Elections 2010 Demokrasia yangu

Alwaz

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,099
10,794
Ikiwa hali ndizo hizi,chaguzi za nini?.
Hivi tunavyoandika chaguzi zenye mizozo ziko Haiti,Misri na Ivory Coast.
Unajua haya mambo ya uchaguzi yana gharama mno,kuanzia mali mpaka muda na afya.
Ikiwa kila siku tunaingia gharama hizo mwishowe matokeo huamuliwa mezani.Ni afadhali tutafute utaratibu mwengine wa kupata viongozi.
Utaratibu ninaopendelea mimi ni:
1. Kuwepo tume maalum inayopokea maoni ya raia na kuyaweka kwenye mtandao kila siku.Raia watasema mtu anayefaa kuongoza baada ya miaka mitano ni fulani na sifa zake ni hizi......Raia wakileta kasoro za mtu huyo tume ambayo itakuwa chini ya taasisi ya bunge itakuwa na taratibu za kufuatilia na hatimaye kuja na jawabu ambayo inaweza kukatiwa rufaa na raia au mhusika mwenyewe ili kusafisha heshima yake.
2.Kiongozi aliyeko madarakani kwa utaratibu huu,iwapo raia wataendelea kuridhika naye hakutokuwa na ukomo wa uongozi.
3.Demokrasia hii ambayo inaweza kuitwa Ami's Democracy (ADE) itakuwa Iko kati na kati baina ya ufalme na demokrasia ya nchi za magharibi inayotesa sasa hivi.
Faida ya ADE ni kuwa gharama za kuendesha nchi zitakuwa chini sana.Fedha na muda vitatumika kwenye mambo ya mendeleo kiuhalisia.
Hasara ya utaratibu wa sasa kwanza ni fedha zinatumika nyingi kwa vipindi vifupi vifupi.Wanaofaidika ni waasisi wa demokrasia kwa kuuza karatasi,wino,masanduku na kadhalika.Raia wa nchi nyingi wanagombana pasi na ulazima.Wanapoteza muda na afya zao bure

Kauli mbiu ya demokrasia yangu ni UCHAGUZI DAIMA!.
 
Watu wabunifu huja na ufumbuzi wakati wa matatizo.Sisi waafrika ni watu wa kushabikia fikra za watu wengine daima.
 
Kwa utaratibu huu wa demokrasia yangu,kungekuwa na vituo vingi vya kutolea maoni kote nchini kadri tume itakavyoona inafaa.Kila kituo kingewahusisha idadi maalum ya raia.
Kituo kama hicho kingekuwa na akaunti yake NEC.Maoni ambayo yangepewa nafasi ni yale tu yatakayopitia akaunti hizi pekee.

Kwa demokrasia hii,mgombea mwenye tatizo lolote lenye kuvunja heshima ya kuwa kiongozi hawezi kufikia kiwango cha kupata umaarufu kwani matatizo yake yatajulikana mapema.
Namna nyengine ambavyo demokrasia hii inafanya kazi ni kuwa mtu ambaye yuko madarakani,iwapo vituo vingi vitaonesha kutoridhishwa naye kwa jinsi ambavyo ataoneshwa kasoro zake na tume ikaridhika na tuhuma hizo, basi ataondoka madarakani mapema bila gharama yoyote.
 
Labda kwanza tuweke mfumo wa kumpata mwenyekiti wa NEC na timu yake vinginevyo itakuwa mambo yale yale ya uchakachuaji. Shida ni tume zinazochaguliwa na watu wale wale wenye malengo yale yale.
 
Nimepata wazo kuwa tuwachane na jina la NEC.Waonaje tukatafuta jina jengine.Hiyo kitu ikawa chini ya bunge badala yake?.
 
Back
Top Bottom