Demokrasia na Maendeleo kwa Taifa Changa ni Vitu Viwili Tofauti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Demokrasia na Maendeleo kwa Taifa Changa ni Vitu Viwili Tofauti

Discussion in 'Great Thinkers' started by Raia Fulani, Sep 6, 2012.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Bado sijajua kwa usahihi mpaka wa uchanga wa umri wa Taifa lolote ni miaka mingapi, ila nikiitazama Tanzania bado naona miaka 50 bado taifa hili ni changa. Katika uchanga huu ni lazima tukubali kutoa sadaka jambo moja kwa ajili ya jingine ili hilo lililotolewa sadaka lije kukutana na lile lililoachwa kushamiri. Nazungumzia Demokrasia na Maendeleo. Tukubali kama Taifa kuacha lipi kwanza na kuongozana na lipi kwanza.

  Demokrasia yetu hadi sasa ipo katika nadharia tu hasa tukitilia maanani yale yanayotokea sasa na yaliyotangulia. Tangu kuanza kwa Taifa hili chini ya Uhuru toka wakoloni, pamekuwa hapana demokrasia ya uwazi kiasi cha kutosha kusema kuwa jambo hili linafanyiwa kazi kivitendo. Azimio la Arusha halikuwa na mrengo wa demokrasia japo lengo lilikuwa jema. Singependa kurudi sana huko awali. Mivutano ya leo katika siasa zetu ni picha ya wazi ya kukosekana hiyo demokrasia-utawala wa Raia na uhuru wa maoni, uhuru wa kuamini dini na itikadi pasina kuvunja sheria za nchi. Matokeo yake tunashuhudia mivutano, mitafaruku, mikandamizo, vitisho, na mauaji. Siasa ndio mwongozo wa taratibu za nchi. Siasa ndio maisha ya kila siku. Katika Demokrasia tumeshindwa.

  Maendeleo ni uboreshwaji wa hali za kimaisha za watu katika jamii wanamoishi. Haya maendeleo huonekana katika miundombinu (barabara, madaraja, reli, anga, elimu, afya, lishe, n.k), matumizi ya rasilimali (watu, ardhi, maji, madini, misitu, n.k), sayansi na teknolojia, n.k. Kote huko sisi kama Taifa tumeshindwa kuwa na comparative advantage pamojja na kuwa na kila namna ya kutuwezesha kama Taifa kutumia tulivyo navyo kujiletea maendeleo.

  Libya hapakuwa na demokrasia lakini palikuwa na maendeleo. Lakini kuminya moja na kukuza jingine isiwe ni ajenda ya kudumu. Wakati fulani katika Taifa watu wanahitaji kufurahia demokrasia na maendeleo kwa wakati mmoja. Hapa kwetu je? Tunafurahia vyote viwili kwa wakati ama tunaumizwa na vyote viwili kwa wakati mmoja?

  Katika hili ndipo nataka pia kuhoji dhana ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Ni walewale? Watapeleka haya mambo mawili kwa pamoja au wataanza na moja? Wanaamini katika demokrasia na maendeleo au demokrasia kwanza, au maendeleo kwanza? Kipi kipewe kipaumbele; maendeleo ama demokrasia.
   
 2. Mourinho

  Mourinho JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 4,622
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Sitaki na sina haja ya kuijadili chadema kwa sababu siamini katika demokrasia hasa kwa vitaifa vidogodogo kama chetu. Bado tunahitaji utawala wa kina Nyerere na kina Kagame kutunasua hapa tulipokwama,lakini niko tayari kukosolewa kwa hoja na mifano halisi kwamba demokrasia itatutoa hapa tulipokwama!
   
 3. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwa Chadema kama chama cha siasa ambacho hakijawahi kukamata dola kimsingi kwa sasa hio ni dhana fikirika au sadikika, dhana ya demokrasia na maendeleo itapimwa endapo chama hicho kitashika dola, vinginevyo sera na ilani za Chadema kwa sasa ni yaleyale...Shopping List...as once said by Jenerali Ulimwengu
   
 4. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Mourinho

  Hata kama tukiupata huo utawala kwa ajili ya maendeleo, ni lazima mwisho wa siku pawe na kikomo. Tatizo la mfumo ambao umeiweka demokrasia kando ni kuwa wale wanaoamini kuwa wako kwa ajili ya kuleta maendeleo huwa hawako tayari kutaka kupisha wengine waendeleze kilichopo.

  Wakati mwingine huwa wanakuwa sahihi kwa sababu kuwa hakuna mfumo rasmi wala sera za kitaifa kwa ajili ya maendeleo. Kila anayeingia madarakani anakuja na mfumo wake ambao unaharibu taratibu zilizowekwa awali. Dhana ya maendeleo kwanza ingekuwa na nguvu kama wanaoingia madarakani wataendeleza kile walichokuta
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  hata kama wakiingia madarakani ni muhimu moja lipewe kipaumbele kwanza. Demokrasia au maendeleo?
   
 6. Mourinho

  Mourinho JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 4,622
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Raia Fulani

  Hakuna lenye mwanzo lisilokua na mwisho, nadhani hata tukiangalia historia ya jamiii mbalimbali duniani utaona kuwa mfumo fulani(uwe wa utawala,teknolojia,kiuchumi,utamaduni hadi dini)uliifaa jamii fulani kwa muda fulani,muda na mazingira vilivyobadilika na mfumo nao ulibadilika.

  Hoja yangu hapa ni kuwa, mfumo wowote wa utawala/uongozi,lazima uakisi mazingira na muda (TIME and SPACE) ya jamii husika na pia maendeleo ya FIKRA katika jamii hiyo. Kwa wakati huu katika mazingira haya na kwa fikra zetu, bado nasisitiza tunahitaji kina NYERERE (Philosopher King) kutunasua hapa tulipokwama.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Mourinho

  Wakati mwingine hata falsafa hubadilika pia kutokana na mazingira. Alichoongea socrates au Nyerere miaka ile sicho ambacho angeongea leo. Nina uhakika na hili. Ndio maana ilifika wakati nyerere akasema anag'atuka maana alikuwa hana jipya tena. Wakati mwingine nataka kuamini kuwa sayansi na teknolojia zinataka kuchukua nafasi ya falsafa.

  Hoja ya maendeleo au demokrasia kwanza au ufafanuzi na utekelezaji wa hayo mawili haiitaji mtu mpya sana kutekeleza. Kila kitu kipo kwenye maandishi na ni suala la utashi tu sasa kuona kuwa yanatekelezeka.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Mourinho

  Mourinho JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 4,622
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Raia Fulani

  Kwanza salaam Mkuu!

  Nakubaliana na mawazo yako kwa asilimia kubwa tu ila tunakopishana ni kwenye kuset those good ideas into motion, hebu tuwe realistic kidogo, kama kila kitu kipo kwenye maandishi kwa nini hakuna huo utashi wa kuyatekeleza? Tunamiss nini hapa? Na hivi kuna uwezekano wa kuwa na sayansi bila falsafa?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  '' The study of the fundamental nature of
  knowledge, reality, and existence, esp. when considered as an academic discipline''

  sasa hapa tujue nini maana ya haya matatu; knowledge (maarifa), reality (uhalisia), na existence (uwepo). Labda pia niko poor kwenye ujuzi wa falsafa, lakini nauliza kwa mfano; mtu kama Dk Albert Sabin aliyegundua chanjo ya polio (ile ya matone), awekwe kwenye kundi la wanafalsafa au wanasayansi? Sabin ni mmoja tu, wako wengi. Sifa za mwanafalsafa ni zipi?

  Mtu kama Bill Gates tumwite mwanafalsafa au mjasiriamali tu? Falsafa ninavyojua inahusishwa zaidi na nadharia ya namna gani mwanadamu aishi. Sayansi/teknolojia ni matokeo ya changamoto za hayo maisha.

  Leo kwa mfano ukimpa nchi hii mwanasayansi mashuhuri kutawala, atatumia vigezo gani? Au ukimpa mwanasheria atatumia vigezo gani? Ndio maana kwenye kila Taifa kuna Think Tank (na hawa haimaanishi ni wanafalsafa bali wasomi wa kada fofauti). Hapa kwetu tuna Tume ya Mipango. Kazi ya Think Tank ya Taifa ni kuandaa sera za kimikakati na maendeleo. Sera hizi mwisho wa siku zinalindwa na sheria. Kwa hiyo sera na sheria ni mihimili miwili muhimu sana kwa ustawi aidha wa maendeleo au demokrasia.

  Si mara moja tumeona kuwa mtu mzuri kabisa mweye maadili na fikra zake akiharibiwa na mifumo anayoikuta katika taratibu zake za kiutendaji. Sasa huyu mmoja hata kama akiwa na falsafa ya aina gani kama mifumo iliyopo (sera na sheria) ni dhaifu atawezaje kupenyeza na kuwa kinara? Ndicho kilichomkuta Nyerere.
   
 10. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #10
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  naungana na wewe kwa asilimia 100,
  ili taifa liendelee lazima liwe na uongozi bora, nchi zote zilizoendelea hazikuendelea kwa democrasia ila udikteta wa serikali na uongozi ulioko madarakani wenye amri zisizopingwa na yeyeto ila kyote hayo yalifanyika kwa maslai na lengo moja tu ya kulikuza taifa hilo kimaendeleo, democrasia huja pale tu ambapo taifa limeshakuwa kiuchumi na kuwa na misingi bora hapo ndipo demokrasia inapoweza kufanya kazi vizuri.
  tanzania hatuhitaji democrasia tunahitaji kiongozi mbabe mwenye nia ya kulikuza taifa kimaendeleo. demokrasia inachelewesha maendeleo na kuruhusu kianya mingi ya rushwa na kunyonyana iwe sisi wenyewe au mataifa mengine kutunyonya sisi. demokrasia inaifanya taifa kuwa na wananchi wenye uhuru mwingi sana wa kuchagua hata yasiyo ya msingi na maendeleo kwa taifa.
  haki haki haki ili taifa liendelee tuweke kwanza haki na uhuru pembeni tufanye kazi kwa lazima kila mtu wajibike sio achague kuwajibika. ningekuwa na muda zaidi ningeendelea kudadavua zaidi
  katika demokrasia sera zaweza kuwa nzuri ila kwa sababu ya kuchagua kufanya ma kutofanya haki uhuru wa watu anaweza kuchagua kutozifanya sera hizo na tunabaki hapahapa.
  demokrasia na maendeleo ni vitu tofauti sanaaaaaaaaaaaaa
   
 11. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #11
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  hata hizi nchi tuzionazo sasa hazikuendelea kwa demokrasia ila udikteta tu mambo ya democrasia yalikuja baadae sana. sasa sisi tunajifanya kupractice SALAMODEL of leadership haitatufikisha popote.
   
 12. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #12
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  bado nyerere alikuwa sahihi namna alivyokuwa anaiendesha hii nchi japo alikosa wasomi wengi wenye kuzitumia resources za nchi vizuri tungenyooka na tungefika mbali.
   
 13. Mourinho

  Mourinho JF-Expert Member

  #13
  Sep 18, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 4,622
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Najaribu nisihame kwenye maada kuu ila nawasiwasi unaichukulia falsafa kama somo kama vile fizikia, historia n.k na unakwepa ku-aknowledge kwamba hizo sera na sheria za nchi( tena kama za hapa kwetu) zimekosa kutoa mwongozo kwa sababu kama taifa hatuna FALSAFA inayotuongoza au kututambulisha, naomba kufahamishwa kama ipo.
  Na pia hujanijibu kuwa kama tuna "sera na sheria na hao so called "think tank" kwa nini hatuna maendeleo neither democracy? kwa nini idadi ya wajinga inakua kila uchao?
  Haya kama Nyerere alishindwa(tena hujafafanua kuwa alishindwa katika nini na alifanikiwa katika nini,au alifeli kote mkuu?),kwa hizi sera zenu na sheria ni nani aliyefanikiwa,katika nini?
   
 14. Mourinho

  Mourinho JF-Expert Member

  #14
  Sep 18, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 4,622
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Kwa hali inavyoenda,tutamkumbuka sana Nyerere.
   
 15. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #15
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  MKUU,
  nakuhakikishia kwa watu wenye kujua nini maana ya uzalendo,kuwa wawajibikaji,kupenda kufanya kazi,kujituma na kuzisimamia sera,sheria na mikakati yote inayosaidia kuleta maendeleo tutamkumbuka sana nyerere,
  angalia sasa sheria zipo lakini zinawalakini kila kukicha watu wenye maslai wanazitafsiri kila namna wanavyopenda, katiba inakiukwa sheria zinapindishwa, watu wanafanya wanavyotaka, maadili hayapo toka ngazi ya familia hadi katika uongozi kila mtu anawaza kuiba maana kachoshwa ama amepata oppotunity ya kufanya hivyo, serikali haiheshimiki.
  haya katika jina la demokrasia na haki za binadamu nguvu kazi watu ipo tu inachezewa, rasilimali za nchi zinaibiwa ovyo na wachahce au wageni kwa kusaidiwa na wachache yani ni shida tupu, serikali haina meno ndani na nje ya nchi, hatuna dira wala muelekeo.
  kwa hakika mimi namtamani nyerere ama kiongozi anayefanana nae. sitaki kurudi katika mjadala wa azimio lakini bado nakiri azimio hata mimi nalisoma na kulirudia bado linamashiko sana.
   
 16. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #16
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  unajua katika nchi ya kidomokrasia unaweza ukahitaji watu wafanye kazi fulani kwa maendelo yao wanao uwezo wa kukwambia tutafanya au hatufanyi na haki zao za msingi kwa mujibu wa haki za binadamu za umoja wa taifa na wakawa sahihi kabisa ila katika utawala wa aina nyingine hawawezi kukataakwa sababu watawajibishwa kwa mujibu wa sheria za nchi. kwa kufanya hivi vijana siku hz wako bize wanatunga mistari kila kukicha nyimbo zenyewe hata hela ya kurekodia hawana. lakini nguvu kazi kama hii nafikiri ingewezwa kubanwa na kuleta faida ktk nchi. huu ndio utawala wa kidemokrasia.
   
 17. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #17
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  na wazungu wajanja sana wanajua nchi za kiafrica au tuseme nyingi zinazoendelea zikiwa na utawala wa kidikteta watashindwa kuzilazimisha kufanya yale wanayoyataka, hivyo kuzilazimisha ni kuziharibu hivyo zitakuwa rahisi kuvurugika. na sisi tulio wajinga twachukua demokrasia na kipigia debe bila kukagua na kukagua misingi yange na madhara ya misingi hio katika taifa changa kama letu.
  mwal aliweza kuibana hii demokrasia na kuitafsiri atakavyo anavyoona inafaa na kutoleta madhara.lakini hii ya maana ya mzungu ni sumu kwa maendeleo ya nchi zinazoendelea.
   
 18. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #18
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  kutolea mifano kwa nchi hii haimaanishi kuwa nakubali yale yanayofanywa ama kusadikika kufanywa na hivyo vyombo nilivyotaja hapo juu. Ukweli sera na sheria tunavyo ila ni butu. Think tank tunayo ila haina meno. Think Tank ya Hitler ilifanya kazi under great pressure, with all available resources at their disposal, na wali deliver. Hapa kwetu sio hivyo. Wataalam wetu wataandika wajuayo kuwa yana tija kimaendeleo na kisha kuikabidhi serikali. Sasa hapo ni juu ya serikali kuamua kutekeleza au kupiga danadana kwa visingizio vya 'vipaumbele' na 'bajeti finyu'. Nyerere yeye alisema kuwa hata angepewa miaka mingine 20 asingekuwa na jipya. Tujiulize ni kwa nini alisema haya. Ndipo ninaporudi kwenye hoja kuwa falsafa za mtu mmoja hazitoshi kuleta mabadiliko bali nguvu na mawazo ya watu kwenye mifumo ya kitaasiisi. Tulishaambiwa kuwa Afrika haihitaji tena strong men bali strong institutions. Hii ni kutokana na ukweli kuwa mambo yamebadilika
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Binafsi yangu sioni ubaya wa Demokrasia wala Maendeleo ikiwa tutafahamu MTAJI wa maskini ni NGUVUKAZI... hivyo matumizi ya Demokrasia na maendeleo yatamtazama maskini na jinsi gani ya kumwondoa ktk umaskini (hapa tulipokwama) maanake kuhalalisha fikra za sisi maskini hatuwezi isipokuwa kwa fimbo ni kudhalilisha uwezo wetu, AKILI na fikra za watu maskini kama walivyofanya wazungu ktk utumwa.

  Muhimu kwetu ni kufahamu Je, ni demokrasia gani na maendeleo gani tunayotahitajji kutoka hapa tulipo ktk mazingira yna nyakati hizi..Siamini ktk matumizi ya demokrasia na maendeleo sawa na nchi zilizoendelea ama zinazoendelea isipokuwa tuwe na mfumo unaolingana na nchi za dunia ya tatu..Gari likwama unatakiwa kulikwamua kwanza na wenye ujuzi wa kulikwamua ndio watakaopewa nafasi sio dereva na tingo wazuri kukadiria speed ya safari nyenyewe..
   
 20. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #20
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  umesomeka mkuu. pamoja na hayo, bora kuchapana bakora au kuacha mambo kwenda harijojo kama yalivyo kwa kisingizio cha demokrasia? kwamba mtu kakwapua mali ya umma kisha uchunguzi kuanza na kuchukua miaka kadhaa? kisa haki za mtu/fisadi? Na kwenye bluu, kama si toka dunia hizo mbili, ni wapi tunatoa mifano ya demokrasia na maendeleo?
   
Loading...