Demokrasia & Mahakama na Katiba Mpya!: Takukuru! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Demokrasia & Mahakama na Katiba Mpya!: Takukuru!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by W. J. Malecela, May 2, 2012.

 1. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #1
  May 2, 2012
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  Ni matumaini yangu makubwa sana kwamba kwenye katiba mpya tutatilia maanani sana events zinazoendelea sasa za Mahakama na Chaguzi za Ubunge, I mean pole pole Tanzania tunaanza kujenga imani potofu sana ya kesi za uchaguzi as the alternative to our General elections!

  - Taifa lolote lenye wananchi wenye akili timamu haliwezi kukaa chini na kufurahia what is going on here, kesi za uchaguzi ni nyingi mno, WHY? Ina maana something is not right na our elections system, now what is that? I mean hizi kesi za uchaguzi zinaishia ku-freeze our National agendas kwa sababu until zimetatuliwa siamini jimbo linaweza kua kwenye mstari na mipango ya maendeleo ya taifa kwa jimbo! Hizi kesi zinazidi kutugawa taifa badala ya kutuweka pamoja kwa sababu zinaishia kutuletea unnecessary tension in our society!

  - Ni matumaini yangu kwamba kwenye katiba mpya tutakuwa waangalifu na kuliangalia kwa undani hili suala, I mean TAKUKURU sio siri wameshindwa kazi tuliyowapa taifa, sasa ni sawa tu ikivunjwa na kuanzisha njia mpya ya kupambana na maovu ya uchaguzi. NEC nao wapo hoi sana, I mean wanafanya nini na kesi zote za uchaguzi? May be they are too old, that they need to go too!


  - Lakini hatuwezi kuendelea na this kind of mediocre National elections, ni too costing economically and politically too!


  William @DSM City!
   
 2. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  le MUtuz kumbe ukiwa bongo unakuwa mwerevu mwerevu nimefuatilia post zako tangia ukiwa bongo kidogo unaandika andika sense kidogo sa ndo tuseme ukiendda @NY Unaacha akili JKN au ndo msemo wa majuu hhamnazo unaaply
   
 3. chipanga

  chipanga JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 661
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 60
  Mtoto kakua ss, hongera sn kwa muono wako lkn humo ndani ulimo ndiko unakoanzia uozo huu wote, sina hakika km mtakuwa tayari kuona katiba inayowavunja miguu.
   
 4. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #4
  May 2, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa sasa Kama mwana CCCM unaonaje ukienda hatua moja mbele zaidi ya kusema TAKUURU IVUNJWE na NEC shouul gO.

  • Upambanue structural reform,management na mfumo wa uteuzi/usaili zinazohtajika kwenye hizo taisis ili zifanye kazi vizuri.

  Mabadiiko gani yanahitajika kwenye hizo taasisi
   
 5. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,770
  Likes Received: 6,094
  Trophy Points: 280
  Yes; nakubaliana na wewe kuhusu "utimamu wa akili" na "matatizo kwenye mfumo wetu wa uchaguzi":-

  (i) Utimamu wa akili: Ni Makamba, Yusufu (former CCM Secretary General) aliyewaagiza wagombea wote wa CCM walioshindwa kufungua kesi then Chama kingegharamia. Nadhani matokeo yake yanaonekana - mrundikano wa kesi mahakamani nyingine hazina kichwa wala miguu. Kama kuna tatizo la utimamu wa akili, CCM na viongozi wao wanaongoza katika hili, at least kwa ku-refer ushauri wa Makamba.

  (ii) Mfumo wetu wa Uchaguzi:- Mkuu hili liko wazi, unaishi dunia gani? Tangu muundo wa NEC, uandikishaji/uboreshaji wa daftari la mpiga kura, upigaji, kuhesabu, na hatimaye matokeo ni vurugu tupu. Hili halina mjadala.
   
 6. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #6
  May 2, 2012
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Ha! ha! ha! ha! una maana Mutuz Le Baharia The Big Shoooow! ha! ha! ha! ha! super sana!

  William.
   
 7. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #7
  May 2, 2012
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Well, sio siri kwamba Takukuru wameshindwa kazi kwa sababu the main ishu kwenye hizi kesi ni rushwa, now where was Takukukuru? The second ishu kura always something to do na kura now where was NEC?

  - Kunapotokea uchaguzi tunawasikia sana NEC wakati wa kampeni tu wakijhusisha na kusimamia maneno ya kampeni, lakini inapokuja matendo ya ku-regulate the process wanapotea kabisa kwenye picture!

  - I mean let them go, tuanze upya na katiba mpya!, hapa tatizo ni kama mihimili mitatu ya serikali inafanya kazi kwa uhuru unaotakiwa? Dawa kurudi back to the foundation ya mihimili mitatu, kuna tatizo kubwa sana!

  William.
   
 8. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #8
  May 2, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,276
  Trophy Points: 280
  Aisee hii thread yako ni bora ungeitunza na kuileta siku nyingine, Hukumu ya leo kumpa ushindi Mahanga ni matusi kwetu watu wa Jimbo la Segerea na nikuzidi kushusha heshima ya Mahakama.

  Sina tena imani na Mahakama at all, kuanzia sasa mtu atakayethubutu kuchakachuwa maamuzi ya wananchi hukumu yake ni kifo tu.
   
 9. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #9
  May 2, 2012
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Great Thinkers tunatakiwa kuangalia ishus muhimu kwa taifa in a big way bro, mambo ya yanga na simba sisi tujiepushe nayo maana ni unproductive, kwenye Sheria kuna FACTS na EVIDENCE, meaning kama unayosema ni kweli zimechezewa huko mahakamani leo, so dawa ni kukata rufaa!

  - Lakini Great Thinkers tunaachana na kuangalia leo tu, tunaangalia faida na hasara kwa taifa na hizi kesi, na hasa the damage to our fragile Democracy!

  William.
   
 10. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #10
  May 2, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Takukuru nadhani hawajapewa uwezo wa kufanya kazi kwa uhuru.Mfano kama sikosei CAG akishakuwa appointed imetoka hakuna ananayeweza kureverse .Hata rais mwenyewe ( If amwong nisahishe). BUT kwa TAKUKURU SIO . Sasa ni vitu kama hivi vinaweza kubadilisha ufanisi wa mambo

  Wakati wewe unatazama uchaguziwa siasa sisi wengine tunatazama EPA,RADA,KAGODA. Rushwa uuhaguzi ni vey complex zaidi kuliko wizi wa EPA,Rushwa ya RADA.
   
 11. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #11
  May 2, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  William, tatizo la Tanzania ni mfumo tulionao tutalaumu punda havuti kumbe toroli lenyewe halina matairi.

  TAKUKURU iliwekwa pale kisiasa kwa kazi maalum ya kulinda maslahi binafsi ya watu, sababu ya pili ni kuyaonyesha mataifa wahisani kuwa tuko serious kupambana na rushwa ili wazidi kutuamini kumbe hakuna chochote kinachofanyika, refer walivyoshughulikia mambo ya rada, EPA, chaguzi nk. TAKUKURU ni sawa na mbwa asiye na meno, kama inafikia TAKUKURU wanaomba wananchi wenye fununu wawape taarifa, polisi wafanye nini. Mimi nafikiri kitengo hiki kivunjwe kwa vile kinaliongezea taifa gharama mara mbili kiimarishwe kitengo cha upelelezi ndani ya jeshi la polisi.

  Yanayotokea leo kesi za uchaguzi kurudiwa ni matokeo ya uzembe wa NEC na TAKUKURU, watu tutaendelea kuwalaumu wanasiasa kina Makongoro kumbe masikini ni uzembe wa NEC na TAKUKURU. Chukulia mfano uchaguzi wa AM, rushwa iliripotiwa kutembea toka primaries za CCM lakini hakuna kilichofanyika hata kule kukemea tu hakuna, kama pingamizi likiwekwa nani wa kulaumiwa. NEC kwa makusudi inachangia sana, itakuwaje kwa mfano msimamizi wa uchaguzi atangaze matokeo bila kujumlisha vituo vyote au abadilishe matokeo?. Still anayeadhibiwa ni mwanasiasa kwa kufutwa matokeo au kutakiwa kulipa gharama za kesi. Nafikiri wasimamizi wa uchaguzi au NEC wangekuwa wanajumuishwa kwenye kulipa gharama za kesi pindi matokeo yanapokuwa nullified ili next time wawe waangalifu zaidi.

  Long term solution ni kuwa na Independent Electral Commission (IEC), wajumbe wake wasiteuliwe bali wachaguliwe kwa meritocracy, na iwe inclusive kwa vyama vyote, au alternative wajumbe wasiwe wanachama wa chama chochote kabisa na wachaguliwe siyo kuteuliwa na rais kwa sababu lazima wata favour chama cha rais aliyewateua. Kama tunataka kujenga taifa letu sote hii inawezekana lakini kama tunataka kujenga taifa la matabaka tuendelee na mfumo uliopo.
   
 12. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #12
  May 2, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  hii thread asingeitoa km hukumu ya mwizi wa masanduku ya kura isingesomwa leo.
   
Loading...