Déjà Vu inathibitisha binadamu tulishawahi kuishi maisha tunayoishi leo tangia kale

exac

exactlly mkuu, huwa inanitokea sana
Ukiona hivyo ujue kwanza ubongo wako una afya nzuri ndio maana unaweza kupata déjà vu kirahisi.

Wewe huwa unafikiri ni nini? Kwani I unayaona maisha uliyowahi kuyaishi?
 
me huwa nadhani katika ulimwengu huu tunaoishi kuna siri nyingi sana na mambo mengi huwa hayaonekani kwa kutazama but huwa ni kama feelings zinakuja ghafla then ukitaka kumwelezea mtu jinsi unavyojisikia kwa ile vision uliyoiona unajikuta huwezi kumhadithia unaishia kuijua wewe tu pekeee
 
Iko hivyo Dunia ina mengi sana ya sirini na hapa Duniani tunaishi Kwenye Dunia mbili inayoonekana na isiyoonekana vyote vipi hapa hapa chini ya jua.

Na dhumuni la secret society kama Illuminate na Freemasons ni kuelewa hii invisible universe ili warahisishe maisha zaidi. Ndio maana hata neno Illuminati linatokana na illuminate, illumination, illuminated likiwa na maana "Mwangaza au Nuru" au kuexpose kitu by lighting it. Kukiangazia ili kionekane. Kuangazia ya sirini ili Dunia iyaone.

Déjà vu its the best experience sir.
 
ukweli mtupu mkuu
 
Good day, good people!

Déjà vu ni neno lenye asili ya kifaransa likimaanisha "already seen, lived" yaani unakutana na situation, event, scenario au hali yeyote ambayo unakuja kugundua ulishawai kuishi hiyo hali au hayo maisha ya muda huo zamani iliyopita. Hiyo ndio inakuwa déjà vu. Yaani akili yako na roho yako inakiri kabisa ulishawai kuona, kukutana au kuhisi kitu flani hapo zamani but umekutana nacho tena ukiwa na umri huo huo na muda huo huo..then akili na nafsi yako zinakiri kabisa Ku experience na kuishi that situation before. Then that's déjà vu.

Kilichonifanya nikaandika haya ni kwamba Leo Niko hapa kigali, Rwanda sehemu moja inaitwa kanombe....nilikuwa nataka kupata lunch hivyo nikajikuta nimeenda straight hadi kwenye restaurant ambayo nikajikuta nahifahamu kwa jina though iko Rwanda na sijawahi kufika before..hii nikaignore but nilipoingia ndani mhudumu aliekuja kunihudumia alikuwa anamuita yule wa kaunta mama na alinisemesha kinyarwanda nikamuelewa vizuri ilhali sijui kinyarwanda kabisa then nikaletewa msosi nilipoanza kula nikajikuta naijua scenario nzima itakayotokea hadi mwisho wake ambapo nilihisi wataniuliza juu ya bei na upatikanaji wa Mchele wa bongo... Na kweli mwishoni kabisa wakaniuliza juu ya Mchele wa bongo. Akili yangu ilikuwa imepigwa butwaa maana yale maisha Ninakumbuka niliwahi kuyaishi mwanzoni..but this time imetokea Rwanda hadi mgahawa naujua tena Kwa jina then hadi vitendo vyote. Wow! What's behind this? Labda kabla ya kuzaliwa niliwahi kuishi Rwanda? Sijui? Sasa nimeyajuaje kuanzia mazingira hadi mgahawa? I'm confused vibaya hapa!

Kimsimgi baada ya kufikiria kwa muda mrefu nimehisi kuna possibility our spirits might be very old...kabla hatujazaliwa kuna uwezekano tulikuwa tunaexist million of years back maana nina uhakika roho zetu zinauwezo wa kutambua hata maeneo, sura, vitu n.k tulivyovipitia miaka ya nyuma sana hivyo zilishawai kuyaishi hayo maisha husika.

Na kwa kupitia déjà vu nimeanza kuamini kwamba binadamu tunaishi kwenye illusion ya space and time and we are immortal and exist forever in the universe of infinity na roho inatuthibitishia kupitia ubongo kwamba haya maisha tulishawai kuyaishi hapo awali tukiwa na umri huu huu na muda ulikuwa huu huu.

Vipi ilishawai kutokea kwako umekutana na scenario ndogo then ubongo na roho yako vikakumbuka kwamba ulishawai kuipitia au kuishi back then? What your experience on this? Ilishatokea kwako?

View attachment 788767View attachment 788770
c9b9c9953dfed2fccb7fb510352982ba.jpg
 
Hiii dunia ina mambo sana..
Labda bado nipo kitandani nimelala na haya maisha yangu yote nayoyaishi huenda ni ndoto
 
Kwa sisi firstborn ni vitu vya kawaida sana hututokea mara lukuki hata biblia inasema mtoto wa kwanza ni mlango wa maono kwa familia
 
Kwa kawaida Ubongo ni kama mashine kuna kipindi hupata hitilafu zisizokuwa na madhara makubwa moja ya hitilafu hii ni pamoja na kuchelewa ku interprate taarifa( information) upande wa kushoto wa ubongo huhusika na lugha ( mazungumzo) na upande wa mwingine ni skill za kawaida
DÉJA HUTOKEA VIPI
Hali hutokea pale ambapo taarifa ku delay kufika kwenye ubongo kwa sababu imechelewa ubongo hufanya interpretation mara mbili kwa taarifa moja, note: hii hutokea ndani ya sekunde chache sana, mfano ukimuona mtu ukahisi ulishawahi kumuona sio kwamba kweli ulishawahi kumuona ni kwamba taarifa imeku duplicated mara mbili ( hitirafu yenyewe hii )

Matukio yote ya de ja vu hatujawahi kuyaona before ni duplication ya taarifa kwenye ubongo.

Sorry sio mfafanuzi mzuri ila kama ntakuwa nipo wrong ninaweza kurekebishwa
 
Kitu Kama hiki kilikuwa kinanitokea zamani nilipokuwa mdogo.Kuna sehemu nilikuwa naweza nikapita,mfano kwenye mto nikahisi upande wa pili wa mto uko hivi na ikawa kweli.Au nikafika eneo fulani nikahisi kabisa nilishawahi kufika eneo hivyo hiyo sio mara ya Kwanza.Lakini tokea nimekuwa mkubwa haijawahi nitokea.

Nakumbuka Kuna siku niliwahi kumshangaza mama nilipomweleza matukio ya sehemu fulani tulikuwa tunapita njiani.Ilikuwa ni zamani kidogo tulikuwa tunapita njiani kuelekea kijijini kwa Babu na ilikuwa mara yangu ya kwanza kwenda huko Magu-Mwanza.Akashangaa sana akasema matukio hayo yalishawahi tokea sehemu hiyo kabla sijazaliwa .Kuna sehemu tulipita kulikuwa Kuna uwanja nikamwambia "ni soko la kuuza ng'ombe" akashangaa akasema kweli zamani lilishawahi kuwa soko la kuuza mifugo.

Lakini kiujumla Mimi binafsi siamini hayo Mambo ya nafsi kuishi mara mbili.Ni hisia fulani tu huwa zipo.Imagine mtu unapita sehemu fulani unaiona nyumba unahisi ushawahi kuwa hapo zamani.Lakini hiyo nyumba unashangaa ina miaka hata kumi tu tokea ijengwe na wewe una miaka thelathini.kiuhalisia ni kitu ambacho hakiwezi kuwa uhalisia.
 
Kwa kawaida Ubongo ni kama mashine kuna kipindi hupata hitilafu zisizokuwa na madhara makubwa moja ya hitilafu hii ni pamoja na kuchelewa ku interprate taarifa( information) upande wa kushoto wa ubongo huhusika na lugha ( mazungumzo) na upande wa mwingine ni skill za kawaida
DÉJA HUTOKEA VIPI
Hali hutokea pale ambapo taarifa ku delay kufika kwenye ubongo kwa sababu imechelewa ubongo hufanya interpretation mara mbili kwa taarifa moja, note: hii hutokea ndani ya sekunde chache sana, mfano ukimuona mtu ukahisi ulishawahi kumuona sio kwamba kweli ulishawahi kumuona ni kwamba taarifa imeku duplicated mara mbili ( hitirafu yenyewe hii )

Matukio yote ya de ja vu hatujawahi kuyaona before ni duplication ya taarifa kwenye ubongo.

Sorry sio mfafanuzi mzuri ila kama ntakuwa nipo wrong ninaweza kurekebishwa
Best explanation so far
 
Good day, good people!

Déjà vu ni neno lenye asili ya kifaransa likimaanisha "already seen, lived" yaani unakutana na situation, event, scenario au hali yeyote ambayo unakuja kugundua ulishawai kuishi hiyo hali au hayo maisha ya muda huo zamani iliyopita. Hiyo ndio inakuwa déjà vu. Yaani akili yako na roho yako inakiri kabisa ulishawai kuona, kukutana au kuhisi kitu flani hapo zamani but umekutana nacho tena ukiwa na umri huo huo na muda huo huo..then akili na nafsi yako zinakiri kabisa Ku experience na kuishi that situation before. Then that's déjà vu.

Kilichonifanya nikaandika haya ni kwamba Leo Niko hapa kigali, Rwanda sehemu moja inaitwa kanombe....nilikuwa nataka kupata lunch hivyo nikajikuta nimeenda straight hadi kwenye restaurant ambayo nikajikuta nahifahamu kwa jina though iko Rwanda na sijawahi kufika before..hii nikaignore but nilipoingia ndani mhudumu aliekuja kunihudumia alikuwa anamuita yule wa kaunta mama na alinisemesha kinyarwanda nikamuelewa vizuri ilhali sijui kinyarwanda kabisa then nikaletewa msosi nilipoanza kula nikajikuta naijua scenario nzima itakayotokea hadi mwisho wake ambapo nilihisi wataniuliza juu ya bei na upatikanaji wa Mchele wa bongo... Na kweli mwishoni kabisa wakaniuliza juu ya Mchele wa bongo. Akili yangu ilikuwa imepigwa butwaa maana yale maisha Ninakumbuka niliwahi kuyaishi mwanzoni..but this time imetokea Rwanda hadi mgahawa naujua tena Kwa jina then hadi vitendo vyote. Wow! What's behind this? Labda kabla ya kuzaliwa niliwahi kuishi Rwanda? Sijui? Sasa nimeyajuaje kuanzia mazingira hadi mgahawa? I'm confused vibaya hapa!

Kimsimgi baada ya kufikiria kwa muda mrefu nimehisi kuna possibility our spirits might be very old...kabla hatujazaliwa kuna uwezekano tulikuwa tunaexist million of years back maana nina uhakika roho zetu zinauwezo wa kutambua hata maeneo, sura, vitu n.k tulivyovipitia miaka ya nyuma sana hivyo zilishawai kuyaishi hayo maisha husika.

Na kwa kupitia déjà vu nimeanza kuamini kwamba binadamu tunaishi kwenye illusion ya space and time and we are immortal and exist forever in the universe of infinity na roho inatuthibitishia kupitia ubongo kwamba haya maisha tulishawai kuyaishi hapo awali tukiwa na umri huu huu na muda ulikuwa huu huu.

Vipi ilishawai kutokea kwako umekutana na scenario ndogo then ubongo na roho yako vikakumbuka kwamba ulishawai kuipitia au kuishi back then? What your experience on this? Ilishatokea kwako?

View attachment 788767View attachment 788770

Experince uliyoipata inatokana in mpression ya past life. Binadamu akifa ya Roho inatafuta Mwili Mwingine na hii inatwa "REINCARNATION" iko kwenye mafundisho ya Elimu za kiroho na hasa kwenye western world. Kwa mfano nita Quote mistari kutoka kwenye kitabu kinaitwa "THE BHAVAGAD GITA" ni mafundisho ya KRISHNA kwa mwanafunzi wake ARJUNA. Krishna ni Eincarnation ya Roho takatifu ambayo huzaliwa duniani pale maovu yanapotamalaki ili kuirudishia dunia utakatifu huya alizaliwa kabla ya Kristo na inaaminika pia ndio Roho hiyo alizaliwa kwa Yesu kristo pia, zamani kulikuwa na ishara fulani kutambulisha uzalio Roho hiyo, ndio maana wale wataaramu na wajuzi wa nyota walitoka Iraq kwenda Israeli kumtafuta mtoto Yesu.

QUOTES:

"As a man discard his threadbare robes and put on new, so the spirit throws off Its worn-out bodies takes fresh one."

"For death is as sure for that which is born, as birth is for that which is dead"

"I Have no beginning, Though I am imperishable as well as Lord of all that exist, yet by My own will and power do I manifest myself. When spirituality decays and materialism is rampant, then, O Arjuna, I reincarnate Myself to protect the righteous, to destroy the wicked and to establish the kingdom of God I am reborn from Age to Age"

Krishna anajaribu kumtia moyo Jemadari Arjuna apigane vita kwani yeye aliona itakuwa na madhara makubwa na kusabisha vifo vya watu wake na ndugu zake. Anamwambia asiogope kufa kwani hata akifa atazaliwa tena, kwani kazi ni kazi tuu. Mbona yeye licha ya kwamba ni Roho ya Mungu mbona anatabika kuzaliwa na kufa kuja kuokoa dunia.

Hiki ni kitabu tuu lakini pia kuna proof za kisayansi kwani kuna magonjwa mengine mtu anaweza kuwanayo kwa kusababishwa ni impression from the past lifes iliatibiwe anafanyiwa HYPNOSIS, utakutwa kuwa watu miili inasisimuka, au kushtuka tuu, wengine anafinya macho, au anjiona anakataa as if anaona hali fulani then haitaki, wengine anakuwa waoga wa vitu fulani, HYPOZER anamrudisha back in time, kwenye past life, kuona kama kuna kitukilimtokea nadio kinasababisha madhara, anamfanya kukubali hali, iliajitibu kutibu.

Nilisoma kwenye scientific Journal moja zamani sana kwenye miaka ya themanini, Dada mmoja masikini tuu hivi, mfanyakazi ya mashamba ya kahawa (coffee plantation) huko America Kusini alikuwa na matatizo ya kisaikologia alikokwenda kufanyiwa Hypnosis akajigundua kuwa katika past lake, moja alikuwa ndiye alikuwa Queen Isabella wa Spain, alikumbuka siku aki mpa Amri mgunduzi Christopher Columbus akafanye ugunduzi wa ardhi ili Spain ipate makoloni ya kuzalisha malighafi na watumwa. Akapata umarufu sana press za kwao sana hadi akapata sponsor na kupewa tour ya kwenda kutembelea Castle la Malikia Isabelle huko Spain, aliwashangaza sana watu baada ya kuwaelekeza watunza Castle ni wapi Malikia alikuwa anaficha Jewels na vitu vya thamani, alijua ramani ya lile jengo in out zaidi alionyesha secrete chemba ambayo ni Queen to alikuwa anajia na hata waliofanya restoration hawaijua waliiziba.

REINCARNATION is real ndio kunasehemu unaweza enda for first time ukaona uko familiar sana au Mtu kama unamkumbuka sana.
 
Inanitokea sana mkuu na kuna vitu zaidi ya ivo.ukizingatia sisi twins ni kama tunaishia dunia mbili.
 
Kuna kipindi nilikuwa naota ndoto kuwa kuna sehemu ina majimaji na majanimajani halafu pembeni ya hayo majani kuna vyoo viwili na kimoja kina pazia ila kimoja hakina.
Hii ndoto ilikuwa inajirudia kwa mwezi mara moja. Na wala sikuwa naitilia maanani.

Basi ndoto ikakata na nikaendelea na maisha yangu.
Sasa siku moja nimeenda kumtembelea rafiki yangu maeneo ya Kipawa, tukaingia sehemu kula na akasema tutembee mwa mguu kwenda kwangu.
Ile tumepiga hatua kama kumi nageuka pembeni nikaona vyoo viwili, kimoja hakina pazia na kimoja kina pazia na hivo vyoo viko sehemu kama ina majimaji na majanimajani.
Yaani yale mazingira niliyoyaona ni sawasawa na ndoto niliyokuwa naipata kwa miezi karibu 3.
Palepale nikamwambia yule rafiki yangu, asante kwa kunipitisha njia hii....ndoto niliyokuwa naiota leo nimeiona.
Nilisimama kama dk 10 nashangaa yale ninayoyaona.
Hadi yule rafiki yangu akawa ananishangaa.

Haya mambo kweli yapo...na mimi ni shahidi.
Kweli yapo.
Sasa hii ni de ja vu?
 
Aisee Dunia ina mambo kwelii, thanks Humble African kwa Uzi huu though ndo nauona leo

Hii scenario mimi ishawahi nitokea mara mbili katika maisha yangu, ila kama ilivo kwa wengine pia naanza kuota af inakuja kutokea reality vile vile kama nilivyoota

Kwanza ilitokea wakati nina miaka 9 au 10 kama sikosei, ila sasa wakati situations inatokea nilipigwa na butwaa kama dk 2 hivi nawaza mbona kama nishawahi kufanya hichi nilichokifanya au hili tukio nilishawahi kuliishi before tena vile vile kuanzia mazingira, watu, vitu vilivyo around

Ya pili this year ukubwani, aisee yaan hapa ndo hadi nilitabasamu na kufurahi
Nilisimama zaidi ya dk 5 kutafakari what's behind this!!
Kiukweli nilifurahi sana tukio nililowahi kuliishi kutokea tena af likiwa vile vile

Asante Sana Humble African kwa Uzi
 
Kama Deja vu ni uthibitisho tuliwahi kuishi hapo kabla ya maisha haya
Je tuliishi maisha haya haya?? Maana muda mwingine deja vu huja katika hali unayohisi hiki kitu kimewahi kutokea na nimewahi kufanya na mazingira ni hayo hayo na watu ni hao.
 
Memories from unknown!!? . Yoo here because you known something but you cant tell yoo can learn and understand but you can't teach other.
 
Mkuu mbna MI naona km hyo ni lucid dream coz Unalala af unaota ndoto then cku unakutan na Hali kam unakumbuka kuwa nlishawah kuota ndoto ya namna hii mda mwingine unafany tukio Af unaona kam ulshawah kufany lkn hukumbk ni wap
 
Kuna kipindi nilikuwa naota ndoto kuwa kuna sehemu ina majimaji na majanimajani halafu pembeni ya hayo majani kuna vyoo viwili na kimoja kina pazia ila kimoja hakina.
Hii ndoto ilikuwa inajirudia kwa mwezi mara moja. Na wala sikuwa naitilia maanani.

Basi ndoto ikakata na nikaendelea na maisha yangu.
Sasa siku moja nimeenda kumtembelea rafiki yangu maeneo ya Kipawa, tukaingia sehemu kula na akasema tutembee mwa mguu kwenda kwangu.
Ile tumepiga hatua kama kumi nageuka pembeni nikaona vyoo viwili, kimoja hakina pazia na kimoja kina pazia na hivo vyoo viko sehemu kama ina majimaji na majanimajani.
Yaani yale mazingira niliyoyaona ni sawasawa na ndoto niliyokuwa naipata kwa miezi karibu 3.
Palepale nikamwambia yule rafiki yangu, asante kwa kunipitisha njia hii....ndoto niliyokuwa naiota leo nimeiona.
Nilisimama kama dk 10 nashangaa yale ninayoyaona.
Hadi yule rafiki yangu akawa ananishangaa.

Haya mambo kweli yapo...na mimi ni shahidi.
Kweli yapo.

Hii hali hata mimi inanitokeaga lakini kwa njia mbili mojawapo ni ndoto na nyingine hunitokea mara mojamoja nikiwa nimepata utulivu inakuja kama kumbukumbu ambayo ambayo haijawai kutokea lkn baada ya muda flani kupita inakuja kutokea.
 
Back
Top Bottom