Demokrasia: CCM na m/kiti wanapotumia mali za umma ila upinzani ni marufuku au intelejensia ya uvunjifu wa amani

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,867
FB_IMG_1503739849053.jpg
Nchi ya kidemokrasia, nchi ya mfumo wa vyama vingi. CCM wanatumia chuo cha umma kufanya makongamano na mikutano ya ndani. Vyama vya upinzani haviruhusiwi kutumia "premises" za aina hiyo (vyuo vya umma) kufanya mikutano ya ndani wala makongamano. Na wakifanya sehemu nyingine watavurugwa na polisi.

Kitu pekee wanachoruhusiwa ni mikutano ya nje. Tena ihutubiwe na mbunge/diwani wa eneo husika. Sasa ole wako ukahutubie jimbo/kata isiyo yako. Utataja majina yote ya Rais Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga. Rejea kilichotokea Tarime.

Hii si sawa hata kidogo. Huu ni upendeleo wa waziwazi. Kiongozi anayependa usawa na anayejiita "mpenzi wa Mungu" lazima akemee hali hii. Sisemi CCM waache operation zao, hapana. Waendelee, lakini fursa hiyo pia vipewe vyama vingine. Na vyenyewe viwe na platform ya kufanya siasa kwa uhuru kama CCM wanavyofanya.

Ili CCM ijipime uimara wake lazima itoe fursa sawa ya ushindani kwa vyama vingine vya siasa. Vinginevyo CCM itadumaa bila kujua maana imepigana na mtu aliyefungwa mikono. Ni sawa na umfunge mikono na miguu John Cena halafu umshindanishe na Ebitoke. Definately Ebitoke atamshinda, lakini hicho hakiwezi kuwa kipimo cha uimara wa Ebitoke.

So CCM iache uoga. Iruhusu ushindani huru, ushindani wa haki, ushindani wa kidemokrasia, ili iweze kujipima vizuri. Serikali kukandamiza upinzani na kuipa upendelea CCM sio kuisaidia, ni kuipoteza na kuiharibu CCM.

And by the way najaribu kuwaza hivi jana JPM angeenda Kigamboni akute vijana wa Chadema ndio wenafanya kongamano hapo Mwalimu Nyerere, possibly saizi tungekua tunaongea habari zingine. Labda uteuzi wa IGP mpya, RPC mpya na OCD mpya. Upinzani nchi hii ni kama utumwa.!
 
Mtaji wa Kura 56% ukitoa uchakavu baada ya miaka mitano 15% ni wazi kuwa yuko kwenye danger zone safari ijayo vituko ni lazima.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom