Demokrasia ya Tanzania si sawa na demokrasia ya China wala Marekani

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
DEMOKRASIA YA TANZANIA SIYO YA CHINA WALA MAREKANI.

Na Elius Ndabila
0768239284

Kufananisha demokrasia ya Tanzania na nchi za USA, UK, CHINA, KOREA ni kuikosea Tanzania. Tanzania ni nchi ambayo haifungamani na Ubepari Wala Ujamaa.

Huwezi kusema Tanzania kunaminywa demokrasia kwa kurejea rejeo ya Demokrasia ya USA au UK. Hapo utakuwa unajaribu kufananisha ladha ya maji na Chai. Kunatofauti kati ya Mataifa ya Kibepari, Kijamaa na yale yanayochanganya Ubepari na Ujamaa.

Ikumbukwe kuwa Dunia hii uchumi na utawala unaendeshwa zaidi na makundi hayo Matatu. Kundi la kwanza Ujamaa, kundi la pili ni Ubepari na kundi la tatu ni kundi ambalo ni Ubepari Ujamaa.


Nchi za Kibepari ambazo watu wanajaribu kulinganisha Demokrasia yao na Tanzania wao moja ya elements ya demokrasia ni lazima kuwe na mfumo wa vyama vingi element ambayo hata Tanzania tunayo. Wanapata viongozi wao kwa kushindanisha sera za vyama. Moja wapo ya nchi hizo ni Marekeni, Uingereza, Canada n.k.Pia katika nchi za Kibepari wanaamini katika Uhuru wa vyombo vya habari. Wakatik katika nchi za kijamaa wao kunakuwa na chombo kimoja Cha habari kinachotoa habari za nchi. Vyombo vingine havina mamlaka hiyo mpaka vipate ridhaa ya serikali.

Kwenye nchi za kibepari wanaamini katika uhuru wa kuzungumza. Kwenye ujamaa uhuru upo lakini si Kwa kiwango kikubwa. Uhuru unadhibitiwa na serikali.


Ninajaribu kukutoa huko ili kuondoa dhana inayojengwa na Wapinzani wa CCM inayosema Tanzania kuna uminywaji wa Demokrasia. Ukisoma mpaka mwisho utakuwa umepata dhana kamili ya Demokrasia na utakuwa na majawabu ya Demokrasia ya Tanzania.


Nchi za kijamaa zenyewe haziamini katika demokrasia ya Vyama vingi. Nchi hizi zinaamini katika kuwashindanisha watu na siyo vyama. Watu wanashindana na kupata mtu mmoja bora atakayewaongoza. Kumbuka kwenye ubepari tulisema lazima kuwe na multiparty system. Moja ya nchi ambazo zipo kwenye ujamaa huu ni Korea kaskazini, China, Urusi n.k. Hivyo ni ngumu kufananisha demokrasia ya Ujamaa na Ubepari.

Maendeleo kwenye ujamaa yanalenga kuwa na viwanda ili kujenga uchumi, wakati kwenye Ubepari wanaamnini kwenye kujenga empire ya uchumi wa mtu mmoja.

Halikadharika, kwenye Ubepari wanasistiza mfumo wa Vyama vingi, Demokrasia na kuunda serikali kwa matakwa ya umma. Ujamaa wao kuna asili ya udikiteta. Hawaruhusu demokrasia Kwa kuwa wanaamini inachelewesha maendeleo. Wanaamini kwenye kula keki ya nchi pamoja na kufanya kazi pamoja.

Turejee Tanzania. Wanaotaka Tanzania kuendeshwa kama Marekani au Uingereza wanakosea. Lakini hata wanaotaka Tanzania kuendeshwa kama China wanakosea.

Ukiisoma viziri Katiba ya Tanzania ambayo ndiyo Sheria Mama haiitaji Tanzania kama nchi ya Kijamaa au Kibepari. Tanzania haifungamani na upande Wowote. Si ujamaa wala Ubepari. Tanzania ina elements za Ubepari na Ujamaa. Hivyo kuwa na dhana mbili Kwa pamoja ni vigumu ku-adopt elements zote za kijamaa au za kibepari.

Kwa mkutadha huu, Demokrasia tunayoifuata ni sahihi kabisa kutokana na sheria za nchi yetu ambazo msingi wake mkubwa ni mila na desturi ya nchi yetu.

Kwa mkutadha huo Tanzania si nchi ya kibepari wala kijamaa. Ni nchi ya katikati yaani NAM. Nchi zote ambazo zipo Chini ya Mstari wa Ikweta hazifungamani na mfumo wa Kijamaa Wala Kibepari. Zina mfumo wao tofauti kabisa wa kuendesha nchi.

Tafakuri.
 
China sio na hajiwahi kuwa nchi ya kidemokrasia, China ni nchi ya kidikteta ya chama kimoja cha kikomunisti. Kwa nini nyie wachumbuzi uchwara kila mara mnarudiarudia huu upotoshaji?!
 
Back
Top Bottom