Demokrasi na Tanzania

Abu Hamdy

Member
Jun 27, 2016
29
17
Utafiti niliyoufanya kwa nchi nyingi duniani bila kutawala na Iron Fist maendeleo hayapatikani, mfano Russia kabla ya Putin kuchukua madaraka nchi hiyo ilikuwa na hali mbaya ya kiuchumi,ufisadi na matumizi mabaya ya mali ya umma kiasi ambacho hadhi ya Urusi kama super power ilipotea, toka Putin achukue madaraka kwa kutumia Iron Fist uchumi wa Urusi umekuwa kwa kasi ufisadi umekwisha na maisha ya warusi yamekuwa mazuri.

Hapa Tanzania vyama vya siasa zinatakiwa zielemishwe nini maana ya demokrasi kwani kutoka nje ya bunge ama kuitisha maandamano na mikutano sio kuitakia mema Tanzania. Kwa kipindi kifupi cha utawala wa Rais John Magufuli mabadiliko makubwa yamefanyika najua yana maumivu makali kwa baadhi ya watu.

Watanzania wengi wanataka kuiona nchi yao yenye matumaini katika maisha yao ya baadaye na dalili za utawala wa Rais Magufuli inaleta matumaini.

Kwa jinsi ya utawala wa Rais Magufuli ulivyoaanza we can see the light at the end of tunnel.
 
Back
Top Bottom