Demokrasia Ni Hatari Kwa Maendeleo Ya Kweli

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
887
705
Wengi wetu tunafahamu ya kuwa kinachoitwa demokrasia ni nyenzo ya unyonyaji,ukandamizaji,ukoloni mamboleo,ubeberu,wizi wa rasilimali {resources plundering} dhidi ya nchi tajiri kirasilimali ingawa maskini kimaisha hususani zinazoendelea au za dunia ya 3.

Demokrasia imekuwa na lengo la kutugawa,kutufarakanisha,kutugombanisha,kutufitinisha [ndugu vs Ndugu,jamaa vs rafiki,etc}..Vita nyingi zinazochochewa kutokea ktk nchi nyingi za kiafrika,arabuni,South america na Asia msingi wake ni chocheo la haki,usawa na mengineo yenye mizizi ya kinachoitwa demokrasia..

Lazima tuelewe na tuache kuabudu wamiriki wa demokrasia ikiwa kweli tunataka kuendeleza nchi zetu,mataifa yetu,jamii zetu..maendeleo hayawezi kuwepo kwa mitazamo,misukumo,mashinikizo,harakati mdebwedo...Nchi yetu ilioza ktk mifumo mingi mnoooo maamuzi magumu sana,uongozi thabiti sana,wenye ,maono juu ya fikra za matakwa ya tabaka lililopo..maono ya vizazi vilivyopo na vijavyo...

China inayotawala dunia kiuchumi kwa sasa si zao la kinachoitwa demokrasia uchwara..Mao na wananchi walijifunga mikanda,vibwebwe,vilemba kufanya kazi kwa bidii,kubidiishwa,mijeredi,shuruti..tunaona matunda leo mpaka tooth pick,vijiko,chupi,...twaagiza kwao...

Watanzania ikiwa kweli tunataka maendeleo ya kweli si ya maneno matamu ya kisiasa tufanye kazi na tuunge mkono jitihada za dhati za kuijenga nchi kwa manufaa ya vizazi na vizazi
 
Lakin siyo kutufunga midomo hata ya kukosoa pale tunapoona kunakasoro,
 
Mkuu,heshima mbele.umenena ukweli ambao ni mgumu kuukubali.watu wanaongelea kuhusu demikrasia pasipo kuelewa maana halisi ya hilo neno..wananchi tunatakiwa kujikita kwenye kufanya kazi kwa bidii,kutii sheria zilizopo na kuiachia serekali nafasi ya kufanya kazi..ni uhuru gani ambao tunajaribu kuupata?uhuru wa kutukana watu?uhuru wa kuropoka?uhuru wa kuvunja amani ya nchi?ndio demokrasia tunayoitaka?
 
Hivi CDM mnaumwa, katiba ya chama mbovu, uongozi wa CDM wa kiukooo, miaka 20 tangu chama kianze hakina kiwanja wala mpango wa kupata kiwanja.

Unaweza kuona namna CDM mlivyo wanaaa, mambo yenu ya msingi yamewashinda, sasa eti mnatangaza vita na Rais, mtaiweza???? ikiwa kivuli cha Dr Tulia mnakikimbia!
 
Lakin siyo kutufunga midomo hata ya kukosoa pale tunapoona kunakasoro,

Mi naona walijifunga wenyewe au
ImageUploadedByJamiiForums1467313883.725396.jpg
 
Demokrasia me naifananisha na sera za ujamaa ambazo ndio chanzo cha nchi nyingi kufeli ikiwemo tanzania!ujamaa ni demokrasia na udikteta ni ubepari.ubepari ndo ndo uliozitoa nchi nyingi ktk lindi la umaskini na ufukara na ujinga!mfano libya ilipigwa mhuri kwamba ni nchi ya kidikteta ila asilimia karibu 70 ya walibya ilikuwa ni university degree!!me kimtazamo demokrasia siitaki me nachotaka nipate unafuu na ubora wa maisha hapo sitalalamikia mtu!hivyo ushauri wa dezo kwa wanademokrasia embu tuache miaka 3angalau ipite ndo tupaze sauti kuu
 
Afrika tutaendelea kwa kuiga zaidi kuliko kubuni maana hakuna jipya la kubuni! Wenzetu walipokuwa wakiendelea walikumbana na vikwazo vingi wakajua kuvitatua. elimu mbalimbali kama banking, ujasiria mali, utafiti, biashara nk. ni miongoni mwa njia walizogundua katika kutatua matatizo.
Kwa upande wa Demokrasia waligundua kwamba ni kitu muhimu kulinda haki kwa wanadamu wote. Wafalme duniani kote walitesa sana raia zao na demokrasia ilkuwa tiba ya huu ugonjwa. Kwa hivi hatuna njia mbadala ya demokrasia kwa nchi zetu. Hatuwezi kubeza demokrasia eti ni ya wakoloni huku mifumo yetu ya utawala na uendeshaji inatoka huko huko. Tuendelee kutamadunika kidunia hakuna option.
 
Ifike wakati wenye upeo wa mambo mtambuka katika nchi hii tusaidie kupambanua njia,kanuni,mifumo sahihi na itikadi sawia kwa maendeleo ya nchi kwa faida ya sasa na baadae
 
Back
Top Bottom