Mati Mkenda
Senior Member
- Mar 4, 2018
- 171
- 211
Kuna wakati wakati kampeni za haki sawa kati ya Mwanamme na Mwanamke zilipoanza, wanawake wengi walizichukua katika muktadha tofauti kabisa na kile kilicholengwa. Walidhani kuwa huo ndo ulikuwa muda muafaka wa kufanya kila kitu ambacho wanaume walikuwa wakifanya hata kama kilikuwa kibaya. Kama Baba alichelewa kurudi nyumbani, Mama naye alitaka achelewe kurudi nyumbani eti kwa sababu ni haki sawa. Ukweli ni kuwa hawakujua wanataka nini hasa katika hizo haki sawa.
Katika uringo wa siasa nao hakuna tofauti. Mara nyingi tumeshuhudia vyama vya upinzani vikionesha kuwa haki imetendeka pale tu ambapo uamuzi au matokeo fulani yanakuwa in their favor. Hapo ndipo wao wanaona kuna haki au demokrasia ya kweli.
Kwa mfano hivi karibuni wapinzani wameitumia sana nchi ya Malawi kama ndiyo nchi ya kuigwa in terms of democracy mara baada ya Dr. Lazarus Chakwera kutoka chama cha MCP kuchaguliwa kama Rais. Wameona kuwa hiyo nchi ndiyo yenye demokrasia eti kwa sababu upinzani wameshinda.
Hapa najiuliza. Hivi inakuwaje upinzani wao waone kuwa haki au demokrasia ipo pale tu wanapofaidika wao? Je, kukubali kushindwa nako hakuwezi kuwa ni sehemu ya demokrasia wanayoitaka? Je, wanajua nini hasa wanakitaka kama sehemu ya demokrasia wanayoililia?
Wahenga walisema, “Asiyekubali kushindwa, si mshindani”. Kauli hii ya Wahenga kwa kiasi kikubwa inabeba maudhui ya maana neno Demokrasia. Vyama vya upinzani mjifunze kuwa kushindwa kwenu ni sehemu ya demokrasia hiyo hiyo, maana washindani wenu nao wanashukuru kama ambavyo mngefanya nyie iwapo mngeshinda.Hivyo, kushindwa nako ni sehemu ya demokrasia mnayoitaka.