Demokrasia ni tunda zuri, tulienzi litatusaidia kwa maendeleo ya tanzania. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Demokrasia ni tunda zuri, tulienzi litatusaidia kwa maendeleo ya tanzania.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WEMBE WENGE, Sep 15, 2012.

 1. W

  WEMBE WENGE Senior Member

  #1
  Sep 15, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 127
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wana JF
  Nimeona na mimi nitoe maoni yangu KWA MUSTAKABALI wa Demokrasia hapa Tanzania,
  Tunda la Demokrasia ni wananchi kuwachagua viongozi kwa uhuru, haki, na usawa, wanaoamini kwamba wanaweza kuwasikiliza, kuwaunganisha na kuwaongoza kuelekea kule ambako wao wanaamini ndiyo goal yao, Kiongozi ni kiungo muhimu katika kufanikisha malengo hayo.
  Wanaochagua viongozi ni wananchi na sababu za wao kufikia mamuzi ya kuwapa uongozi viongozi hao wananchi wanazifahamu na wanatarajia mrejesho fulani toka kwao.
  Wananchi wanavyo vipimo na sababu za kumchagua kiongozi fulani kwa ngazi fulani, zikiwa nzuri ama dhaifu wao ndiyo wanaomjua nani atakayefaa kuwa kiongozi wao.
  Ushawishi huru kwa njia ya kampeni ama elimu, huwa unaweza kusaidia kuongeza mapenzi ya wananchi kwa chama kuchaguliwa lakini huwa na msaada mdogo mahali ambapo wananchi wanaelewa wanakotaka kwenda na wanamjua wanetaka awaongoze kwenda huko.
  CDM wanafanya na wataendelea kushawishi, kuelimisha na kuwaunganisha wananchi wazijue haki zao na hata mpaka 2015 na hata baada ya uchaguzi kwa kuwa ndiyo moral responsibility ya CDM.
  Kushinda uchaguzi wa 2015, ndiyo goal lakini CDM lakini itakuwa champion hata kama haikushinda ili mradi tuu elimu ya demokrasia inayoitoa kwa wananchi ndiyo itakayo fanya kazi kwenye chaguzi zitakazofanyika nchini, pale ambapo uchaguzi utafanywa katika mazingira ya uhuru na haki, kwa kuwa demokrasi ya kweli ndiyo itakayochagua uongozi.
  Wakati CCM ikihangaika usiku na mchana kupika majungu ya chuki na fitina na maumbo ya kuvunja amani ya nchi kwa kutuia vyombo vya dola, (Msajili wa vyama, polisi, vyombo vya habari, TBC, Redioza serikali) propaganda kwenye mitndao ya simu, CDM inawekeza kwenye elimu ya uraia kwa mustakabali wa Tanzania ya kesho.
  Wanachofanya CDM ni kitu kidogo tuu ambacho wala hakihitaji kutafuta PHD kukijua, ni kutoa elimu ya uraia kwa wananchi ili wajitambue, baada ya kuanza kujitambua, wananchi waondokana na minyororo mizito ya ghilba ya CCM za udini, ukanda, rangi, ukabila, mauaji, vita n.k, n.k.
  CDM inaamini kuwa nchi hii ni ya watanzania na nguvu ya umma ndiyo ukombozi wao (hasa kwenye Tanzania iliyogubikwa na dhulma, uzembe, uvivu, na ghilba) CDM wameonyesha kuwa wao ni pekee wanaoweza kufill gap inayowashinda/iliyowashinda CCM.
  Kautafiti kadogo huru nilikokafanya kamegundua kwamba, CCM imekuwa ikichaguliwa si kwa kuwa wananchi wanaipenda, ila ni kwa kuwa yamejengwa na hila na ghilba ya chama cha Mapinduzi ambayo wakati wote wamekuwa wakitumia dola, rushwa na vitisho, wakati kundi dogo la wapiga kura limekuwa likichagua CCM kwa mazoea tuu kwa sababu eti ni chama kilicholeta uhuru (kurithi kutoka TANU) ama kimesomesha watu wa Tanzania (kundi hili dogo nila wazee). Demokrasia imetupwa kapuni
  Hakuna sababu yeyote ya maana ambayo CCM wanaweza kuja nayo ikawa ya maana inayowfanya wananchi waichague. Kama utakumbuka kwa nyakati na sehemu mbalimbali Nape amesikika akisema mtaji wa CCM ni wananchi wa vijijini, sasa kwa akili ya kawaida kuna mwananchi wa kijijini gani anayeweza kuichagua CCM kwa sababu gani ya maana zaidi ya mazoea, woga wa vitisho, ama Rushwa? Tuimarishe demokrasia ili wananchi wajiamini.
  CDM imejisajili kwenye orodha ya chama chenye demokrasia na mapenzi kwenye nyoyo za wananchi pale ambapo kimeweza kuwaambia dhahiri kwamba bila wananchi wenyewe kujielewa wasitarajie maendeleo, watayaona kwenye maandiko mbalimbali na ahadi tofauti totauti kutoka kwa viongozi wa CCM lakini kwa ukweli hawatayaona kama mtoto anayesubiri mawe yaliyopikwa jikoni. Kwa kuwa imekuw hivyo kwa kipindi kirefu.
  Ufisadi umekuwa ni shughuli ya zamu kati ya viongozi waliopo madarakani akitoka huyu mwingine anasubiri achukue zamu ya kufisadi. Kila kona ni ufisadi tangu CDM wameanza kuibua ufisadi wa watawala hakuna siku tumeacha kusikia ufisadi wa rangi tofauti tofauti, ambayo hayakuweza kuonekana kabla ya CDM kuchachamaa? kwa kweli haya hayatakwisha bila CDM kuchukua dola.
  CDM si tu kwamba inapendwa kwa kuwa CCM inachukiwa ila inaoenekana ni mbadala wa CCM, ambayo mtaji wake wa vitisho na rushwa unaelekea kuchoka kabisa.
  WANANCHI WANAELEWA SANA TOFAUTI YA PUMBA NA MCHELE, NA TOTAUTI YA CHAMA CHA KICHINA (CCM) CHENYE VIONGOZI WENYE GHILBA NA CHEAP POLARITY LAKINI UWEZO WAO WA KUONGOZA NCHI NI DHAIFU KABISA..

  TANZANIA NI YETU WOTE
  Hata hivyo Tanzania ni yetu wote, inasikitisha sana watawala kutumia vyombo vya dola, ili kuvuruga demokrasia inayoanza kuwafikia wananchi kwa juhudi na bidii za vyama vya upinzani, nilitarajia CCM ambacho ni chama kikubwa na chenye uzoefu wa uongozi kiwa mbele kuheshimu makuzi haya ya demokrasia ambayo kwa kweli bado yana manufaa kwa watanzania wote.
  CCM kama chama kilitakia kisimamie vyema demokrasia iweze kukua ili pale ambapo wao wameonakana kupoteza mungÂ’aro wao kwa wananchi wangesimamia mabadiliko ili tuweze kuvuka salama kwenye mabadiliko haya ili wao warudi mezani na kujipanga upya, kwa uchaguzi mwingine. Mawazo mapya huwa ni neema, ingawa inaweza kuwa ni laana kama tuu hayakuandaliwa vizuri.
  Kutumia nguvu za aina mbalimbali kwenye kipindi hiki ambacho wananchi wapo kwenye kasi ya mabadiliko ni kuhatarisha amani na usalama ya taifa. Hatuhitaji sana kuwa hivyo tulivyo, nchi hii ni ya watanzania ambao ni mimi wewe na yeyote aliye raia wa Tanzania, kama wananchi wanataka kubadili uongozi zha demokrasia ituwezeshe kufikia mabadiliko hayo na kama wananchi hawayahitaji mabadiliko hayo, basi acha wananchi wasme kidemokrasia kwamba hawataki mabadiliko.
  Kutumia vyombo vya dola kuendesha demokrasia ya ghilba, kuna madhara makubwa zaidi kuliko kuacha demokrasia ifanye kazi yake kwa uhuru na haki.
  Asante naomba kuwasilisha.
   
Loading...