David Djumbe
Member
- Oct 14, 2013
- 42
- 36
Watu wengi wamekuwa wakiitaja demokrasia lakini bila kujua maana na misingi yake, na kwa vigezo hivyo wamejikuta wakifanya maamuzi na kutoa matamko yanayoashiria kutokuridhishwa na maamuzi fulani na kisingizio kikubwa kimebaki kutokuwepo demokrasia kwenye maamuzi hayo.
Misingi mikubwa miwili inayopaswa kuzingatiwa katika utawala wa kidemokrasia ni UCHAGUZI na UENDESHAJI wa TAASISI,
katika yote haya, maamuzi ya wengi ndiyo yanayoheshimiwa na kufanya wachache kukubali kushindwa kwao na hivyo kusubiri muda mwingine tena kujaribu kushawishi na kukubaliwa na wengi.
Katika uchaguzi, tunategemea atakayepata kura nyingi zaidi ndiye anayepewa nafasi ya kuongoza kwa wakati huo, tunapompa nafasi ya kuongoza maana yake ni kukubali atuongoze kwa UTASHI wake lakini bila kwenda kinyume na katiba ya Taasisi.
Aliyechaguliwa kuongoza sio Mungu ila ni Binadamu hivyo tunapaswa kutambua kwamba tunaheshimu uongozi wake kwa sababu watu walimpa nafasi yeye kwa wakati huu, na kama kuna mambo yasiyoridhisha katika uongozi wake vikao husika vinapaswa kuweka wazi mambo hayo na utaratibu wa kikatiba ufuatwe.
Maamuzi yeyote kwenye vikao yanapaswa pia kufuata mawazo ya wengi, kama walio wengi wanapingana na kiongozi wa juu, basi hapa mara nyingi ni mgogoro wa kiuongozi ambapo maamuzi magumu yanapaswa kufikiwa kwa lengo la kuinusuru Taasisi husika.
Kumekuwa na matamshi ya viongozi mbalimbali wa CHADEMA kupinga maamuzi ya CC na wengine kujiuzulu huku wakitaka baraza kuu liitishwe, wanaofanya hivyo wamekuwa wakitaja Kubakwa kwa demokrasia ndani ya CHADEMA na hivyo kutokuridhishwa na maamuzi hayo ya CC, kimsingi wanaoibaka Demokrasia ni wao maana wanashindwa kuheshimu mamlaka iliyopo inayoongoza kwa mujibu wa katiba, maamuzi yaliyofanywa na mamlaka halali hayawezi kupingwa na watu ambao hawakuridhishwa kwa kutoa matamko hadharani, watu hao wanapaswa kufuata katiba na hatimaye kushawishi waweze kuungwa mkono kwenye vikao husika na sio vinginevyo. kwenda kinyume na hapo kunaweza kutafsiriwa tofauti kwenye taasisi.
watu wasioheshimu mamlaka husika wanaweza kuwa na nia tofauti na lengo kuu la taasisi husika? kukosoana pia ni hatua mojawapo katika utekelezaji wa Demokrasia, lakini tunahitaji kukosoana kwa kufuata utaratibu unaoilinda taasisi zaidi kuliko watu Binafsi.
Changamoto hizi tulizonazo tunapaswa kuzichukulia kitaasisi zaidi kuliko kibinafsi ili zituimarishe na sio kutubomoa au kuturudisha nyuma kwenye safari yetu.
Ni mawazo yangu binafsi kwa leo...