Demokrasia si mazingaombwe

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,685
1,111
Mazingaombwe kila kona ya nchi,sasa nimeielewa ile kauli ya kuhakikisha upinzani unatokomezwa kabisa. Dalili ziko wazi,vyombo vya serikali kwa maana nyingine vyombo vya umma vimegeeuzwa kuwa jumuiya za CCM,hatari ninayoiona hapa tusipokuwa makini na kusimamia haki na kuiona ikitendeka tutaliangamiza taifa.

Sisi tutaandika kama kawaida kuhakikisha tunakosoa kila hatua yenye lengo baya kwa mustakabali wa amani ya nchi yetu,kilichotokea jana bungeni ni mwendelezo wa kutekeleza demokrasia kwa njia ya maigizo,lakini ukweli wake unaendelea kuwa demokrasia bado sana iko shimoni.

Athari ya demokrasia kuonekana shimoni ikitafuta Uhuru ambao kwa lugha rahisi,Uhuru wa bendera ni pamoja na kuitekeleza demokrasia hiyo kwa njia ya vitendo kwa kuvikwa joho la demokrasia ilihali matendo yote yanaashiria ukiukwaji wa misingi yenyewe ya demokrasia. Mbaya zaidi hata chombo chetu cha utungaji sheria kimeshindwa kuyaona makunyanzi hayo kwa kuendeleza misingi ya ushabiki huku rasilimali za taifa zikiendelea kutumika kuwalipa posho na mishahara.

Athari kubwa ni pale bunge linapotaka kuwachagulia wawakilishi wa upinzani kugombea nafasi za ubunge wa EALA,wawakilishi watakiwao na chama tawala kwa maelezo ya vikao vyama chama kwa kutumia mwamvuli wa demokrasia. Mathalani,mwakilishi toka chama cha CUF Habib Mnyaa,alishafufukuzwa uanachama na vikao halali vya chama hicho hali inayomuondolea sifa ya kuwa mwakilishi japokuwa ameendelea kuwa mwanachama wa msajili wa vyama vya siasa kwa jina CUF,lakini bunge leo limemthibitisha na kumchagua kuwa mbunge wa EALA na kumuacha MH. Taslima ambaye ni mwanachama halali kwa minajili ya kudhoofisha nguvu ya CUF na kuimarisha nguvu ya CUF-msajili.

Hakuna asiyejua kesi ya msingi iliyoko mahakamani ya CUF dhidi ya Lipumba na wafuasi wake,lakini iweje Leo chombo hicho cha kutunga sheria kivae miwani ya mbao na kufumbia mazingaombwe hayo. Vyama vya Upinzani vipo kwa mujibu wa sheria njia pekee ya kuvifuta ni kupeleka muswaada bungeni ili kuifuta sheria inayoruhusu uwepo wa mfumo wa vyama vingi nchini. Lakini pia kama wanataka kudhoofisha nguvu ya kisiasa ya upinzani wajikite kwenye nguvu za hoja na si kupandikiza migogoro kwa kujificha kwenye mwamvuli wa demokrasia.

Sijasikia sheria na kanuni za uchaguzi ndani ya bunge zikizungumzia mshindi wa uchaguzi ndani ya bunge atapatikana kwa jinsi ipi,ila kwa mujibu wa katiba ya JMT Rais, wabunge na madiwani hupatikana kwa njia ya simple majority leo bunge letu linapo ruhusu kura za maruhani wanamkomoa nani au walikuwa wanapitisha muswaada kwa kura za ndiyo au hapana.

Bunge libaki kama mhimili unaojitegemea kwa kutekeleza majukumu yake ili kulinda hadhi na madaraka yake. Bunge linapaswa kurejea kesi ya ubunge wa EALA iliyofunguliwa na mh. Komu na Matokeo ya hukumu ile.
 
Maslahi ya nchi ni zaidi ya vyama,vyama vinapita lakini nchi inabaki kuwa Tanzania
 
Back
Top Bottom