Demokrasia ya Uingereza, Uchaguzi wa Meya na Mahitaji ya Wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Demokrasia ya Uingereza, Uchaguzi wa Meya na Mahitaji ya Wananchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by George Kahangwa, Apr 20, 2012.

 1. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ifikapo tarehe 3 Mei, 2012 waingereza kwa mara nyingine tena watapiga kura kuwachagua Mameya wa miji mbalimbali ya nchi hii. Tofauti na ilivyo nchini kwetu Tanzania, ambapo viongozi hawa huchaguliwa na madiwani wenzao, hapa UK wapigakura wanashiriki moja kwa moja kuamua akina nani washike nafasi hizi za uongozi. Tofauti nyingine ni kwamba hata raia wa kigeni walioko hapa hususan wanaotoka katika nchi wanachama wa jumuiya ya madola ni ruksa kushiriki uchaguzi huu kwa kupiga kura.
  Naam, hata mimi nitapiga kura, ama kwa kwenda kituoni, au kwa njia ya posta, au kwa kumtuma mwakilishi wangu (lakini katika njia hizi mbili za mwisho ilinipasa kutoa taarifa mapema), na kama siku yenyewe ya kupiga kura nitapata dharula kwa mfano kuugua ghafla, ruksa kutuma mtu aniwakilishe.
  Utaratibu huu unalenga kuhakikisha haki ya mtu kumchagua kiongozi haipotei. Je, Tanzania inaweza kuumudu utaratibu huu, au wachakachuaji ndio kwanza watapata fursa pana!?
  Aidha, kabla ya kura kupigwa wagombea wanapata fursa ya kujieleza mbele ya wapigakura, matharan kwa njia ya mdahalo wa pamoja.
  Hivi leo katika jiji la London kwa mfano, wagombea watatu; Bw. Boris Johson wa chama cha Conservative (ambaye ni meya wa sasa anayeomba kuchaguliwa tena), Bw. Ken Livingstone wa chama cha Labour, na Bw. Brian Paddick wa Liberal Democrat waliwekwa kitimoto na wakazi wa jiji hilo. Nilipata fursa ya kufuatilia mdahalo huu. Nimevutiwa zaidi na jinsi wananchi walivyokuwa wakiuliza maswali ambayo moja kwa moja yanagusa kero na mahitaji yao halisi katika jiji. Yaani wananchi kwa maana hiyo ndio watoa maeneo ya sera, na mgombea wajibu wake ni kueleza ni nini atafanya katika eneo tajwa.
  Ni mdahalo ambao umenipa hamu ya kuona kwamba hata watanzania walio wengi, tungepata sio tu fursa ya kuwachangua Mameya wetu bali pia tunatoa maeneo ya sera kwa njia ya kuwauliza wagombea maswali. Kama lingekuwa jiji la Dar es Salaam kwa mfano, wagombea wangeulizwa ni nini watafanya katika;
  · Kumaliza tatizo la msongamano wa magari barabarani, ajali za bodaboda, ubovu wa barabara, nk.
  · Kuondoa uchafu wa jiji
  · Kukomesha mafuriko ya kila baada ya mvua moja tu
  · Kukomesha mgawo wa giza
  · Kudhibiti kero za ujenzi holela, mitaa isiyopitika, baada na kumbi za starehe zenye kelele usiku wa manane katika makazi ya watu, nk.
  · Kudhibiti utapeli wa viwanja na uvamizi wa maeneo ya wazi
  · Na mengine
  Pengine ipo haja ya kuidai hii haki yetu ya kuwachagua Mameya. Yamkini si vibaya kulifikiria hata hili tunapoelekea kuandika upya mwongozo wa nchi yetu (Katiba Mpya)
   
Loading...