demokrasia na kitanzi cha CHADEMA UKOMBOZI WA Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

demokrasia na kitanzi cha CHADEMA UKOMBOZI WA Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MPAMBANAJI.COM, Nov 9, 2011.

 1. MPAMBANAJI.COM

  MPAMBANAJI.COM JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  Natambua wote tunayaona yanayofanyika Mjini Arusha na kwingineko katika kuibinya demokrasia kwa Watanzania wazalendo. Hii inamaana gani pale viongozi wakuu wa Chama wanapokamatwa na kuwajibishwa katika mazingira tata.Naamini kuwa Jeshi la Polisi lina haki ya kufanya kazi na kutekeleza wajibu wake katika kulinda usalama wa Raia na mali zake.ILA Sijui haswa kwa nini viongozi wa CDM walikamatwa pale NMC kwa kufanya mkesha.Je mbona watoto wamitaani wanakesha mitaani usiku kucha bila kuchukuliwa hatua yeyote? Mbona baadhi ya viongozi wa CCM wanavunja amri halali za jeshi la Polisi na hawachukuliwi hatua.mfano UVCCM mjini Arusha,Mbona kuna mikutano mingine inafanyika na kufunga barabara na wanaCCM lakini hawachukuliwi hatua.mfano Kiusa road/Street mjini Mshi?. Ukweli ni kwamba kadri haya yanavyofanyika ndivyo na waliolala wanaamka na siri ni haya yote ni 2015-2020 katika uchaguzi mkuu.Wachache wataamini kuwa CHADEMA wanajitafutia umaarufu au niwavurugaji kwa kadri ya uwezo wao ila pia nawaonea huruma kwani wengi bado hawajui nama kodi zao na haki zao zinavyominywa.Kizazi chote cha kufumbwa macho hakitakuwepo na kitakachokuwepo hakitafumbwa macho miaka ya 2015-2020 kwani mengi yafafahamika kupitia teknolojia ya utandawazi na elimu.Pia naamini sio wanaCCM wote wanofurahia yanayowakumba CHADEMA kwa kuutetea ukweli.Nachoamini kwa Nchi Makini hiki kingekua ni kipindi cha utekelezaji sera za chama kilichopewa ridhaa na Wananchi wa Tanzania na kukubali changamoto za kiuchumi na kimaisha sambamba na joints efforts katika utatuzi wake. Serikali kupambana na chadema nakuacha kutekeleza sera zake ni kuupanua mwanya wa Watanzania kuendelea kuichukia serikali yao wenyewe. Naamini katika demokrasia na amani. Watanzania tupambane kutekea haki na ustawi wa Taifa la Tanzania na pia tuamini katika amani na mshikamano. Ukombozi wa kweli utakuja tuu na tena amani na utulivu ni nguzo ya mafanikio yetu katika kutetea haki,wajibu, utawala bora na demokrasia
   
Loading...