Demokrasia na visingizio vya Wakosoaji CHADEMA

David Djumbe

David Djumbe

Verified Member
42
95
Watu wengi wamekuwa wakiitaja demokrasia lakini bila kujua maana na misingi yake, na kwa vigezo hivyo wamejikuta wakifanya maamuzi na kutoa matamko yanayoashiria kutokuridhishwa na maamuzi fulani na kisingizio kikubwa kimebaki kutokuwepo demokrasia kwenye maamuzi hayo.

Misingi mikubwa miwili inayopaswa kuzingatiwa katika utawala wa kidemokrasia ni UCHAGUZI na UENDESHAJI wa TAASISI,
katika yote haya, maamuzi ya wengi ndiyo yanayoheshimiwa na kufanya wachache kukubali kushindwa kwao na hivyo kusubiri muda mwingine tena kujaribu kushawishi na kukubaliwa na wengi.

Katika uchaguzi, tunategemea atakayepata kura nyingi zaidi ndiye anayepewa nafasi ya kuongoza kwa wakati huo, tunapompa nafasi ya kuongoza maana yake ni kukubali atuongoze kwa UTASHI wake lakini bila kwenda kinyume na katiba ya Taasisi.
Aliyechaguliwa kuongoza sio Mungu ila ni Binadamu hivyo tunapaswa kutambua kwamba tunaheshimu uongozi wake kwa sababu watu walimpa nafasi yeye kwa wakati huu, na kama kuna mambo yasiyoridhisha katika uongozi wake vikao husika vinapaswa kuweka wazi mambo hayo na utaratibu wa kikatiba ufuatwe.
Maamuzi yeyote kwenye vikao yanapaswa pia kufuata mawazo ya wengi, kama walio wengi wanapingana na kiongozi wa juu, basi hapa mara nyingi ni mgogoro wa kiuongozi ambapo maamuzi magumu yanapaswa kufikiwa kwa lengo la kuinusuru Taasisi husika.

Kumekuwa na matamshi ya viongozi mbalimbali wa CHADEMA kupinga maamuzi ya CC na wengine kujiuzulu huku wakitaka baraza kuu liitishwe, wanaofanya hivyo wamekuwa wakitaja Kubakwa kwa demokrasia ndani ya CHADEMA na hivyo kutokuridhishwa na maamuzi hayo ya CC, kimsingi wanaoibaka Demokrasia ni wao maana wanashindwa kuheshimu mamlaka iliyopo inayoongoza kwa mujibu wa katiba, maamuzi yaliyofanywa na mamlaka halali hayawezi kupingwa na watu ambao hawakuridhishwa kwa kutoa matamko hadharani, watu hao wanapaswa kufuata katiba na hatimaye kushawishi waweze kuungwa mkono kwenye vikao husika na sio vinginevyo. kwenda kinyume na hapo kunaweza kutafsiriwa tofauti kwenye taasisi.

watu wasioheshimu mamlaka husika wanaweza kuwa na nia tofauti na lengo kuu la taasisi husika? kukosoana pia ni hatua mojawapo katika utekelezaji wa Demokrasia, lakini tunahitaji kukosoana kwa kufuata utaratibu unaoilinda taasisi zaidi kuliko watu Binafsi.
Changamoto hizi tulizonazo tunapaswa kuzichukulia kitaasisi zaidi kuliko kibinafsi ili zituimarishe na sio kutubomoa au kuturudisha nyuma kwenye safari yetu.

Ni mawazo yangu binafsi kwa leo...
 
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
14,198
2,000
MSIMAMO WA CHADEMA MKOA WA SINGIDA

(i)Tunalaani, kuipinga na kuikemea kamati kuu ya chama dhidi ya maamuzi yao haya ya kipuuzi yaliyojaa chuki, hofu na wasiwasi mwingi kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani ya chama

(ii)Tunamtaka mwenyekiti na katibu mkuu waitishe mara moja mkutano wa baraza kuu la chama kutolea maamuzi suala hilo.

(iii)Tunamtaka katibu mkuu awazuie wakurugenzi na maafisa wake aliowatuma kusambaa mikoani kusambaza waraka wa siri unaowachafua zitto na kitila na kwamba kufanya hivyo ni kujidharirisha wao wenyewe.

(iv)
Tunampa onyo kali katibu mkuu Dkt. Slaa kuwa asithubutu kukanyaga SINGIDA ikiwa bado hajayafanyia kazi maelekezo yetiu hapo juu, kuzunguka kwake mikoani baada ya kumvua vyeo zitto ni kwenda kuthibitisha kuwa amefanya makusudi mpango wake huo.

(v)Tunapenda wanachadema na watanzania watambue kuwa
Hatuna Imani na Mwenyekiti wa Taifa wa chama, Katibu Mkuu wa Chama, Kamati kuu kwa ujumla na tunamuagiza mbowe aivunje mara moja kisha nay eye ajiudhuru.

MWISHO, Kutokutii maamizio yetu haya ni kusababisha mgogoro usiokuwa na kikomo ndani ya chama hiki,Singida tunasema kuwa ''
kamati kuu inaweza kumvua zitto kabwe uongozi, inaweza kumuondolea heshima yake ndani ya jamii, inaweza pia kumsingizia kila aina ya uwongo itakavyo, lakini kamwe kamati kuu haiwezi KUZUIA MPASUKO NDANI YA CHADEMA.''
 
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
14,198
2,000
chadema imeshakufa mkuu, poleni sana mliipenda lakini israeli ameipenda zaidi
 
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
14,198
2,000
hausomeki, unatetea uhuni, ubabaishaji, umangimeza na wizi
 
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
14,198
2,000
kasome kwanza matamko ya viongozi waliojiuzulu na wanachama mbalimbali waliokosoa ujuha wa chadema na kamati kuu yake ndio urudi hapa na porojo zako hizi
 
Dr.Mo

Dr.Mo

JF-Expert Member
3,811
1,225
Leo ni zamu ya raisi wa migomo.....kusema ukweli....Sijawahi kuona kijana wa CCM humu jf mwenye akili na uwezo mzuri wa kusoma mada kuielewa na kuchangia point....sijawahi ona...wote ni pumba tu...ni hasara kubwa pia kwa taifa kuwa na vijana kama hawa
 
kambitza

kambitza

JF-Expert Member
1,940
2,000
Chadema kuwafanya watanzania wajinga ni unafiki wa kiwango cha juu....
 
CHAMVIGA

CHAMVIGA

JF-Expert Member
7,688
1,225
Mnaliwazana baada ya kulikoroga!? Poleni sana wabakaji wa demokrasia jipangeni tena kukijenga chama kwani kimekwisha. Itakuchukueni miaka 30 mpaka mtakaporudi hapa mlipokuwa. Poleni sana. Ni zamu ya wengine mlitesa na sasa tesekeni. Comeon CUF,NCCR,CHAUMA,CCJ et al.
 
Kitoabu

Kitoabu

JF-Expert Member
5,886
1,500
Mchaga kalewa Chimpumu kaamua kuja kutapikia huku. Hata ufanyeje CDM itabaki kua taasisi ya kichaga tu sisi wamikoa mingine haituhusu.
 
Kiboko.

Kiboko.

JF-Expert Member
2,815
2,000
Leo ni zamu ya raisi wa migomo.....kusema ukweli....Sijawahi kuona kijana wa CCM humu jf mwenye akili na uwezo mzuri wa kusoma mada kuielewa na kuchangia point....sijawahi ona...wote ni pumba tu...ni hasara kubwa pia kwa taifa kuwa na vijana kama hawa
Wemwenyew n janga la kitaifa pia hujishtukiii mada inasema vingne we waja kudsc Mtu aliechangia,akil yako n sawa na ya Bavicha,Lema,sugu,Msigwa na Dj Mboowe
 
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
34,333
2,000
Leo ni zamu ya raisi wa migomo.....kusema ukweli....Sijawahi kuona kijana wa CCM humu jf mwenye akili na uwezo mzuri wa kusoma mada kuielewa na kuchangia point....sijawahi ona...wote ni pumba tu...ni hasara kubwa pia kwa taifa kuwa na vijana kama hawa
Vijana hao wa CCM huwa ndio baadae wanakuwa viongozi baada ya maandalizi ( yaani hapo wako kwenye maandalizi) ya muda mrefu. Hao ndio wakina Nchimbi,Lukuvi, Lusinde nk.
Hicho ndio Chama tawala ambacho kinafanya kila kiwezacho kisitoke madarakani wakati hakijui kiko madarakani ili kifanyeje kuleta maisha bora kwa wananchi.
 
Msingida

Msingida

JF-Expert Member
5,761
2,000
Nimeisoma na kuielewa makala uliyoandika,inasikitisha watu kuiona kama mzaha lakini ni uhalisia wa Demokrasia.Sina ushabiki wa kichama sana bali ,kinachoendelea sasa katika siasa za Tanzania ni janga litalochukua mda mrefu kulitatua tusipo kuwa makini na kuichukulia kwa uweledi unao stahili.Ushabiki na umamluki hautatusaidia kufikia malengo ya muda mrefu ambayo watanzania tunaitaka zaidi ya mahitaji ya mda mfupi kitu ambacho hakitatuondoa katika hali tulionayo sasa.
Mbinu hizi zinazotumika kuibomoa CDM zitatumika kubomoa makambi yaliyopo kwenye kinyang`anyiro cha kugombea Urais ndani ya CCM kwakuwa wanaoinitiate wapo humo ndani yao.Sijui wata sustain vipi wakati huo kwa kuwa watu sasa wamebadilika kuliko wanavyo fikiria.
Ushauri:
CCM wajikite kuiokoa Tanzania kuondokana na umaskini uliokithiri hasa baada ya miaka 50 ya uhuru.Tuna rasilimali nyingi ambazo zinahitaji umakini kuzisimamia lakini wapo busy kuiangamiza CDM.Mnachekela kuwapata wafuasi wengi kipindi hiki cha mgogoro wa CDM,lakini wanahama na legacy za CDM kwenu hivyo mnajiingizia CDM ndani yenu bila kujijua na mwisho wake mtajutia mnachokifanya sasa.2015 siyo mbali tusije kujilaumu.
 
amakyasya

amakyasya

JF-Expert Member
3,463
0
Upepo unapita,wana ccm hujifanya wanachadema na kuhoji maamuzi ya cc.Wanapoteza muda kwani mabadiliko hayazuiliki.Chadema itakuwa imara zaidi bila zitto maana kijana huyu amekuwa kirusi ndani ya chama kwa muda mrefu.
 
Nicholas

Nicholas

JF-Expert Member
25,289
2,000
Mchaga kalewa Chimpumu kaamua kuja kutapikia huku. Hata ufanyeje CDM itabaki kua taasisi ya kichaga tu sisi wamikoa mingine haituhusu.
very good vilaza...Kwa jisni mnavyoamka na wachaga,mnalala na wachaga, na mtakufa kimyakimya ni wazi mnaonyesha mnachoamini "wachaga ni superior kuliko nyie vilaza".
 
P

Puruma

Member
97
0
INASHANGAZA SANA KWA NINI WANACHAMA CHADEMA HAWAUHOJI UONGOZI WA CHAMA UBADHIRIFU HUU:-

1. Fedha alizotoa Mzee Sabodo.

2.Kwanini fedha za ruzuku zinatumika Makao Makuu pekee.

3. Kwanini Fedha za ruzuku za chama anakopeshwa mtu badala ya kutumika matumizi halisi yaliyopangwa.

4.Fedha kutoka kwa wafadhili kwa ajili ya M4C kutolewa maamuzi na Mwenyekiti na katibu badala ya bodi ya manunuzi.

5. Fedha zilizotolewa na wafadhili kwa ajili ya kununulia magari ya kusaidia kuimarisha chama kupewa mtu mmoja bila
kupitia Tenda bodi ya chama.

6.Harambee mbalimbali za chama, fedha zake zimetumiwaje maana hazijawahi kuonekana popote pale.
 
Mr Dhaifu

Mr Dhaifu

JF-Expert Member
775
225

wananchi wanapaswa kuhoji haya kwanini ,fedha za epa zipo wapi?mabilio ya Rais ya kuwakopesha wananchi yapo wapi?kwanini mikataba kumi na saba ya wachina ipo wapi?kwanini tembo wanauwawa na serikali ipo?kwanini hospitali hakuna hata panadol ya shilingi ishirini?kwanini Arv feki zinakuwepo na hakuna aliyekamatwa?kwanini kuna madaraja A mpaka Z form four?kwanini Dar maji hakuna?kwanini mikataba inasainiwa hotelini ulaya?kwanini walimu hawalipwi mishahara yao lakini hatujasikia bunge au ziara ya Rais imehairishwa kwa kuwa serikali haina hela. na mengine mengi.
 
iron2012

iron2012

JF-Expert Member
442

Kinachonishangaza kwa wanachadema kwa nini hawajibu hoja badala yake wanalinganisha maovu ya ccm. Toeni kwanza Boriti katika macho yenu ndipo muwe na ujasili wa kuikosoa ccm. Nani atakayewaamini kweli mna moyo wa dhati kuondoa ufisadi wakati ndani ya chama kumejaa ufisadi? Inatutia mashaka kama mna kipande tu cha mkate ufisadi unaonekana Je mkipewa mkate mzima inakuwaje?
 
Mandown

Mandown

JF-Expert Member
1,669
1,250
Kuna mtu humu alifananisha CDM na ze komedi...! Naona ni kwajinsi hawa jamaa wanavo shambuliana kwa MAJUNGU.. upande fulani unao zidiwa wanakimbilia kulaumu CCM
 
Dr.Mo

Dr.Mo

JF-Expert Member
3,811
1,225
Vijana hao wa CCM huwa ndio baadae wanakuwa viongozi baada ya maandalizi ( yaani hapo wako kwenye maandalizi) ya muda mrefu. Hao ndio wakina Nchimbi,Lukuvi, Lusinde nk.
Hicho ndio Chama tawala ambacho kinafanya kila kiwezacho kisitoke madarakani wakati hakijui kiko madarakani ili kifanyeje kuleta maisha bora kwa wananchi.
...Ndo maana mkuu nasema ni HAsara kwa taifa kuwa na vijana kama hawa
 
N

nkongu ndasu

JF-Expert Member
22,567
2,000
Mnaliwazana baada ya kulikoroga!? Poleni sana wabakaji wa demokrasia jipangeni tena kukijenga chama kwani kimekwisha. Itakuchukueni miaka 30 mpaka mtakaporudi hapa mlipokuwa. Poleni sana. Ni zamu ya wengine mlitesa na sasa tesekeni. Comeon CUF,NCCR,CHAUMA,CCJ et al.
naomba nikijue hicho chama chenye demokrasia mkuu hapa nchini!
 
Forum statistics

Threads
1,425,226

Messages
35,085,100

Members
538,249
Top Bottom