Democratic wamkalia kooni Trump, asusia kikao

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
Mvutano kati ya Rais wa Marekani, Donald Trump na viongozi wa chama cha Democratic kuhusu ujenzi wa ukuta wa mpakani unaotakiwa na rais huyo, umeingia sura mpya baada ya Trump kuondoka kwa hasira kwenye mazungumzo.

Tofauti kuhusu ukuta huo kwenye mpaka kati ya Marekani na Mexico, ambao umekataliwa na wanachama wa chama cha Democrats, umesababisha kufungwa kwa baadhi ya wizara na Idara kadhaa za serikali kwa muda wa siku kumi na tisa sasa.
Katika mkutano huo baina ya Rais Trump na viongozi wa chama cha Democratic bungeni, Nancy Pelosi ambaye ni spika wa baraza la wawakilishi na Chuck Schumer, kiongozi wa wanachama wa Democrats katika baraza la seneti, haukudumu kwa muda mrefu.

Aidha, mazungumzo baina yao yalikuwa yakijaribu kwa mara nyingine kutafuta muafaka wa kumaliza mkwamo wa shughuli za serikali, ulioanza siku 19 zilizopita baada ya Trump kukataa kusaini mpango wa bajeti ambao haujumuishi dola bilioni 5.7 anazozitaka kwa ajili ya ujenzi wa ukuta katika mpaka baina ya Marekani na Mexico, ambao ni ahadi yake kuu ya kampeni yake ya urais.

Hata hivyo, katika ukurasa wake wa Twitter, Trump ameandika kuwa ”Nimeondoka sasa hivi katika mkutano na Chuck na Nancy, ambao ulikuwa ni kupoteza muda kabisa. nimewauliza ikiwa nitazifungua haraka shughuli za serikali, kipi kitafanyika katika siku 30 zitakazofuata, mtaridhia fedha za kujenga ukuta mpakani, Nancy akajibu ‘hapana’, nikawaambia, ‘kwa heri, hakuna kitakachofanyika hapa’
 
nchi zinazofata sheria ndio nchi zinazoendelea,mawazo ya mtu mmoja mmoja hayawezi hata kujenga nyumba achilia mbali nchi,hapa tz tunapotezeana wakati tu.
Ila mawazo ya mtu mmoja yamesababisha tukanunua ndege sits bdani ya miaka mi3; na kwa mawazo ya mtu mmoja zile ndege 2 za Rais zitakuwa za biashara pia. Kwa mawazo ya mtu mmoja (anayesadikika kuwa na akili nyingi sana) uwanja wa ndege wa kimataifa wa Chuttle (CIA) umejengwa ili air bus itue huko.

Kwa mawazo ya mtu mmoja wanasiasa wanajaza mahabusu; wanapotea au kupotezwa'; wananusurika kuuwawa.

Kwa mawazo ya mtu mmoja tu 'wadanganyika' wanapiga vigelegele na kushangilia.

Dah!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania itajengwa na wenye moyo!
Hiki ni kipindi cha mabadiliko sio mahaba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mvutano kati ya Rais wa Marekani, Donald Trump na viongozi wa chama cha Democratic kuhusu ujenzi wa ukuta wa mpakani unaotakiwa na rais huyo, umeingia sura mpya baada ya Trump kuondoka kwa hasira kwenye mazungumzo.

Tofauti kuhusu ukuta huo kwenye mpaka kati ya Marekani na Mexico, ambao umekataliwa na wanachama wa chama cha Democrats, umesababisha kufungwa kwa baadhi ya wizara na Idara kadhaa za serikali kwa muda wa siku kumi na tisa sasa.
Katika mkutano huo baina ya Rais Trump na viongozi wa chama cha Democratic bungeni, Nancy Pelosi ambaye ni spika wa baraza la wawakilishi na Chuck Schumer, kiongozi wa wanachama wa Democrats katika baraza la seneti, haukudumu kwa muda mrefu.

Aidha, mazungumzo baina yao yalikuwa yakijaribu kwa mara nyingine kutafuta muafaka wa kumaliza mkwamo wa shughuli za serikali, ulioanza siku 19 zilizopita baada ya Trump kukataa kusaini mpango wa bajeti ambao haujumuishi dola bilioni 5.7 anazozitaka kwa ajili ya ujenzi wa ukuta katika mpaka baina ya Marekani na Mexico, ambao ni ahadi yake kuu ya kampeni yake ya urais.

Hata hivyo, katika ukurasa wake wa Twitter, Trump ameandika kuwa ”Nimeondoka sasa hivi katika mkutano na Chuck na Nancy, ambao ulikuwa ni kupoteza muda kabisa. nimewauliza ikiwa nitazifungua haraka shughuli za serikali, kipi kitafanyika katika siku 30 zitakazofuata, mtaridhia fedha za kujenga ukuta mpakani, Nancy akajibu ‘hapana’, nikawaambia, ‘kwa heri, hakuna kitakachofanyika hapa’
Ameshasema atachukua budget ya hela ya dharura
 
Huyo jamaa kama mtoto wa kike ..yeye akizidiwaga hoja tu basi ananuna ... nafsi yake imejaa ubinafsi so anapenda kusikia kile tu ambacho yeye ana kiamini ..hata kama hakipo sahihi ... mxiiisswuuhh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom