Demokrasia inatupotezea sana muda na nguvu

We unaleta hoja mfu. Ungekaa kimya.Kuna wakati hoja za JF zinakuwa za kijinga kwa kuwa mnakimbilia hisia zenu badala ya kujadil mada. Nani kakuibia kula. Hata Trump kasema kaibiwa. Wengine wanadai Urusi kaingilia. Haya hayatusaidii. JF ilitakiwa sehemu ya kujadili na kuwa na mawazo mapya.

Wote mnaongelea Demokrasia na maendeleo. Taja hapa nchi Zote zilizoendelea kwa sababu ya Demokrasia. Zipi. Hakuna.

Baada ya maendeleo ndo mambo ya Siasa yakachukua mkondo na ustaarabu. Na hata Demokrasia unayozungumzia haina one Definition na nahisi nyinyi Demokrasia Ni kufanya mambo tu Kadiri mnavyoamka. Kwa nchi ya Tansania, mikutano na ujinga ujinga baada ya uchaguzi ndo mambo yanayotufanya Tuwe chini kabisa. Nchi hizi zilizoendelea. Watu wanaendelea na majukumu Yao. Na Hata Siasa haziwahusu. Wanasiasa wanaendelea na Yao. Sisi tunaacha kazi tunasingizia Demokrasia.

Kama kwa mawazo yako uchaguzi wa mwaka jana ulikuwa wa huru na haki na hakuna kura zimeibiwa basi hatutaweza kuelewana. Imefika wakati wa kuwaacha watu wamebishane na wenzao wanaopenda ligi za mabishano yasiyo na tija mimi sina muda huo. Siku ukiaamka ndugu yangu tutakutana kwenye hoja lakini endelea kulala!. Uelewa wa vijana wetu siku hizi unatisha kwa uduni kuliko hata udikteta. Hawa ndiyo viongozi wetu wajao ambao tutawapa nchi waendeshe wakati wanajidanganya mpaka nafsi.
 
Demokrasia na maendeleo ni vitu tofauti kabisa. Si lazima kuwa na demokrasi ili kupata maendeleo, tena demokrasia ni adui wa maendeleo. Maana demokrasia na kodi/tozo kubwa ni kaka na dada.
Mbona jpm alizima demokrasia lakini nchi ilikuwa inaenda ICU kwa wawekezaji wote kukimbia na mzunguko wa pesa kukata
 
Mbona jpm alizima demokrasia lakini nchi ilikuwa inaenda ICU kwa wawekezaji wote kukimbia na mzunguko wa pesa kukata
Wawekezaji hawakukimbia sababu ya kukosekana kwa demokrasia, walikimbia sababu ya sera za kiuchumi za JPM. Hazikuwa rafiki kwao.
 
Demokrasia imekuwa kitu cha hovyo sana kinachorudisha nchi nyuma, hasa nchi za kiafrika. Wanasiasa hawawazi tena maendeleo bali wanawaza jinsi ya kuingia madarakani na jinsi ya kubaki madarakani. Hakuna anayejali maslahi ya nchi. Kenya walianza kuongelea uchaguzi wa 2022 miaka 3 iliyopita.

Rais Samia anaongelea uchaguzi wa 2025 leo. Nchi haina dira yoyote bali ni kusikiliza kelele huku na huko na kuzifanyia kazi, imaendeshwa kwa matukio.

Kwenye demokrasia Serikali inatapanya mali, inakopa na kufuja ikijua kesho mzigo wa deni siyo wake. Ndiyo maana kila utawala mpya ukiingia utakuta unalalamika hazina imekombwa.

Tungerudi tu kwenye chama kimoja. Au tukae chini tuumize vichwa tuje na utaratibu mwingine na si demokrasia. Demokrasia ni uongo.
Wewe ni miongoni mwa hao wakwamishao Afrika kupiga hatua kwasababu ya viashiria vyako vya ubinafsi mkubwa ulivyovionyesha.

(Samahani kwa kukushut namna hii)

Demokrasia unayoilaani inaelekeza watu kujadili mambo yao kwa ukweli na uwazi ili kupata suluhisho. Wewe unaonekana kupenda zile kauri za kufanya kila kitu siri - huko kwenye siri ndiko hujaa wabadhirifu wenye vichwa mgando wasio na utu wala aibu.

Kinachotokea Afrika ni ushamba wa madaraka. Mtu akipata madaraka anajiona yeye si binadamu wa kawaida na kujiona kuwa ana akili kuliko watu wote walio chini yake.

Mtazame yule mama wa Ujerumani(nchi yenye demokrasia hata USA wakasome) Yule mama kila linapotokea jambo huita mawaziri wake hukaa pamoja wakijadiri tena wakati mwingine live kwenye tv, uamuzi unaotolewa kila mtu anakubaliana nao.


Itazame Ujerumani iliyokuwa chini ya mataifa yaliyoshinda WW2 hadi mwaka 90 yakipora mali ya Ujerumani kwa kisingizio cha kujilipa hasara ya vita. Ujerumani ya leo baada ya 1990 imekuwa ni nguzo ya Ulaya.

Tunachotakiwa kukifanya ni kupigania kupata wawakilishi wetu walio sahihi kwenye uongozi wa nchi. Tunapokosa uwakilishwaji ulio sahihi ndipo hutokea utopolo wote huo unaousikia.
Amen
 
Hoja mujarabu kabisa, hii kitu sio ya Africa, pia hii inadhihirisha ni kwa kiasi gani vuguvugu la ukombozi wa Africa kupitia kina Nyerere, Kenyatta, Nkurumah, Lumumba na wengineo lilivyokwama au kufeli kabisa.

Ikiwa mfumo wako wa uongozi ni lamiza, bila hiyari kuwa Copy and Paste kutoka kwa jirani budi kujitafakari uhuru wako wa maamuzi.
Kama mfumo unaruhusu matatizo kwa karibu bara zima basi haufai kabisa. Au hautufai kabisa. Na si Africa tu, huko South Amerika na South East Asia shida tupu.
 
Demokrasia imekuwa kitu cha hovyo sana kinachorudisha nchi nyuma, hasa nchi za kiafrika. Wanasiasa hawawazi tena maendeleo bali wanawaza jinsi ya kuingia madarakani na jinsi ya kubaki madarakani. Hakuna anayejali maslahi ya nchi. Kenya walianza kuongelea uchaguzi wa 2022 miaka 3 iliyopita.

Rais Samia anaongelea uchaguzi wa 2025 leo. Nchi haina dira yoyote bali ni kusikiliza kelele huku na huko na kuzifanyia kazi, imaendeshwa kwa matukio.

Kwenye demokrasia Serikali inatapanya mali, inakopa na kufuja ikijua kesho mzigo wa deni siyo wake. Ndiyo maana kila utawala mpya ukiingia utakuta unalalamika hazina imekombwa.

Tungerudi tu kwenye chama kimoja. Au tukae chini tuumize vichwa tuje na utaratibu mwingine na si demokrasia. Demokrasia ni uongo.
Wavivu wengi hukimbilia kwenye kulalama

Na demokrasia is a very good Avenue for that
 
Wavivu wengi hukimbilia kwenye kulalama

Na demokrasia is a very good Avenue for that
Na watu wanapredict itakuja kuharibu mambo kama ujamaa tu. Sababu watu wanapiga kelele, na kwenye demokrasia wengi wanaopiga kelele wanasikilizwa. Unapaswa kuwapa wanachotaka la sivyo wanakuangusha. Wanapiga kelele wanapewa bima ya afya kwa kila mtu, wanapiga tena kelele wanapewa elimu bure, wanapiga tena kelele wanapewa hiki na kile bure. Sasa serikali inapata wapi pesa zote hizo? Inazidi kuongeza tozo na mwisho wa siku ni mkwamo mkubwa wa uchumi, na shida tupu. Mwisho wa siku serikali haitaweza kufanya chochote zaidi ya kuhudumia mahitaji yasiyoisha ya wapiga kelele. Wanapredict hiyo ndiyo hatima ya welfare state zinazozalishwa na demokrasia.
 
Tatizo sii Demokrasia ila ni mfumo wa chama kimoja kungangania kubaki madarakani il-hali wanajua hawapendwi tena na wananchi. Matumizi ya dola kubaki madaraki ndicho kitu kingine kinachoichafulia nchi.
 
Si lazima. Libya iliendeshwa kibabe na ilikuwa tulivu kwa miaka mingi. Huko North Korea hatusikii watu kuuuana kama walivyouawa watu Zanzibar mwaka jana, au Kenya 2008.
Ndugu, kwa mifano hiyo ya utawala HAPANA.
Libya ya Gadafi ilikandamiza makabila madogo ya kusini mwa nchi na iilkuwa kichaka cha magaidi waliosumbua sana dunia. .
North Korea; Ukitofautiana na MKUU unapotezwa kama yaliyomtokea hata KAKA mtu pale Kuala Lumpur International Airport, Malaysia.
Kote huko yawezekana panakuwa na utulivu kwa kiasi fulani, ingawaje PIA inategemeana hilo linasemwa na nani.
Lakini juu ya yote kinachohitajika katika nchi ni AMANI. Huu ndio msingi wa haki na hatimae MAENDELEO.
 
umenikumbusha kipindi cha wimbi la kununua viongozi wa wapinzani, wabunge na madiwani aisee kilikuwa kipindi cha mavuno kweli kweli
Aliyechezea fursa ni kigogo pekee ndo alipishana live na hela za jiwe.Waunga juhudi walimdisi jiwe kutengeneza cv ya kununuliwa na jiwe kwa bei juu
 
Back
Top Bottom