Demokrasia barani Afrika ni ya kuogopa kama ukoma, mwenye hoja ya kupinga aje ulingoni

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,023
40,693
Demokrasia ndani ya Afrika ni nyenzo ya ukoloni mamboleo. Hivi umeshawahi kujiuliza ni kwanini mabepari/ mabeberu hupenda sana kuona nchi za Afrika zikizingatia demokrasia na haki za binadamu? Na hawakupi msaada kama huzingatii demokrasia na haki za binadamu (wapinzani).

Jibu ni rahisi sana, demokrasia (upinzani) ni sauti ya mabeberu ndani ya nchi husika, hasa bungeni. Beberu hufanikiwa kupenyeza maslahi yake kwa kutumia sauti yake (wabunge wa upinzani) kwani wengi ni njaa na ni rahisi kununuliwa na kuwa vibaraka wa mabeberu, hupewa kila wanachohitaji kushinda chaguzi ili wakawe sauti ya bepari bungeni.
Hivyo basi kuminya upinzani na demokrasia kwa ujumla ni sawa na kuiminya sauti ya beberu kiasi cha kushindwa kupenyeza maslahi yake, hivyo ni lazima atakushinikiza uheshimu demokrasia kwa kukunyima misaada, sharti la ushoga ni decoy tu, lakini lengo kuu ni demokrasia ambayo ndio mlango wanaotumia kutikisa na kuingilia nchi za Afrika kwa mgongo wa upinzani, Kagame sio mjinga kuuona huu mtego.

Ilifikia hatua mbunge aliyekuwa anapigia kelele suala la mikataba mibovu ya madini, na kisha baada ya mikataba hiyo hiyo kufumuliwa anabadilisha gia angani na kusema eti tutashtakiwa MIGA sijui, kumbe ni mabeberu yanamtumia tu kama microphone kufikisha vitisho, halafu anatumika kuleta ujumbe wa blackmail kwamba tusiporuhusu makontena ya mchanga eti ndege yetu itakamatwa huko Canada, msaliti hana aibu!

Sasa hata ingekuwa wewe ndio bepari, usingeipenda demokrasia Afrika? Sasa unapoiminya demokrasia na kukiuka za haki za binadamu kwa kummiminia njugu kama mvua huyo msaliti ni lazima bepari apige kelele kwamba unavunja haki na demokrasia, hata msaada lazima akunyime kukushinikiza, na sisi tulivyo majinga tunaimba haki na demokrasia kama misukule!

Bepari akiona unambana mbavu kama jiwe anavyofanya, basi karata yake huwa ni kutumia upinzani kuendesha maandano ya 'amani' na kufanya mikutano ya kuwalisha sumu wananchi; sasa hata ingekuwa wewe ndio jiwe ungekubali kuona adui yako anaitumia demokrasia kama fimbo ya kukumaliza? Je, hutaivunjilia mbali hiyo fimbo?

Bepari siku zote anaangalia maslahi yake, ilifikia mahali akawa anahonga wafanyakazi wa mabwawa ya kuzalisha umeme ili wafungulie maji na kutengeneza uhaba wa umeme ili watukodisha ma-symbion na ma-aggeko yao ya kinyonyaji! Leo tunajenga stieglers gorge wapinzani wazito kama kabwe wanakuja kupaza sauti ya bepari eti tunaharibu mazingira?

Jiwe endelea kuminya demokrasia na kusigina haki za binadamu hadi mabeberu wajambe damu na kuharisha urojo mwekundu
===============================
Update: 19/01/2021

================================
Update: 15/11/2020


UPDATE: 03/11/2020

Screenshot_20201103-131045.png


============================
UPDATE: 04/10/2020

Mnaowaita Mabeberu wamekohoa sasa
===============================
UPDATE: 18/12/2018
Haya ndio majibu dhaifu ya Zitto juu ya uzi huu
A Joint Declaration by Leaders and Senior Members of Six Opposition Parties who met in Zanzibar on 16th - 18th December, 2018 to deliberate on the Sta - JamiiForums

================================

Update: 21/01/2019
Mabeberu wanajihami biashara yao ya Majenereta ya kufua umeme isije ikaota nyasi, kuna wabunge wanatumika vibaya kuhujumu maendeleo


Sub-update: 12/05/2020
Kampuni ya ElSewedy Electric Co inayotengeneza bwawa la umeme Rufiji imewekewa vikwazo, haitaweza kukopesheka nje - JamiiForums

==============================
Beberu anavyotumia demokrasia kuipindu aserikali ya Venezuela yenye utajiri wa mafuta duniani.Demokrasia nyoko!

=============================
09/02/2019
Rais Erdogan wa Uturukia awaaibisha mabeberu juu ya demokrasia na wanachokifanya Venezuela



Update: 22/06/2019
=================================
=================================

PIA SOMA:
=================================
=================================
=================================
Update: 25/01/2020

=================================
Update: 31/01/2020


==============================

 
mwambie jiwe siasa sio vita na Tanzania sio mali yake

pia mwambie awekeze kwenye elimu na kilimo

kuuwa upinzani sio kipaumbele cha raia

mikataba mibovu ilisainiwa na chama cheke aache ujinga kabisa

Watanzania sio wajinga ni wavumilivu tu ila vikwazo vikija hatutomvumilia kabisa
 
Kwamba nawe umetoa hoja . Kwa kweli wafuasi wa Lumumba hamna uwezo wa kujieleza . Waliowapa hao mabeberu migodi, Gas na mafuta ni wapinzani kweli? Wakati wapinzani wakifukuzwa bungeni ili miswaada ipite nani walihusika? Je, wajua sauti inayopitisha upumbavu ni ile ya ndiyo, ni sauti ya nani hiyo?

Wewe hata shule za MEMKWA hukumaliza , hujielewi, hujiwezi na huna hoja.
 
Kwamba nawe umetoa hoja . Kwa kweli wafuasi wa Lumumba hamna uwezo wa kujieleza . Waliowapa hao mabeberu migodi , Gas na mafuta ni wapinzani kweli ?! Wakati wapinzani wakifukuzwa bungeni ili miswaada ipite nani walihusika ?! Je wajua sauti inayopitisha upumbavu ni ile ya ndiyooooooo, ni sauti ya nani hiyo ?!.

Wewe hata shule za MEMKWA hukumaliza , hujielewi, hujiwezi na huna hoja.
Kwahiyo awamu iliyopo haina haki ya kurekebisha madudu yaliyofanywa awamu zilizopita? Halafu masuala ya chama yanakujaje hapa?
 
Hizi nchi zinazolazimisha ushoga ni serikali zao na wengi wa wananchi hawapendi huu ushenzi.
Nilikutana na marafiki zangu wa muda mrefu baada ya salaam nikamuuliza mmoja so how's your son mwenzake akaruka na kusema kijana kawa gay.

Jamaa aliona aibu sana na hakujibu kitu ila mwenzake akaongezea kuwa dogo aliondoka na kuhamia nchi jirani ambapo anafanya kazi ya saloon. Wanalazimisha tuwe na uhuru lakini hata wao hawafurahii ila ni mkakati wa kupunguza uzazi tu
Rais aliposema tuzaane sana alikuwa anajua zaidi
 
Kama maslahi ya mabeberu kwetu ni mikataba minono ya madini na gesi, ungeonyesha ni namna gani upinzani umesaidia kuwafanikishia hayo waliokwisha chuma. Kama ni kuingiza ushoga ungeonyesha kutokuwepo kwa ushoga kabla ya 1992, au huu uliopo sasa umeletwa na sheria ipi iliyopitishwa bungeni.
 
Kama maslahi ya mabeberu kwetu ni mikataba minono ya madini na gesi, ungeonyesha ni namna gani upinzani umesaidia kuwafanikishia hayo waliokwisha chuma. Kama ni kuingiza ushoga ungeonyesha kutokuwepo kwa ushoga kabla ya 1992, au huu uliopo sasa umeletwa na sheria ipi iliyopitishwa bungeni.
Awamu zilizopita mabeberu hawakuhitaji upinzani kufanikisha maslahi yao kwani zilikuwa ni awamu zenye maelewano na mabeberu, to put simply ni kwamba walikubali mabeberu wafanye wanavyotaka hivyo hawakuhitaji kuitumia karata ya upinzani na demokrasia.

ila awamu hii imekuja kuwabana, wanatumia karata ya demokrasia na haki za binadamu ili watuvuruge kama walivyowafanya wa-Libya, hadi wakamuua jemedari wa Afrika Muammar Gadaffi, leo wanateseka kama mbwa koko, na wao walifurahia alipouawa, bepari mbaya sana! Mi nasema demokrasia na haki za binadamu kama yuke aliyeenda kutalii kwa lazima ubelgiji ziminywe tu, hatuwezi kumchukia kiongozi wetu kisa bepari anafanya maisha yawe magumu ili tuanze kuandamana, Libya leo wanaishi kama mbwa koko wakati walikuwa na kila kitu.

leo beberu anafyonza mafuta kama yake. Kule Iraq 2003 nadhani tunakumbuka bepari alichofanya kwa mgongo wa demokrasia na utawala bora, eti wajadai Saddam ananyanyasa watu wake, pia wakasingizia eti ana mabomu ya hatari, wa-Iraq wakajaa kingi na kung'oa masanamu ya Saddam wao wenyewe, alichokifanya beberu sina hata haja ya kueleza, leo anafyonza mafuta kama kisina cha bibi yake! Alikuwa wapi beberu wakati watutsi wanachinjwa kama kuku Rwanda 1994 kama anajali sana haki za Wa-Afrika? Mbina moyo aliouonyeaha Libya hukuuonyesha Rwanda? Ni sababu hapakuwa na maslahi (Mafuta).

Alaaniwe beberu na fimbo anayotuchapia ya demokrasia na utawala bora, to hell with democracy!
 
Hakuwa na final say, ni maelekezo toka juu, ila kwa sasa ana final say
kwenye utawala wa Mzee Jakaya Kikwete (JK) jamaa ndio alipopatia umaarufu nadhani

pia JK alikuwa anawaheshimu saana mawaziri na walikuwa na nguvu haswa

utawala wa JK Mawaziri pendwa walikuwa Rais Magufuli na membe aliitumia hiyo fursa kufanya nini kwe ujenzi.
 
kwenye utawala wa JK jamaa ndio alipopatia umaarufu nadhani

pia jk alikuwa anawaheshimu saana mawaziri na walikuwa na nguvu haswa

utawala wa jk mawaziri pendwa walikuwa jpm na membe aliitumia hyo fursa kufanya nini kwe ujenzi
Rais ndie alikuwa na final say
 
Back
Top Bottom