FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 36,035
- 40,700
Demokrasia ndani ya Afrika ni nyenzo ya ukoloni mamboleo. Hivi umeshawahi kujiuliza ni kwanini mabepari/ mabeberu hupenda sana kuona nchi za Afrika zikizingatia demokrasia na haki za binadamu? Na hawakupi msaada kama huzingatii demokrasia na haki za binadamu (wapinzani).
Jibu ni rahisi sana, demokrasia (upinzani) ni sauti ya mabeberu ndani ya nchi husika, hasa bungeni. Beberu hufanikiwa kupenyeza maslahi yake kwa kutumia sauti yake (wabunge wa upinzani) kwani wengi ni njaa na ni rahisi kununuliwa na kuwa vibaraka wa mabeberu, hupewa kila wanachohitaji kushinda chaguzi ili wakawe sauti ya bepari bungeni.
Hivyo basi kuminya upinzani na demokrasia kwa ujumla ni sawa na kuiminya sauti ya beberu kiasi cha kushindwa kupenyeza maslahi yake, hivyo ni lazima atakushinikiza uheshimu demokrasia kwa kukunyima misaada, sharti la ushoga ni decoy tu, lakini lengo kuu ni demokrasia ambayo ndio mlango wanaotumia kutikisa na kuingilia nchi za Afrika kwa mgongo wa upinzani, Kagame sio mjinga kuuona huu mtego.
Ilifikia hatua mbunge aliyekuwa anapigia kelele suala la mikataba mibovu ya madini, na kisha baada ya mikataba hiyo hiyo kufumuliwa anabadilisha gia angani na kusema eti tutashtakiwa MIGA sijui, kumbe ni mabeberu yanamtumia tu kama microphone kufikisha vitisho, halafu anatumika kuleta ujumbe wa blackmail kwamba tusiporuhusu makontena ya mchanga eti ndege yetu itakamatwa huko Canada, msaliti hana aibu!
Sasa hata ingekuwa wewe ndio bepari, usingeipenda demokrasia Afrika? Sasa unapoiminya demokrasia na kukiuka za haki za binadamu kwa kummiminia njugu kama mvua huyo msaliti ni lazima bepari apige kelele kwamba unavunja haki na demokrasia, hata msaada lazima akunyime kukushinikiza, na sisi tulivyo majinga tunaimba haki na demokrasia kama misukule!
Bepari akiona unambana mbavu kama jiwe anavyofanya, basi karata yake huwa ni kutumia upinzani kuendesha maandano ya 'amani' na kufanya mikutano ya kuwalisha sumu wananchi; sasa hata ingekuwa wewe ndio jiwe ungekubali kuona adui yako anaitumia demokrasia kama fimbo ya kukumaliza? Je, hutaivunjilia mbali hiyo fimbo?
Bepari siku zote anaangalia maslahi yake, ilifikia mahali akawa anahonga wafanyakazi wa mabwawa ya kuzalisha umeme ili wafungulie maji na kutengeneza uhaba wa umeme ili watukodisha ma-symbion na ma-aggeko yao ya kinyonyaji! Leo tunajenga stieglers gorge wapinzani wazito kama kabwe wanakuja kupaza sauti ya bepari eti tunaharibu mazingira?
Jiwe endelea kuminya demokrasia na kusigina haki za binadamu hadi mabeberu wajambe damu na kuharisha urojo mwekundu
===============================
Update: 19/01/2021
================================
Update: 15/11/2020
UPDATE: 03/11/2020
============================
UPDATE: 04/10/2020
Mnaowaita Mabeberu wamekohoa sasa
===============================
UPDATE: 18/12/2018
Haya ndio majibu dhaifu ya Zitto juu ya uzi huu
A Joint Declaration by Leaders and Senior Members of Six Opposition Parties who met in Zanzibar on 16th - 18th December, 2018 to deliberate on the Sta - JamiiForums
================================
Update: 21/01/2019
Mabeberu wanajihami biashara yao ya Majenereta ya kufua umeme isije ikaota nyasi, kuna wabunge wanatumika vibaya kuhujumu maendeleo
Sub-update: 12/05/2020
Kampuni ya ElSewedy Electric Co inayotengeneza bwawa la umeme Rufiji imewekewa vikwazo, haitaweza kukopesheka nje - JamiiForums
==============================
Beberu anavyotumia demokrasia kuipindu aserikali ya Venezuela yenye utajiri wa mafuta duniani.Demokrasia nyoko!
=============================
09/02/2019
Rais Erdogan wa Uturukia awaaibisha mabeberu juu ya demokrasia na wanachokifanya Venezuela
Update: 22/06/2019
=================================
=================================
PIA SOMA:
=================================
=================================
=================================
Update: 25/01/2020
=================================
Update: 31/01/2020

Uchaguzi 2020 - Marekani: Kuanzia leo, tunaweka vizuizi kwa waliohusika na kuvuruga Uchaguzi nchini Tanzania
Kupitia akaunti yake ya Twitter, Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Mike Pompeo ameandika "Kuna matokeo ya kuingilia mchakato wa kidemokrasia. Kuanzia leo, tunaweka vizuizi vya visa kwa wale wanaohusika na uvurugaji wa uchaguzi nchini Tanzania. Tunabaki kujitolea kufanya kazi pamoja kuendeleza...
www.jamiiforums.com
Update: 15/11/2020
ICC yakiri kupokea rasmi malalamiko kutoka Tanzania juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa uchaguzi uliopita
The International Criminal Court (ICC) in The Hague, has confirmed receipt of two formal letters alleging human rights violations by the Tanzania government in the wake of the October 28 election and its aftermath. The Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo), one of the main...
www.jamiiforums.com
UPDATE: 03/11/2020
Widespread Irregularities Observed during the Tanzanian Elections - United States Department of State
The United States commends the Tanzanian people for attempting to exercise their right to vote in the October 28 general elections. However, we remain deeply concerned by credible reports of significant and widespread voting irregularities, internet interruption, arrests, and violence by...
www.state.gov
============================
UPDATE: 04/10/2020
Mnaowaita Mabeberu wamekohoa sasa
===============================
UPDATE: 18/12/2018
Haya ndio majibu dhaifu ya Zitto juu ya uzi huu
A Joint Declaration by Leaders and Senior Members of Six Opposition Parties who met in Zanzibar on 16th - 18th December, 2018 to deliberate on the Sta - JamiiForums
================================
Update: 21/01/2019
Mabeberu wanajihami biashara yao ya Majenereta ya kufua umeme isije ikaota nyasi, kuna wabunge wanatumika vibaya kuhujumu maendeleo
Sub-update: 12/05/2020
Kampuni ya ElSewedy Electric Co inayotengeneza bwawa la umeme Rufiji imewekewa vikwazo, haitaweza kukopesheka nje - JamiiForums
==============================
Beberu anavyotumia demokrasia kuipindu aserikali ya Venezuela yenye utajiri wa mafuta duniani.Demokrasia nyoko!
=============================
09/02/2019
Rais Erdogan wa Uturukia awaaibisha mabeberu juu ya demokrasia na wanachokifanya Venezuela
Update: 22/06/2019
=================================
Maskini Dar es Salaam imeanza kushikwa shikwa sasa
......Waamerika ni watu wabaya, wameanza kutia mdomo Dar es salaam ya Watanzania, maskini wee, mji mzuri kwa jina lake, ila sasa unatafutiwa sababu kuchafuliwa. Waamerika ni ndumi la kuwili, ni watu wenye choyo na hasada sana kwa mafanikio ya wenzao, na hasa pale wasipokuwa na maslahi ya moja...
www.jamiiforums.com
Canada yaungana na Marekani na Uingereza kuelezea wasiwasi wao juu ya kuzorota kwa Haki za raia Nchini
Ubalozi wa Canada umesema unaungana na ubalozi wa Marekani na Uingereza katika kutilia wasiwasi wa uzorotaji wa utoaji haki nchini Tanzania.
www.jamiiforums.com
PIA SOMA:
=================================
Uarabuni hamna demokrasia, hamna umaskini
1. Nimetembea na kuishi nchi kadhaa za Qatar, UAE (Dubai, Abu Dhabi na Sharjah), Oman, Kuwait, Saudi Arabia na Bahrain sikuwahi kuona wazawa maskini. 2. Hakuna NGO's kama Afrika. 3. Hakuna kinachoitwa "Demokrasia". Sasa, huku Afrika 24/7 NGOs kila mtaa, vyama vya upinzani kila kukicha...
www.jamiiforums.com
Libya ya Gadaffi vs Libya ya Wamarekani
www.jamiiforums.com
Update: 25/01/2020
Tanzania yatajwa kuwa miongoni mwa nchi 7 zinazotarajiwa kuwekewa vikwazo vya kuingia Marekani
Serikali ya Marekani chini ya Rais Mtata, Donald Trump imetangaza kuwa iko mbioni kuziongeza nchi nyingine 7 kwenye orodha ya nchi ambazo Wananchi wake watawekewa vikwazo vya kuingia nchini humo (Marekani) Tanzania imetajwa pamoja na nchi za Belarus, Eritrea, Kyrgyzstan, Myanmar, Nigeria na...
www.jamiiforums.com
=================================
Update: 31/01/2020
Zuio la Watanzania kwenda Ng’ambo: Paul Makonda awa kiongozi wa kwanza kuzuiwa kuingia Marekani
Serikali ya Marekani imemzuia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuingi nchini humo kutokana na kuhusika kwake kwenye uvunjifu wa Haki za Binadamu unaohusisha kunyima haki ya kuishi, uhuru na ulinzi wa watu. Katika uongozi wake, Makonda ameonesha uonevu kwa wapinzani, kuminya uhuru wa...
www.jamiiforums.com
Watanzania wazuiliwa kucheza bahati nasibu ya kupata ukazi wa kudumu (Green Card) Marekani
Wadau Vyombo vya habari nchini Marekani vinaripoti kuwa raia wa Tanzania wamepigwa marufuku kushiriki katika mchezo wa bahati nasibu wa kupata viza ya kuingia Marekani. Bahati nasibu hiyo hutoa visa kwa watu takribani 50,000 kutoka nchi zenye kasi ndogo ya maendeleo kila mwaka kuingia na...
www.jamiiforums.com