thetallest
JF-Expert Member
- Oct 21, 2017
- 8,256
- 9,085
Kupanga ni kuchagua.marudio ya chaguzi ndogo zinazoendelea nchini ni halali kwa mujibu wa katiba ,kanuni na taratibu tulizojiwekekea kama nchi,na wabunge waliopitisha mswaada huu walikua ni wa vyama vyote vya siasa vilivyokua na wabunge wakati huo.
Inashangaza sasa kuona baadhi yetu tunalaumu utaratibu huu wa kisheria.
Naamini kwa wanaolaumu wako sawa kwa sababu nguvu yao inapungua kwa kasi sana. Ingekuwa wabunge na madiwani hao wa chama X wangekua wanahama toka chama Y kuja chama X ingekua ni shangwe sana kwa chama X, wakijinasibu kwamba wahamaji hao wamejitambua na sifa kedekede kuwamwagia.
Nionavyo mimi ni kwamba kuna tatizo ndani ya vyama vyenyewe vya siasa ,ni ngumu kunielewe kwa mwenye itikadi ,ushabiki,na mtanguliza maslahi binafisi. Pamba walizoweka masikioni watazitoa wakati muda umewatupa mkono.
Tusipokubali kusikia maoni tofauti, kuhojiwa, tukaamua kuhodhi vyama vya siasa kama mali binafsi, tunaviua vyama vyetu kwa kiburi cha kusingizia wanachama wananunuliwa.
Ifike mahala demokrasia itawale ndani ya vyama vya siasa ili kuondoa hii sintofahamu ya wimbi la hamahama.
Niwapongeze wabunge na madiwani wanaotumia demokrasia kufanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi.
Mwisho kabisa, naomba mchanganuo toka kwa yeyote yule ambae ana data kamili za gharama za uchaguzi walau za jimbo moja tu la uchaguzi wa marudio,kwa maana ya shilingi kwa shilingi, ili sisi wadau tuone kisha tulipeleke suala hili bungeni kufanyiwa amendments