Elections 2010 Demokrasia gani? Rais kuchaguliwa na watu mil. 5 kuongoza mil. 45

Matata

Member
Mar 28, 2006
23
10
Huu ni UPUUZI, Watanzania tuko Million 45.
Waliojiandikisha kupiga kura eti ni Million 19
Waliopiga kura ni Million 8
Walio mchagua rais ni million 5
swali, Je Million 11 kwanini hawakupiga kura?
Utaratibu huu ni mbovu inabidi ufanyiwe marekebisho, hii ni kasoro kubwa sana kama tunataka kujenga demokrasia ya kweli. Wala nchi wanasema ni ushindi wa kishindo!!!!!!
Unachaguliwa na watu Million 5 ili uongoze watu million 45??!!
 
Katika hili hamna tatizo maana hao ndio waliojitokeza kupiga kura, huwezi kulazimisha kama hawataki, ni wajibu pia wa kila chama kuhamasisha wanachama na washabiki wake kwenda kupiga kura. Hata kama siku ya kupiga kura wangeenda milioni Nne, bado uchaguzi ungeendelea na yeyote ambaye angeshinda angepata usukani wa kuwa Rais kuongoza nchi yetu, that is the cost of democracy.
 
Huu ni UPUUZI, Watanzania tuko Million 45.
Waliojiandikisha kupiga kura eti ni Million 19
Waliopiga kura ni Million 8
Walio mchagua rais ni million 5
swali, Je Million 11 kwanini hawakupiga kura?
Utaratibu huu ni mbovu inabidi ufanyiwe marekebisho, hii ni kasoro kubwa sana kama tunataka kujenga demokrasia ya kweli. Wala nchi wanasema ni ushindi wa kishindo!!!!!!
Unachaguliwa na watu Million 5 ili uongoze watu million 45??!!
so kikwete anaongoza kwa kuchaguliwa na minority du! Najua anaona aibu ila anashindwa kusema. Nadhani lowasa atachaguliwa na watu 2M tu 2015
 
Viongozi wa ccm maeneo mbalimbali walikamatwa wakiwa wamenunua shahada. Inawezekana hili zoezi lilikuwa ni kubwa sana.

Kwakuwa wamesha uza shahada, wasingeweza kwenda kupiga kura!

Shame tume ya uchaguzi ya ccm , shame waliojitangazia ushindi!

Hata mkipita na ving'ora tafakari kwamba idadi kubwa ya watanzania haiwapendi, mnalazimisha kutawala.
 
Matata asante sana kwa kauli yako nzuri. Mimi kilichonitisha sana ni kile cha mwenyekiti na Katibu wa CCM kuchukua ndege hadi Mwanza kabla kura hazijahesabiwa. Kufika Mwanza na kuona mtu wao kashindwa na CHADEMA na kuwa akapatwa na heartattack, wakaondoka na kuelekea Shinyanga. Huko wakakuta yaleyale kwamba CHADEMA imeshinda. Wakatoa sanduku lenye kura zao za bandia na kumpa Mkurugenzi wa kutangaza matokeo na kumwambia: TANGAZA KUWA CCM IMESHINDA. Hata kijana wao wa CCM waliyekuwa wamemuweka pale akakana na kusema LAKINI JAMANI NI KWELI CHADEMA IMESHINDA. bado mwenyekiti na Makamba wake wakasisitiza kuwa ni CCM ndo imeshinda, bila ya kukumbuka hapo zamani Shinyanga kulitokea nini wakati Mwinyi alikuwa huko. Je hii ni demokrasia kweli? CCM walijua wazi kwamba mwaka huu wanashindwa lakini kwa kuwa wana malengo yao ya ufisadi wa miaka mitano ijayo, walitayarisha kadi za kura maalum tayari kwa kuziingiza ili JK ashinde. Kumbukeni lori lenye kura za Rais tayari lililotokea mpakani Mbeya na mjini musoma. Je hii kweli ni demokrasia? Wewe utasemaje umeshinda kugombea urais wakati bado vituo 9 vilikuwa havijamaliza kuhesabu kura ? Utasemaje umeshinda wakati ni 5 ya 45 milioni waliopkupigia kura? Kwa nini miji mingi mikubwa imechagua kuwapa kura CADEMA? Lazima watu wameona uppuzi wa CCM tangu Mwalimu afariki, sasa hivi CCM inaendeshwa na mafisadi na wezi wa mali ya taifa. JK kumbuka una kazi nzito mbele yako, kuongoza taifa ambalo halikubaliani na uongozi wako. Huyo katibu mkuu wa CCM ni mtu wa kuangalia zana. Alipokuwa mkuu wa wilaya ya Tanga alifanya nini? Leo ukienda Tanga utadhani ni kijiji wala si jiji.
 
Huu ni UPUUZI, Watanzania tuko Million 45.
Waliojiandikisha kupiga kura eti ni Million 19
Waliopiga kura ni Million 8
Walio mchagua rais ni million 5
swali, Je Million 11 kwanini hawakupiga kura?
Utaratibu huu ni mbovu inabidi ufanyiwe marekebisho, hii ni kasoro kubwa sana kama tunataka kujenga demokrasia ya kweli. Wala nchi wanasema ni ushindi wa kishindo!!!!!!
Unachaguliwa na watu Million 5 ili uongoze watu million 45??!!

Wewe ulitaka na watoto (under 18) wakapige kura? Makosa makubwa yamefanyika kikifanya kitambulisho cha kupigia kura kuwa kinamtambulisha Mtanzania kila sehemu ya huduma ambako kinahitajika kitambulisho. Hiki kitambulisho kinatakiwa kuwa maalum kwa ajili ya kupiga kura ili kupata idadi kamili ya wapiga kura nchini.

Mimi huwa sikitumii kabisa mbali na kupiga kura!
 
Tanzania tuna demokrasia ya aina yake, aliyeko madarakani hata kama hapati kura kwa njia ya kura halali zilizopigwa lazima atengenezewe kura zake na lazima ashinde. Uliwahi kuona wapi anayegombea ndiye huyo huyo anayeagiza vyombo vinavyosimamia uchaguzi? Akiona anashindwa atawaambia nini walio chini yake? Atakubali wamtangaze kuwa ameshindwa?
 
Huu ni UPUUZI, Watanzania tuko Million 45.
Waliojiandikisha kupiga kura eti ni Million 19
Waliopiga kura ni Million 8
Walio mchagua rais ni million 5
swali, Je Million 11 kwanini hawakupiga kura?
Utaratibu huu ni mbovu inabidi ufanyiwe marekebisho, hii ni kasoro kubwa sana kama tunataka kujenga demokrasia ya kweli. Wala nchi wanasema ni ushindi wa kishindo!!!!!!
Unachaguliwa na watu Million 5 ili uongoze watu million 45??!!
Tatizo hata kujiandikisha kupiga kura ni DEMOCRACY YA MTU........... asipojiandikisha hakuna tunachomfanya
Kwenda kupiga kura ni DEMOCRACY YA MTU............................. asipopiga hakuna tunachomfanya
 
Tatizo siyo kutojiandikisha na wala siyo kutopiga kura bali ni kutokuwepo uwazi kwamba kweli watu idadi fulani ndiyo waliojiandikisha na kweli idadi fulani ndiyo ambao hawakupiga kura. Ni uwongo kusema kuwa watu milioni 19 wamejiandikisha wakati hakuna anayehakiki hilo, baadaye daftari linatolewa dakika za mwisho kabala ya uchaguzi ikiwa na mapungufu ya kutokuwepo majina ya baadhi ya watu wenye kadi zao. Swali likiulizwa Tume ya Uchaguzi inajiumauma. Hiyo ndiyo demokrasia unayoisema?
 
Tanzania haina Demokrasia yeyote ile mambo yanafanyika ni uozo mtupu na hata nashindwa kuelewa hawa wanaojichukulia madaraka bila idhini ya Majority roho zao hazi wahukumu? Kila mtu Tanzania anajua alichofanya JK na wenzake kwanini watutawale kwa mabavu? Kuna nini Ikulu mpk ang'ang'aniepo wakati hatumtaki? hawa sisiem wawe na adabu ipo siku kutalipuk ala kulipuka kwa sababu siamini kama uonevu huu utaendelea milele.
 
Tatizo hata kujiandikisha kupiga kura ni DEMOCRACY YA MTU........... asipojiandikisha hakuna tunachomfanya
Kwenda kupiga kura ni DEMOCRACY YA MTU............................. asipopiga hakuna tunachomfanya

Huoni kamahilo sio Tatizo la msingi............anayetakiwa kujiandikisha na kupiga kura anao ufahamu wa kutosha juu ya faida na hasara za yeye kutoshiriki haya?
 
Matata asante sana kwa kauli yako nzuri. Mimi kilichonitisha sana ni kile cha mwenyekiti na Katibu wa CCM kuchukua ndege hadi Mwanza kabla kura hazijahesabiwa. Kufika Mwanza na kuona mtu wao kashindwa na CHADEMA na kuwa akapatwa na heartattack, wakaondoka na kuelekea Shinyanga. Huko wakakuta yaleyale kwamba CHADEMA imeshinda. Wakatoa sanduku lenye kura zao za bandia na kumpa Mkurugenzi wa kutangaza matokeo na kumwambia: TANGAZA KUWA CCM IMESHINDA. Hata kijana wao wa CCM waliyekuwa wamemuweka pale akakana na kusema LAKINI JAMANI NI KWELI CHADEMA IMESHINDA. bado mwenyekiti na Makamba wake wakasisitiza kuwa ni CCM ndo imeshinda, bila ya kukumbuka hapo zamani Shinyanga kulitokea nini wakati Mwinyi alikuwa huko. Je hii ni demokrasia kweli? CCM walijua wazi kwamba mwaka huu wanashindwa lakini kwa kuwa wana malengo yao ya ufisadi wa miaka mitano ijayo, walitayarisha kadi za kura maalum tayari kwa kuziingiza ili JK ashinde. Kumbukeni lori lenye kura za Rais tayari lililotokea mpakani Mbeya na mjini musoma. Je hii kweli ni demokrasia? Wewe utasemaje umeshinda kugombea urais wakati bado vituo 9 vilikuwa havijamaliza kuhesabu kura ? Utasemaje umeshinda wakati ni 5 ya 45 milioni waliopkupigia kura? Kwa nini miji mingi mikubwa imechagua kuwapa kura CADEMA? Lazima watu wameona uppuzi wa CCM tangu Mwalimu afariki, sasa hivi CCM inaendeshwa na mafisadi na wezi wa mali ya taifa. JK kumbuka una kazi nzito mbele yako, kuongoza taifa ambalo halikubaliani na uongozi wako. Huyo katibu mkuu wa CCM ni mtu wa kuangalia zana. Alipokuwa mkuu wa wilaya ya Tanga alifanya nini? Leo ukienda Tanga utadhani ni kijiji wala si jiji.

Chagula wabeja sana Ong'wise .Shinyanga tuna hasira sana tunajiandaa kuwaadabisha akina Makamba na group lake wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa hapo ndipo watajua kama chama chao hatukitaki, kwa sasa tunamsubiri huyo mbunge wa Makamba tuone atashirikiana na nani kujenga shinyanga.Kwa sasa tumekubali maendeleo shinyanga yaende likizo kwa miaka 5 tutasubiri mbunge wa 2015 ndiyo tutaendelea kuijenga shinyanga yetu, SHY TOWN ni ya wana shinyanga si ya MAKAMBA, RIDHIWANI WALA KIKWETE ni ya wasukuma pamoja na ndugu zetu wakaazi wa hapa, hatuwezi kuchaguliwa kiongozi.Tunawa subiri chaguzi za serikali za mitaa kwa hamu tuwaadabishe mafisadi wale.KAENI MKAO WA KUSIKILIZA
 
naona hii itakuwa sayansi ya mbinu za uchaguzi kwamba unaretain wale unaojua watakuchagua wewe tu kwa kuwapitia na kuwahamasisha kisha unaachana na wale wanaokupinga. kwa hiyo utaona kuwa elimu ya ucahguzi ilikuwa poor. na watu walisikika wwakisema CCM itashinda Tu BWana ya nini kupuiga kura? Mwishowe kweli wakashinda. ni jukumu la wapinzani pia kutoa elimu ya wapiga kura
 
Back
Top Bottom