwa kumsalimia Rais Magufuli na wakataniana.

Jambo ambalo hata katika shughuli nyingine wabunge mbalimbali wa Chadema aidha wamewahi kuitwa kushikana mkono na Rais (Lema na Mbowe) au wameshiriki katika matukio ya kitaifa kama vile ufunguzi wa miradi lakini ukitoka kwenye "Chadema inner circle" haina shida.

"Udikteta unaonekana kuimarika kila siku hasa sasa ambapo ndani ya Chama ni kama vile hakuna Katiba, hakuna miongozo, ni mawazo ya Mbowe na genge lake ndiyo yanaendesha chama."


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
BREAKING NEWS za kutekwa watu na kupigwa risasi ndani ya nchi hii mbona hushangai..?
Umbea utawazika wengi maganda nyie
 
Ila kwa yote hayo cdm wajenge ofisi ya maana asee,waache porojo porojo.

Mimi huvutiwa na appearance nzuri ndipo ufanya maamuzi kuingia au lah..!
 
Back
Top Bottom