Demokrasia ya Malawi kuelekea Uchaguzi Mkuu

moyafricatz

JF-Expert Member
Nov 27, 2015
2,900
4,865
Nimetafsiri kutoka kwa dada Maria Mhandire wa Lilongwe.
____________
Wanaodhani Afrika nzima haina demokrasia waje wajifunze Malawi. Nadhani sisi ndio nchi ya kwanza kwa demokrasia Afrika na tuna mengi ambayo hata wazungu walioanzisha demokrasia wanaweza kujifunza. Kwa wale wasio wakazi wa Malawi ngoja niwaeleze hali ilivyo hapa;

Mwaka huu tutafanya uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge. Rais Peter Mutharika anagombea kwa awamu ya pili kupitia chama tawala cha DPP. Makamu wake Saulos Chilima anagombea kupitia chama cha upinzani cha UTM.

Yani Rais na Makamu wake wanagombea kupitia vyama viwili tofauti, na kampeni zinaendelea, kila mmoja akinadi sera zake. Wakikutana kwenye matukio ya kitaifa wanakaa pamoja kama Rais na Makamu wake. Baada ya hapo wanakutana majukwaani wakipingana kwa hoja.

Mutharika na Chilima walikua chama kimoja cha DPP. Lakini mwaka jana wakatofautiana. Chilima akajiondoa na kujiunga na chama cha upinzani cha UTM. Hakupoteza nafasi yake ya Umakamu wa Rais, maana Katiba ya Malawi inaruhusu kiongozi kuhama chama bila kupoteza nafasi yake ya uongozi.

Mgombea mwingine ni Atupele Muluzi, Waziri wa ardhi ambaye anagombea kupitia chama cha upinzani cha UDF. Rais Mutharika hajamfukuza kazi. Kamuacha aendelee na kampeni za Urais akiwa bado Waziri wa ardhi. Demokrasi ya hali ya juu.

Rais wa zamani Joyce Banda nae anagombea kupitia chama chake cha PP. Licha ya tuhuma za ufisadi zinazomkabili, lakini Rais Mutharika ameruhusu agombee akisema wananchi ndio watakaoamua.

Mgombea mwingine ni Lazarus Chakwera wa MCP. Hiki ndio chama cha ukombozi cha Malawi. Ndio chama cha Rais wa kwanza Hastings Kamuzu Banda.

Kampeni zinaendelea. Hakuna vurugu, kakuna fujo, hakuna polisi wanaopiga raia. Hakuna drama za kijinga za polisi kuvuruga mikutano ya wapinzani kwa taarifa feki za kiintelijensia.

Wanaotaka kuandamana wanaandamana, Wanaotaka mikutano ya hadhara wanafanya. Wanaotaka vikao vya ndani ewala. Ili mradi kila mmoja anatumia njia yake kushawishi achaguliwe.

Raia wa Malawi tunaendelea na maisha yetu kama kawaida, tukila Nsima (ugali) na kusikiliza sera za kila mgombea. Ni mataifa machache sana duniani yanaweza kuwa na kiwango hiki cha demokrasia. Tunajivunia nchi yetu.!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom