Demokrasia ya bunge na uamuzi kwa kwa njia ya kelele | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Demokrasia ya bunge na uamuzi kwa kwa njia ya kelele

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kimbunga, Jun 21, 2011.

 1. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Nimekuwa nikijiuliza kuhusu maamuzi ndani ya Bunge ambapo maamuzi mengi hutolewa kwa kuuliza walioafiki wanasema ndiyo na wasioafiki wanasema hapana. Kiongozi wa shughuli za bunge wakati huo (Spika, Naibu Spika ama Mwenyekiti) hutoa uamuzi wake kwa kusikiliza sauti iliyo kubwa kati ya Ndio na Hapana. Nadhani huu ni utaratibu wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola (Westminster) kwa sababu hata majuzi nilikuwa naangalia Bunge la Kenya wakati wa kuwapitisha CJ, Deputy CJ na DPP nao pia walitumia utaratibu wa kupiga kelele za ndiyo na hapana. Bunge linapitisha maamuzi makubwa ya mustakabali wa Nchi lakini utaratibu wa kupitisha maamuzi haya kwa kupiga kelele huwa mimi unanishangaza sana. Hivi kwa ajili ya kudumisha demokrasia haujafika muda muafaka kwa Bunge letu ama Mabunge yanayofuata utaratibu wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola kufuata utaratibu wa kura ya siri kwa kila uamuzi ambao unatakiwa kufanywa na Bunge?
   
 2. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  yaani hata kwenye vikao vya madiwani kuna demokrasia zaidi.
  inabidi ifike mahali tubadilike.
   
Loading...