Demokrasia: Maana, misingi yake na faida kwa jamii

mdau wetu

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
548
58
Hivi Tanzania tuna misingi ya demokrasia? Tangu kuingia mfumo wa vyama vingi Tanzania hadi sasa kumekuweko kweli na mazingira huru ya harakati za vyama vya kisiasa? kama kama kweli kwa nini upinzani umeshindwa kuitoa CCM?

========

1595171434690.png


Demokrasia (kutoka neno la Kigiriki δημοκρατία, dēmokratía, maana yake utawala wa watu: δῆμος, dêmos, maana yake "watu" na κράτος, krátos, maana yake "utawala") ni aina ya serikali.

Neno hilo lilitumika kuanzia karne ya 5 KK kuelezea mtindo wa utawala uliotumika katika Athene na miji mingine kadhaa ya Ugiriki, kinyume cha ἀριστοκρατία, aristokratía, "utawala wa masharifu".

Kwenye demokrasia watu fulani wa jamii wanamchagua kiongozi wao.

Kuna njia nyingi za kufanya hivi, lakini mchakato kamili kwa kawaida huitwa kushikilia uchaguzi.

Vyama vya siasa huhusika na masuala ya siasa. Yaonekana kwamba yaweza kuwa rahisi kuwa na chama cha kisiasa. Chama kitakachoshinda uchaguzi kitamchagua kiongozi kinayemtaka.

Demokrasia ni nini?
Demokrasia ni mfumo wa serikali ambapo wananchi wote ni sawa mbele ya sheria na wanashiriki katika kufanya maamuzi ya kitaifa juu ya masuala ya Umma. Wakati mwingine wananchi hushiriki moja kwa moja - hii ina maana kwamba wao hupiga kura moja kwa moja kwenye masuala kama vile sheria na katika chaguzi. Wakati mwingine huwakilishwa na viongozi wao waliowachagua. Ni utawala wa watu, na watawala hutawala kwa ridhaa ya watu.

Kwa hiyo kwa kifupi Demokrasia ni mfumo unatoa fursa ya madaraka kwa Umma moja kwa moja au kutokana na uwakilishi.

Abraham Lincoln, Rais wa 16 wa Marekani, alisema Demokrasia ni serikali ya watu/mfumo wa utawala wa watu, kwa ajili ya watu na unaotokana na watu. Watu wanaunda serikali.

Aina za demokrasia
1. Demokrasia ya moja kwa moja (kwa Kiingereza "Direct Democracy") ni aina ya demokrasia ambayo wananchi wote wanaweza kushiriki katika kuamua masuala ya kisiasa, ya kijamii, ya kisheria na ya kiuchumi bila kutumia chombo cha uwakilishi kama vile bunge. Uwezo huu wa wananchi kutoa maamuzi unaweza kuwapa hata uwezo wa kimahakama, ingawa mara nyingi wananchi hupewa uwezo wa kutunga au kupitisha sheria tu.

Demokrasia ya moja kwa moja ni tofauti na demokrasia inayofuatwa katika nchi nyingi duniani hivi sasa, ambapo wananchi huchagua wawakilishi wao katika uchaguzi. Nchi ya Uswisi ni maarufu kwa mfumo wake wa demokrasia ya moja kwa moja ambako sheria nyingi zinaamuliwa na wananchi wote kwa njia ya kura.

2. Demokrasia shirikishi ("Representative Democracy"): hapo wachache hupewa na wengi dhamana katika uwakilishi wa jamii katika maamuzi. Wachache huchaguliwa na wengi kwa njia ya demokrasia huru na ya haki kwa kufuata Katiba ya nchi hiyo. Mfano: Wabunge huwakilisha wananchi wao katika kuleta maendeleo na kuishauri serikali juu ya maendeleo ya nchi yao.

Misingi ya demokrasia
  • Uwepo wa vipindi vya uchaguzi wa viongozi na chaguzi zenye kuzingatia haki na usawa.
  • Kuwepo uchaguzi huru na uwanja sawa wa kisiasa.
  • Wananchi wawe na fursa kikatiba kupata taarifa, vyanzo vya taarifa viwepo na kulindwa kisheria.
  • Wananchi na wanajamii wawe na fursa ya kuunda vyombo vya kijamii mathalani asasi za kiraia.
  • Kuwa na taasisi zinazolinda na kuchochea ustawi wa demokrasia nchini.
Umuhimu wa demokrasia
  • Kukosoa matumizi mabaya ya fedha na viongozi kwa misingi ya demokrasia.
  • Kushirikishwa kupanga kusimamia miradi ya maendeleo katika maeneo yao.
  • Kuunga mkono jitihada za serikali katika kuchochea ustawi na maendeleo kwa jamii.
  • Kuhoji utendaji wa serikali kuanzia ngazi ya mtaa, kata, kijiji, wilaya kuhakikisha uwazi, uadilifu na uwajibikaji.
Faida za demokrasia
  • Matumizi mazuri ya rasilimali za nchi.
  • Maendeleo endelevu.
  • Kupungua kwa umasikini, ujinga na maradhi.
  • Kutokomea kwa rushwa.
  • Huduma bora za jamii.
  • Amani na utulivu.
  • Kuheshimiwa kwa haki za binadamu.
  • Utatuzi wa migogoro kwa mujibu wa sheria na taratibu.
  • Kuleta ustawi wa wananchi.

Michango ya wadau

Demokrasia ni nini?

Demokrasia ni mfumo wa serikali ambapo wananchi wote ni sawa mbele ya sheria na wanashiriki katika kufanya maamuzi ya kitaifa juu ya masuala ya umma. Wakati mwingine wananchi hushiriki moja kwa moja - hii ina maana kwamba wao hupiga kura moja kwa moja kwenye masuala kama vile sheria na katika chaguzi. Wakati mwingine huwakilishwa na viongozi wao waliowachagua.

Tanzania ni nchi ya kidemokrasia . Baadhi ya mambo ya kidemokrasia katika utawala wa Tanzania ni:

· Watu humchagua rais, ambaye ni mkuu wa nchi na kiongozi wa serikali.

· Watu huchagua na kuwakilishwa na wabunge.

· Tanzania ina mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Kushiriki katika uchaguzi
· Uchaguzi ni mchakato wa kufanya maamuzi ambapo wananchi huchagua viongozi wa umma.

· Ili ushiriki katika uchaguzi Tanzania, ni lazima uwe umetimiza miaka 18, na lazima uonyeshe kitambulisho cha mpiga kura. Kupata kitambulisho hiki ni lazima ujiandikishe kwenye daftari la wapiga kupiga kura.

· Daftari la taifa la wapiga kura kimsingi lina majina yote ya watu wanaostahili kupiga kura. Mara kwa mara, serikali hupitia na kuboresha daftari hilo ili kuandikisha watu ambao kwa wakati huo wanakuwa wametimiza umri wa miaka 18 na kuondoa waliofariki na waliojiandikisha mara mbili.

· Moja ya faida za kujisajili kupiga kura ni kupata kadi ya mpiga kura, ambayo pia ni kitambulisho muhimu kwako.

· Kwa mujibu wa katiba, rais ambaye amekwishatawala vipindi viwili hatakiwi kuongoza kipindi kingine. Hivyo rais ambaye alichaguliwa mwaka 2015 ni rais wa tano wa nchi.

· Wakati huo huo, chama tawala kinaweza kuendelea kubaki madarakani kama kitashinda katika uchaguzi. Viongozi wa Watanzania wameendelea kuheshimu utaratibu wa ukomo wa rais kuwa madarakani tangu tuliporuhusu mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992 na uchaguzi

Umri na ushiriki katika utawala
Kwa mujibu wa katiba ya sasa, linapokuja suala la umri, kwa Watanzania lazima angalau uwe na umri wa miaka 21 ili kugombea ubunge. Kugombea nafasi ya urais lazima uwe umetimiza umri wa miaka 40.

Ni nini Misingi ya Demokrasia, Tujadili
----
Demokrasia ni serikali ya watu, iliyochaguliwa na watu, kwa ajili ya watu!.
"of the people, by the people and for the people".

Tanzania ni nchi ya kidekrasia tele!, na uchaguzi wa Zanziba ilikuwa ni uchaguzi huru na wa haki!.
Hata kule kususia uchaguzi huo, nako ni demokrasia!.

Pasco
----
Kimsingi, neno Demokrasia linatokana na maneno mawili ya asili ya Kigiriki, Demos likiwa na maana ya Watu (People) na Kratos likiwa na maana ya Madaraka (Power). Kwa hiyo, kwa tafsiri fupi, Demokrasia au Demoskratos ina maana ya Madaraka kwa Umma (Rule of the People).

Historia inaonyesha kuwa dhana ya demokrasia iliibuka na kuanza kutumika kwa mara ya kwanza katika mji wa Athens wakati wa Ugiriki ya zamani, kwenye miaka ya 508–507 BC (kabla ya ujio wa Kristo). Katika mji huu, Demokrasia ilianza kama mfumo unaotoa fursa ya moja kwa moja kwa watu au umma kuwa na maamuzi ya mwisho juu ya mustakabali wa pamoja wa maisha yao. Na Demokrasia hii ilijengwa na nguzo kuu mbili; kwanza baadhi ya raia walikuwa wakichaguliwa kujaza nafasi za kiutawala za uongozi wa kiserikali na wengine wakishika uongozi wa kimahakama. Kwa hiyo, walikuwa na Serikali na Mahakama.

Na pili, walikuwa na Baraza au Bunge kama chombo kikuu cha kutunga sheria za dola ya Athens. Bunge hili lilijumuisha raia wote wa Athens. Raia wote walikuwa wanaruhusiwa kuzungumza na kupiga kura. Isipokuwa, wanawake, watumwa, wageni, watu wasiomiliki ardhi na wanaume wa chini ya miaka 20 hawakuruhusiwa kushiriki kwenye Bunge la Wananchi. Hili lakubagua wanawake na wasiomiliki ardhi ndio lilikuwa moja ya dosari kuu za demokrasia hii.

Lakini jambo la msingi la kuzingatia hapa ni kuwa Demokrasia ni Mamlaka kwa Umma na Demokrasia hii ilikuwa inatoa mamlaka hayo kwa umma moja kwa moja. Na Demokrasia hii ya Athens iliwezekana wakati huo kwasababu watu hawakuwa wengi na kwa hiyo iliwezekana wote kukutanishwa pamoja kama Bunge na kufanya maamuzi. Lakini kutokana na ongezeko la watu na haja ya kufanya maamuzi yanayozingatia nguvu ya umma ndipo nadharia ya kidemokrasia ikatanuka na kuwa ni utawala au mfumo unaotoa fursa kwa mamlaka ya umma kwa njia ya ama moja kwa moja au kwa uwakilishi.

Katika mifumo ya kidemokrasia (maana ipo mingi) watu wanakuwa wanashirikishwa katika michakato ya kufanya kimaamuzi kwa ama kuwakilishwa na wawakilishi wao wanaokuwa wamepatikana kwa njia ya kuchaguliwa au kwa watu wenyewe kushiriki moja kwa moja kwenye Bunge/Baraza la Wananchi (citizens assembly). Demokrasia ni kuwa na serikali ambayo nguvu na mamlaka yote ya mwisho ya serikali hiyo yanakuwa ni watu walioiweka serikali hiyo madarakani.

Mwezi Novemba mwaka 1883 aliyekuwa Rais wa Marekani wa wakati huo, Abraham Lincoln alitoa hotuba fupi na maarufu sana katika eneo la Gettsburg wakati Marekani ikiwa inakabiliwa na madhila ya vita “American Civil War”. Pamoja na mambo mengine, hotuba hiyo inayojulikana kama “The Gettsburg Address” ilibeba maneno mazito yanayotumika hadi leo kuifafanua kwa ufupi na kwa uzito dhana ya Demokrasia. Kwamba, Demorasia ni kuwa na Serikali ya Watu, Inayotokana na Watu, Kwaajili ya Watu.

Wanazuoni mbalimbali duniani (intellectuals) wanaitumia tafsiri hii ya demokrasia baada ya kuichomoa kutoka kwenye hotuba ya Abraham Lincolin pale aliposema, nanukuu “that this nation, under God, shall have a new birth of freedom -- and that government of the people, by the people, for the people, shall not perish from the earth”, mwisho wa kunukuu. Kwamba, “Taifa hili,chini ya Mungu, lazima lipate uhuru mpya (akimaanisha Demokrasia) – na ile Serikali ya Watu, inayotokana na Watu ,kwaajili ya Watu, haitatoweka kamwe duniani”
Na kwa mujibu wa Mwanasayansi wa Siasa Larry Diamond (huyu ni Profesa wa Sosholojia na Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Stanford Marekani, Demokrasia inakamilishwa na nguzo kuu nne;

• Kwanza ni lazima kuwe na mfumo wa kuchagua na kubadilisha serikali au viongozi wa kiserikali kupitia chaguzi huru na za haki

• Pili, kuwe na ushiriki hai wa watu (active participation of the people) kama raia, katika michakato ya kisiasa na katika michakato ya maamuzi na muelekeo wa nchi katika maisha ya kila siku mbali na wakati wa chaguzi.

• Tatu, ni lazima haki za binadamu za raia wote zilindwe

• Nne, kuwe na utawala wa sheria, akiwa na maana kuwe na fursa sawa kwa raia wote mbele ya sheria na ya kupata haki kwa mujibu wa sheria.

Nadharia ya demokrasia leo hii imetanuka zaidi kuvuka ile demokrasia ya kiuchaguzi. Na hii inatokana na ukweli kuwa ni hatari kwa umma kupoteza mamlaka yake kwa muda mrefu hadi uchaguzi ufike. Kwa hiyo zipo nadharia za kidemokrasia kama Right of Recall ambayo hii ni nguvu ya wananchi kuwa na mamlaka ya kubadilisha serikali au viongozi hata kabla ya kipindi rasmi cha uchaguzi kufika, pale wanapoona serikali yao au viuongozi waliowachagua wanafanya ndivyo sivyo. Na nadharia nyingine ya kidemokrasia ambayo inazidi kupata nguvu hivi sasa ni nadharia ya Uwajibikaji wa Kijamii, yaani Social Accountability.

Ni mchakato wa kuwawezesha wananchi kudai utawala bora na uwajibikaji katika utoaji wa huduma za jamii. Wananchi wanakuwa na fursa ya kufuatilia na kupata taarifa na kuzichambua ili kuweza kufuatilia na kusimamia mipango, bajeti na utekelezaji wa miradi ya jamii inayotekelezwa serikali kwaajili yao. Katika nadhari hii ya kidemokrasia Jamii inakuwa na uwezo wa kuhoji uwajibikaji wa watendaji na watoa huduma mfano afya, elimu, maji na viongozi wanapaswa kuwajibika kwa wananchi kwa kuwa wawazi na kuwa tayari kueleza au kufafanua kwa wananchi nini kinaendelea.

Hii ni kwasababu kati ya uchaguzi mmoja hadi mwingine, mambo mengi yanakuwa yanatokea na ni muhimu wananchi waweze kuyajua kwa uwazi na kufuatilia kama msingi mkuu wa mamlaka ya kidempkrasia ambayo ni umma.

Peter Msigwa the MP for Iringa
----
Demokrasia Duni

ni aina ya demokrasia inayotokana na makundi
ya watu na kisha kupitia makundi hayo watu
kuunda serikali mfano: chama - serikali

Demokrasia Endelevu

ni aina ya demokrasia inayotoa fursa ya
usawa na kupinga ma tabaka katika jamii.

Demokrasia Shirikishi

katika aina hii ya Demokrasia wachache
hupewa dhamana na wengi katika uwakilishi
wa jamii katika maamuzi.
Wachache huchaguliwa na wengi kwa njia ya
Demokrasia huru na haki kwa kufuata Katiba
ya nchi hiyo. Mfano: Wa bunge uwakilisha
wananchi wao katika kuleta maendeleo na
kuishauri serikali juu ya maendeleo ya nchi.

DEMOKRASIA

ni mfumo unatoa fursa ya madaraka kwa
umma moja kwa moja au kutokana na
kuwakilishwa.
----
Zurri Mada kama hizi, inabidi uanze na definition, ili mtu anapojibu, tuwe tunaongelea kitu kimoja na si vitu viwili au zaidi tofauti.

Mathalani, kuna definitions tofauti za demokrasia, kuna ile inayosemademokrasia ni utawalawa watu, uliowekwa na watu, kwa ajili ya watu.

Mapungufu ya mfumo huu ni kwamba, kamawatu ni wajinga, wanaweza kuchagua uongoziwa kijinga, wakadumu katika ujinga bila maendeleo.

Hapo hapo, kuna wengine wanasema, demokrasia nipana zaidi ya mfumo wa utawala wa watu, uliowekwa na watu, kwa ajili ya watu. Ili demokrasiaiwepo,kunatakiwa kuwepona mambo mengine, kamaupatikanaji wa habari, elimu, utawala bora, haki za binadamu etc.

Katikamfumohuu wa pili, ambaounataka elimu iwe sehemu ya demokrasia, kusema mapungufu ya demokrasia ni pale watu wajinga watakapochagua utawalakijinga hauwezi kusimama.

Kwahiyo, utaona kwamba, uchambuzi wa mapungufu ya demokrasia unategemea na definition gani ya demokrasia unatumia.
----
Uko sahihi bro ! Ila mara nyingi ninapo weka jambo kuhusiana mfumo,mwenendo au taaluma fulani huwa nalenga katika misingi. Kwani husemwa ya kuwa kutokana na misingi hujengwa mambo kadha wa kadha.

Ama kuhusu maana,hapa leo nataka nitoe faida kidogo juu ya tamko MAANA,japokuwa kuna mada hasa niliwahi kuiweka hapa nikauliza "NI NINI MAANA YA MAANA ?" au kama nilivyoandika katika mada hiyo.

Maana ya maana ni kuruhusu kuingia yale yote yahusuyo jambo au tendo au neno husika na kuzuia kuingia yale yote yasiyo husika katika jambo husika. Nini namaanisha hapo,mathalani katika tamko Demokrasia hapo nimemaanisha yaingie yale yote yahusuyo dmokrasia na kuzuia kuingia yale yote yasiyo husu demokrasia.

Tukirudi katika ombi lako,ambalo kwalo nimelidodosa kidogo hapo juu. Mimi nimejikita katika misingi. Najua kabisa katika hizo maana ulizozitoa kuna jambo au sifa anuai za demokrasia sifa ambazo zinaitofautisha na mifumo mingine.

Au kwa kuliweka wazi hilo na ili nieleweke kirahisi zaidi ni kuwa hawa nazungumzia Siasa za Kidemokrasia.

Kwa maneno hayo mafupi naomba uendelee kutupa faida juu ya mada husika.

Sent using Jamii Forums mobile app
----
Mimi nakrudi niliposema.

Naona kama hujanielewa.

Nimesema hivi,

1.Neno "demokrasia" linaweza kuwa na maana nyingi tofauti.
2. Kama hatujawa makini, ku define "demokrasia" maana yake ni nini, na ipi tunayoiongelea, tunaweza tusielewane, kwa kuwa tutakuwa tunaongelea vitu viwili tofauti
3. Ili kuepuka mgongano wa kujadili nyekundu wakati tunaiita bluu na bluu wakati tunaiita nyekundu, inabidi kabla ya mjadala, tu define tunaongelea nini tunaposema tunaongelea demokrasia.

Kwa mfano, kwa definition ya demokrasia ya "utawala wa watu, kwa ajili ya watu, uliowekwa na watu" aliyoitoa Abraham Lincoln, demokrasia inaweza kuwa utawala mbaya, kwa sababu kama watu ni wajinga na wanachagua uongozi kijinga, na viongozi wanwaacha wawe wajinga, hiyo sehemu itazidisha ujinga tu.

Lakini kuna definition ya demokrasia iliyoenda kwa kina zaidi kuhusu hiyo ya Lincoln, inayosema kwamba, bila ya watu kuwa na elimu, uhuru wa habari, usawa chini ya sheria, haki za binadamu etc, huwezi kuwa na demokrasia.

Utaona kwamba, kwa definition ya pili, huwezi kusema kwamba demokrasia ina upungufu kwa sababu ya ujinga kuweza kuchagua uongozi mbovu. Ujinga ukiwepo sana hapo hatuhesabu kwamba kuna demokrasia. Mtu mjinga akipewa nafasi ya kuchagua, atachaguaje wakati hana ujanja wa kfanya uchaguzi sahihi?

Ukiulizwa "Tanzania ina demokrasia?" unaweza kujibu ndiyo kwa definition ya kwanza (in theory watu wanachagua viongozi wao), na hapana kwa definition ya pili (kuna ujinga mwingi, wizi wa kura mwingi, udikteta mwingi, uvunjwaji wa haki za binadamu mwingi, hakuna uhuru wa kujieleza na uhuru wa habari etc).

Sasa hapa, ili kujadili, inabidi wote tuelewane pamoja.

Tubaongelea demokrasia kwa definition gani?

Maana swali moja kama "Je, tanzania ina demokrasia?" linaweza kuwa na majibu tofauti, kutegemea na definition yetu ya demokrasia tunayoitumia.
----
Ni mfumo wa utawala ambamo viongozi wa serikali huchaguliwa na wananchi wa nchi husikia kwa kupiga kura.

Wagombea wanaopata kura nyingi ndio wanaunda serikali kwa msingi wa wengi wape, yaani wale walioshindwa wanakubali kuongozwa na waliowashinda hata kama ushindi huo ni wa kura moja tu kati ya kura milioni 50, bado demokrasi inasema wengi wape. Hiyo ni fofauati na utawala wa kidikiteta ambapo mtu mmoja anatumia nguvu kuingia madarakani mara nyingi kwa njia ya mapinduzi ya mabavu bila kujali kama anaowangoza wanamkubali au hapana; kwa mfano utawala wa iddi Amini ulikuwa wa kidikteta.

Utawala mweingine wa kidikiteta, ambao ni ule ambao kunapigwa kura ya mtu mmoja tu, halafu anapata kura zote, kama ilivyokuwa wakati wa Utawala utawala wa Saadam na pia wakati wa Nyerere ingawe yaye aliruhusu Bunge liwe la kidemokrasia, uraisi haukuwa unapatikana kidemokrasia.

Haki za bianadamu hazina uhusiano kabisa na demokrasi ingawa serikali ya kidemokrasia sahihi itakuwa pia inafuata haki za binadamu. Utawala wa Ghadafi, kwa mfano haukuwa wa kidemokrasisa, lakini ni utawala uliokuwa unafuata sana haki za binadamu, wakati utawala wa Hitler ulikuwa wa kidemokrasia lakini haukuwa unafuata haki za binadamu; wao walikuwa na haki za wajerumani tu, wengine wote walijulikana kam subhuman.

Je utawala wentu tanzania uko kwenye mizani gani, maana nimesikia wakubwa wanasema hatuna demokrasia. Je tuna viongozi waliojinyakulia madaraka bila utashi wa wanachi wetu?
 
Ndugu wana jf wenzangu ili swali la [nini maana ya democrasia] lilizunguka sana jana kichwani mwangu,baada ya hotuba ya kambi rasmi ya upinzani kuwasilisha hotuba yeke,ya wizara ya [habari utamaduni na michezo] bungeni,iliyo wasilishwa na mbunge wa mbeya mjini,joseph mbilinyi,maswali yaliyo nijia ni haya

[1]kumbe serikali ya chama cha mapinduzi inapenda hotuba ya kambi ya upinzani ilenge yale wao ccm wanayo yapenda wao,
[a]kuwasifia,
kuwapongeza.

[c]kusema yanayo wafuraishatu,nilishuhudia spika wa bunge haki wapangia kambi ya upinzani,yale yeye na ccm,wanayo penda kambi ya upinzani wa yazungumze,masikioni mwao,nikajiuliza swali pale spika alipomzimia mic joseph mbilinyi ili yale ambayo hawayapendi yasisikike kwa wanachi, lakini hakujua muwasilishaji ni mwana tahaluma wa kuongea bila mic, nikagundua democrasia ndani ya bunge la ccm, hamna, ila democrasia ni [1]kuisifu serikali[2]kuipongeza[3]na kuipigia makofi.

Nawasikitikia sana chama cha mapinduzi kwa bomu litakalo walipukia 2015 kwa kitendo walicho kifanya jana kimewa chefua sana waandishi wa habari tanzania na kauli ya juma mkamia, kukihita chama cha waandishi wa habari [ngo,s] hii ni dharau ya kupitiliza sana kwa waadhishi, naye bulaya, nikajiuliza je ccm inawataka waandishi waandike habari kama za gazeti la uhuru,amakweli hii ndio tanzania na democrasia za sifia sifia bungeni.
 
Katafute kwenye vitabu hata kwenye internet utajuwa maana yake na miiko yake halafu urudi kwenye hoja yako,watanzania hatujui democracy na hatutaijuwa kamwe!!!!
 
Jambo la msingi amabalo nimeliona ni kwamba hatuna reflective mechanism of democracy (uhuishaji demokrasia).Tumeingia mfumo wa vyama vingi tangu mwaka 1992 ni zaidi ya miongo miwili.lakini sasa tumeusahau mfumo wenyewe tena kwa reje reje tuu.

CCM lazima wajue serikali ni watu na watu ndio sisi wananchi ambao tunawakilishwa maoni yetu na mfumo wa vyama vingi ili kucheck balance of power. HIVO BASI MISINGI YA DEMOKRASIA LAZIMA IFATWE.
 
jambo la msingi amabalo nimeliona ni kwamba hatuna reflective mechanism of democracy (uhuishaji demokrasia).tumeingia mfumo wa vyama vingi tangu mwaka 1992 ni zaidi ya miongo miwili.lakini sasa tumeusahau mfumo wenyewe tena kwa reje reje tuu. Ccm lazima wajue serikali ni watu na watu ndio sisi wananchi ambao tunawakilishwa maoni yetu na mfumo wa vyama vingi ili kucheck balance of power. Hivo basi misingi ya demokrasia lazima ifatwe.

Naunga mkono hoja ndugu.
 
Nahisi demokrasia ya ukweli angalau kiasi fulani itapatikana labda kuwe mfumo wa serikali ya mseto, zaidi ya hapo wimbo ni ule ule tu!!! watu mnaabudu vyama kuliko hata dini zenu!!!! yaani hii inaitwa ukipata pa kubonyeza mpaka patoboke....

CCM wana ndoto za kutawala milele, Chadema nao wanaona ndio wanajua nini watanzania tunataka!!! wote wanasahau kuwa tuna Tabia zetu kama watanzania ambazo zipo ktk vyama vyote, yaani KUPATA NAFASI NI KUPATA SIO Kutumikia... na kinachofanyika sasa hivi ni kugombea nafasi tu!!!!

Ikiisha patikana tutasikia nyimbo zifuatazo.. ''MAZURI hayataki haraka'' Pole pole ndio mwendo, bandubandu humaliza gogo au miaka 50 aliyekuwepo mbona hakufanya sembuse mimi na mwaka 1? na mengine kibaoooo!! Ntawakumbushia tu hii post wakati ukifika. anyway akili mkichwa...
 
Nahisi demokrasia ya ukweli angalau kiasi fulani itapatikana labda kuwe mfumo wa serikali ya mseto, zaidi ya hapo wimbo ni ule ule tu!!! watu mnaabudu vyama kuliko hata dini zenu!!!! yaani hii inaitwa ukipata pa kubonyeza mpaka patoboke....

CCM wana ndoto za kutawala milele, Chadema nao wanaona ndio wanajua nini watanzania tunataka!!! wote wanasahau kuwa tuna Tabia zetu kama watanzania ambazo zipo ktk vyama vyote, yaani KUPATA NAFASI NI KUPATA SIO Kutumikia... na kinachofanyika sasa hivi ni kugombea nafasi tu!!!! ikiisha patikana tutasikia nyimbo zifuatazo.. ''MAZURI hayataki haraka'' Pole pole ndio mwendo, bandubandu humaliza gogo au miaka 50 aliyekuwepo mbona hakufanya sembuse mimi na mwaka 1? na mengine kibaoooo!! Ntawakumbushia tu hii post wakati ukifika. anyway akili mkichwa...

Wewe tunajuaga upande wako siku zote na hapa umejidai kubalance ila upande wako unajihirisha hapo mwishoni.
 
Wewe tunajuaga upande wako siku zote na hapa umejidai kubalance ila upande wako unajihirisha hapo mwishoni.

Upande wangu sio siri SIKO CCM wala CHADEMA!!!!!! na huwa Najadili hoja kama inavyokuja!!! Ila nahisi kwa jinsi hoja yangu ilivyokuingia unaona soo tu kuikubali lkn kwa kuwa uko upande mmoja kati ya CCM au CHADEMA unajua kabisa wote hamna sera kama hiyo ya serikali ya mseto....

Nakushauri uwe huru tu kusema ya rohoni hata kama wenzako watakuona unawasaliti... roho yako itakuwa na amani sana mkuu!!! kwa faida ya Tanzania Tunayoiota.....
 
Demokrasia ni nini? Na kwanini America wanatulazima katika nchi za bara Afrika kufuata mfumo wa demokrasia? kuna siri gani iliyopo ndani ya demokrasia? na je, Wingereza wanafuata mfumo wa demokrasia ?

Na kwanini katika nchi za kiarabu walazimishwe mfumo wa demokrasia wakati wao wanamfumo wao wa sharia? Nawasilisha ndugu manaJF intellgnc.
 
Demokrasia ni nini?

Demokrasia ni mfumo wa serikali ambapo wananchi wote ni sawa mbele ya sheria na wanashiriki katika kufanya maamuzi ya kitaifa juu ya masuala ya umma. Wakati mwingine wananchi hushiriki moja kwa moja - hii ina maana kwamba wao hupiga kura moja kwa moja kwenye masuala kama vile sheria na katika chaguzi. Wakati mwingine huwakilishwa na viongozi wao waliowachagua.

Tanzania ni nchi ya kidemokrasia . Baadhi ya mambo ya kidemokrasia katika utawala wa Tanzania ni:

· Watu humchagua rais, ambaye ni mkuu wa nchi na kiongozi wa serikali.

· Watu huchagua na kuwakilishwa na wabunge.

· Tanzania ina mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Kushiriki katika uchaguzi
· Uchaguzi ni mchakato wa kufanya maamuzi ambapo wananchi huchagua viongozi wa umma.

· Ili ushiriki katika uchaguzi Tanzania, ni lazima uwe umetimiza miaka 18, na lazima uonyeshe kitambulisho cha mpiga kura. Kupata kitambulisho hiki ni lazima ujiandikishe kwenye daftari la wapiga kupiga kura.

· Daftari la taifa la wapiga kura kimsingi lina majina yote ya watu wanaostahili kupiga kura. Mara kwa mara, serikali hupitia na kuboresha daftari hilo ili kuandikisha watu ambao kwa wakati huo wanakuwa wametimiza umri wa miaka 18 na kuondoa waliofariki na waliojiandikisha mara mbili.

· Moja ya faida za kujisajili kupiga kura ni kupata kadi ya mpiga kura, ambayo pia ni kitambulisho muhimu kwako.

· Kwa mujibu wa katiba, rais ambaye amekwishatawala vipindi viwili hatakiwi kuongoza kipindi kingine. Hivyo rais ambaye alichaguliwa mwaka 2015 ni rais wa tano wa nchi.

· Wakati huo huo, chama tawala kinaweza kuendelea kubaki madarakani kama kitashinda katika uchaguzi. Viongozi wa Watanzania wameendelea kuheshimu utaratibu wa ukomo wa rais kuwa madarakani tangu tuliporuhusu mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992 na uchaguzi

Umri na ushiriki katika utawala
Kwa mujibu wa katiba ya sasa, linapokuja suala la umri, kwa Watanzania lazima angalau uwe na umri wa miaka 21 ili kugombea ubunge. Kugombea nafasi ya urais lazima uwe umetimiza umri wa miaka 40.

Ni nini Misingi ya Demokrasia, Tujadili
 
Misingi ni pamoja na Shein kuheshimu misingi ya demokrasia na kumwachia Seif madaraka kwa ushindi mnono alioupataa
 
Ukifatilia kwa karibu na hata kuuliza mwanachama, au mshabiki eidha viongozi wa CCM na serikali yake kuwa maana ya domekrasia ni nini watakuambia ni CCM kuendelea kutawala hata kwa kumwagika damu ya watanzania bado wataita demokrasia.

Ni nani mwenye ujinga na mwenye akili finyu atapinga kuwa tanzania hakuna demokrasia hasa kilichotokea Zanzibar kimeonyesha wazi bila wananchi kujitoa muhanga na kupinga uonezi unaofanywa na CCM kamwe maamuzi huru ya wananchi hayataheshimiwa.

Makamba alipokuwa anahojiwa na TBC ameishia kujikanyaga kujibu maswali mepesi sana je hii ndio demokrasia? Yeye anasema kwamba wenzetu wameamua kujitoa wenyewe.....

Tanzania hakuna demokrasia
 
Nikiambiwa kuchagua Demokrasia au Amani na Usalama nitachagua amani na Usalama kama walivyochagua Wa Zanzibari leo
 
KWAHIYO AMANI NA USALAMA NI KUCHAGUA CCM?

Sahihi! CCM ndio chama pekee ambacho hakina historia ya kuhamasisha ghasia hapa nchini na Viongozi wake wa staafu wako busy duniani kurejesha Amani maeneo mbali mbali.

Hivi tunavoongea Mzee Mkapa yupo Burundi na Mdogo wake wa kisiasa Mzee Kikwete yupo Oman kusuluhisha Walibya.Thamani ya kitu mtaijua isipokuwepo, Uzuri wa CCM utaujua ikitokea ikahujumiwa ikaanguka.
 
Hakuna Demekrasia katika ulimwengu huu hilo liko wazi mkuu… wazungu wanatuhubiria tu lakin angalia america kwa Trump ndio utapata jibu… lakini hata hivo mi.nasema malipo ni hapahapa duniani …

Huyu Seif munaemlilia leo ndiye huyuhuyu aliyeenda kumchoma.Mh Aboud Jumbe kwa Mh Nyerere baada ya Aboud Jumbe kutaka kupeleka shauri mahakaman kuhoji juu ya muungano wetu na Seif aliiba zile nyaraka zote ambazo Aboud Jumbe aliziandaa na.

Kupeleka kwa Nyerere ilimradi tu awe karibu na Nyerere ampatie kiti ila kwa bahati mbaya naue alishaonekana nasura ya kinafikhi… Nyerere akafanya juu chini Aboud Jumbe akavuliwa uanchama ndani ya CCM na uraisi akaukosa rasmi yote hayo Seif sasa.leo Seif acha naww wakusurubu leo
 
Demokrasia kwa mujibu wa chama kubwa ni maigizo yanayofanyika ili kuiridhisha jumuia ya kimataifa lakini kiuhalisia si kweli. Hakuna kitu kinaniuma kama maoni yetu tuliyoyatua kwenye katiba ya Warioba kutupwa jalalani halafu wakajitengenezea rasimu yao wanayoitaka wao.

Haya ndiyo maigizo wanayoyaita Demokrasia. Mnauonyesha ulimwengu maigizo kana kwamba ni watanzania ndio wanaoamua, huku kichinichini wanaamua mabosi wa chama kubwa. Hali hii iko kwenye chaguzi zetu mpaka kwenye kura za maoni.
 
Back
Top Bottom