Demokrasia ya furugano ili kwenda ikulu - demokrasia isiyo na mipaka- uchu bila ushauri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Demokrasia ya furugano ili kwenda ikulu - demokrasia isiyo na mipaka- uchu bila ushauri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkwawa, Oct 7, 2012.

 1. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,290
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 160
  Raisi Kikwete aliusaka uraisi tangia mwaka 1995 mpaka alipoupata mwaka 2005. Raisi Kikwete akiwa kwenye harakati za kuusaka huu uraisi alijenga makundi nadani na nje ya chama chake ili kushinda huu uraisi. Alisahau jimbo lake la chalinze na kufikiri kwamba amemaliza kazi ya kuliletea maendeleo. Alikataa ushauri wowote ule ulikokuwa unamwelekeza kutokwenda Ikulu ama kwa uwezo au kwasababu yeyote.

  Harakati zake zilimfanya kuhakikisha ananunua wahariri wa habari kwa fedha au ahadi na kuunganisha nguvu na akina RA EL nk. Kwa kutumia neno demokrasia akaingia ikulu huku akiwa ameacha majeraha mengi sana ndani ya chama chake na nchini.

  Kwenda ikulu kwa uchu kama huku kumeifanya serikali yake kuzalisha mafisadi ambao waliiba kwa miaka zaidi ya mitano kabla hajaingia ikulu ili kuwezesha wao kama kundi kwenda Ikulu. Madhara yake ni EPA, kagoda, deeepgreen nk

  Madhara mengine ni nchi inakuwa masikini kwani walioingia ikulu walitakakufanikisha tu matakwa yao kwani hawakuingia kitaasisi bali waliingia kama kijikundi chenye malengo yao wenyewe. Ndio maana walipoingia tu ikulu waligawana madaraka ya serikali na chama kama genge la watu wachache. Walihakikisha sehemu zote nyeti wamewekana wenyewe mfano RA alipewa uweka hazina wa Chama na EL waziri mkuu na wengine kama walivyokubaliana, vikao vya chama, sera na ilani ya uchaguzi ikawekwa kapumi kwani deal done. Urais wa mtu mmoja huo.

  Tafakari na chukua hatua mapema.

  Chief Mkwawa wa Kalenga
  Dharau ya vijana kwa wazee itawamaliza
   
Loading...