JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 625
- 938
Demokrasia katika nchi nyingi za Afrika imekuwa ikilegalega kutokana na Sheria ambazo Bunge linatakiwa kumtii Rais hali inayopelekea Marais kutengua Katiba na kujiongezea muda wa kukaa madarakani.
Suala hilo la kubadilisha Katiba kwa kuondoa ukomo wa muda au umri wa Urais linafahamika kama Mapinduzi ya Katiba (Constitutional coup) na ni maarufu sana kwenye nchi za Afrika huku likiwa kikwazo kikubwa cha Demokrasia.
Marais ambao wamebadilisha Katiba za nchi zao kuondoa kikomo cha mihula miwili baadhi yao ni pamoja na Gnassingbé (Togo), Museveni (Uganda), Déby (Chad), Biya (Cameroon), Kagame (Rwanda), Hayati Nkurunziza (Burundi), el-Sisi (Misri) na Sassou (Brazavelle).