Demokrasia ya 'Kamati Kuu kuamua' ni aina nyingine ya Udikteta, tuupige vita

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,602
Yaani mfano Wanachadema au WanaCCM wa jimbo la Mchinga huko, wameamua kumpitisha mtu wao aende akagombee, halafu eti mwisho wa siku eti hichi kitu kinaitwa 'Kamati kuu' kinakaa na kuamua tofauti, eti ya kwamba aliyepitishwa kwa kura na wana Mchinga, hafai, halafu wanaamua kumpa nafasi mwingine aliyeshindwa kwa kura na yule aliyekatwa

Hakuna upuuzi wa demokrasia kama huu, ni UHANANGWA kama anavosemaga Baba Levo.

Yaani hao kamati kuu waaamua kuwadharau wana Mchinga, kuwaona kwamba hawana akili ya kumchagua waliyemchagua

Mbaya zaidi, unakuta hao wanaojiita kamati kuu, unakuta hawana uelewa wowote wa siasa zinavoenda jimbo la Mchinga.

Kama kuna jambo linapaswa kukemewa vikali ni hili la chombo kinachoitwa kamati kuu, kuchagua wagombea wa ubunge.

Waliopigiwa kura wapitishwe kugombea, hakuna haja ya kuanza kuleta ujuaji wa mambo wa kumkata aliyeshinda kwa kura kwamba hawezi, kama angekuwa hawezi ni kwanini amepigiwa kura?

Waliopitishwa kwa kura, wakawakilishe waliowapigia kura. Huu udikteta wa sijui 'Kamati kuu' nayo pia itakaa ni udikteta wa kukemewa.

N.Mushi
 
Pia nashauri wabunge waliotumikia jimbo miaka 10 wasitaafu au watafute majimbo mengine make inatengeneza mazingira fulani ya kuchokwa, ujumbe huu uwafikie Lema, Mbowe, Sugu, Mdee na Msigwa na wengineo wa CCM.
Absolutely, naunga mkono hoja, ila kuwepo na mtu sahihi anayeweza kweli kweli wa kubadilishana kijiti.. sio tu kuachia madaraka kwa mtu asiyeweza huo ni ujinga
 
Back
Top Bottom