Déjà Vu inathibitisha binadamu tulishawahi kuishi maisha tunayoishi leo tangia kale

Aisee ndio maana naipenda sana JamiiForums. Hii mada inanigusa sana kwa maana hili swala limeniweka katika fikra tofauti bila ya kupata ufumbuzi wa uhakika.

Imekuwa ikitokea mara kwa mara kwa upande wangu ninaweza fika eneo geni ambalo najua sijawahi kanyaga katika maisha yangu lakini ghafla naanza kuhisi jambo kwamba kitatokea hiki na kile eneo husika na mambo ya kawa vile vile yaan kwa jinsi nitakavyohisi inaonesha wazi kwamba nimewahi kufika eneo lile lakini sikumbuki ni lini yaani.

Pia leo nimestuka zaidi maana katika kumbukumbu zangu nimewahi kukutana na hii mada ila sijui ni wapi..

Natumaini tutapata elimu zaidi hapa juu ya swala hili.
 
Kwangu mimi huwa inanitokea hiyo hali mara chache sana naweza pita sehemu au eneo ambalo sijawahi kupita hata siku moja na nikalikumbuka vizuri tu huwa najisemea tu moyoni..... Dah hii sehemu nishawahi kuiota ndotoni hii... Na nadhani ni kweli maana binafsi siamini kama kuna kuishi zaidi ya mara mbili ktk uhai wa binadam
 
Mkuu Humble African this can be true its happen to me some times naenda mahali naona kila kitu nikitu ambacho kilishapita maishani mwangu,hivyo nikweli kuna maisha baada ya kifo!pia humu kuna uzi kama huu na kama sikosei aliuleta Mshana Jr ndiyo maana mchango wake ni mdogo ila sina uhakika ila nakumbuka kitu kama hicho. Ila hiyo story ilienda mbali kwani mleta mada alikutana na wazazi wake USA na alikuwa akiota alipoenda USA akutana nawale wale watu! Tafuta huo uzi uko very interested
 
Kwenye movie ya Matrix ya kwanza Neo anamuona paka sekunde hii, inayofuata anamuona tena akifanya tukio lile lile.

Anaulizwa na Trinity "Vipi?" anajibu "Huyu paka nilishamuona ni kama deja vu" Trinity anamwambia "Ikitokea hivyo maana yake kuna kitu kimekua adjusted tukimbie"
 
Hakuna binadamu anaishi mara 2 ni nafsi ambazo binadamu amejaliwa nazo na ndio zinakupa iyo memory, kwangu ni kwaida hayo kwa kila kitu. Hata ukiwa na shida na mimi tu hata kama hatujawahi kuonana ninaweza kujua unataka kuniambia nini.
 
Hakuna binadamu anaishi mara 2 ni nafsi ambazo binadamu amejaliwa nazo na ndio zinakupa iyo memory, kwangu ni kwaida hayo kwa kila kitu. Hata ukiwa na shida na mimi tu hata kama hatujawahi kuonana ninaweza kujua unataka kuniambia nini.
aisee ustaadh mbona unatupiga kamba kwenye huu mwezi mtukufu. Dah yani bonge la saund na fiksi.

Ramadhan karim
 
Mimi naona ni tofauti, nilikua naweza kukaa nikapata kama picha ya jinsi ntakavokua naishi mbele lakini mostly naona niko na mama pekee mpaka nakumbuka siku hiyo nimekaa najiuliza baba atakua wapi mbona hua simuoni kulikua na sauti ndani yangu ikanambia atakua amekufa nilishtuka na kweli alikuja kufa miaka miwili baadae nikawa najisemea bas nilichokua nakiona ni sahihi nikapgopa na kukataa hiyo hali nilikua nikikaa nikitulia kuna hali flan nazama kwenye fikra tokea nimekataa hiyo hainijii kabisa
 
Pole sana mkuu..wewe una ugonjwa wa akili (psychosis ) wahi ukatibiwe..
Deja vu ni scenario ya kawaida kwa wagonjwa..

Kama unahisi uliwahi kuishi zamani unafikiri zamani hio hoteli ilikuwepo??
Ungesema labda uliona mabanda ya nyasi hapo ningekuelewa lakini kusema uliona hotel ya kisasa kabisa halafu useme ni past life yako huo ni ugonjwa...

Pole sana mkuu na get well soon
 
Acheni kujifariji wakuu, Deja vu ni miongoni mwa dalili za psychomotor seizures....mojawapo ya aina za kifafa(epilepsy) na ikitokea mara kwa mara inawezapelekea psychiatry problems.o_Oo_Oo_Oo_O
 
Ilishawah nitokea hiyo hali mo thn 4 ama 5 times. Niliishuhudia tu mwenyew kila kikitokea nakumbuka hili lishawah kutokea. Ila moja ilikuwa kubwa kuliko nhadi ikapelekea nipate mfedheheko na kujiona labda nina tatizo la kichwa.. Nina rafiki mmoja tu nnae mwamini na kushauriana nae kwenye mambo km haya,nlitoka dsm hadi singida kumtafuta huyo jamaa,nlipomuelezea situation ilonikuta alichonijibu ni kwamba HATA YEYE HUWA INAMTOKEA KABISA na alipoonana na watu flani wakamwambia ni MASWALA YA SPIRITUAL TUU.hii hali ipo. Nashukuru mungu kumbe huwatokea wengi tuu
 
Hivi unamuelewa huyu jamaa kweli?
Achana nae " huyo Anataka kutuhatibia Uzi ""....Uzi mzuri tu huu".....ijapokuwa sijatoa ushuhuda wangu"",....lakini " ukisoma comments za wachangiaji...Ambao ndio wengi " waliokili" kuwa huwa "" wanafikwa " na hiyo hali"....basi" Niseme Moja kwa Moja kuwa Hiyo hali ""...huwa inawafika watu ""......kikubwa zaidi "" nikwamba " binaadamu "" anapolala"" roho Yake huwa "" huwa inaendelea"" kuzurula "" huku na huko".....so huwa inaweza kufika mahala popote "" pale " "inapotaka....so wakati roho " inapotembea "" sis kama binaadamu "" huwa tunayaona "" Yale matembezi "" kwa kupitia Ndoto""...."" Hii hali pia ...huwa inapelekea "" ujio wa hiyo de javu ...''...Maana kwa kuwa roho Yako huwa inatembea "".... ipo siku nawewe wawezs kuzuru "..katika maeneo ambayo "" roho yko "" ili shawahi kuzuru kabla...."" kisha ubongo" huwa unakurejeshea " kumbu kumbu "" ya ile ndoto yko ""........MAISHA HAYA
 
Hii hali humpitia mtu kwa muda mfupi sana,huwa haikai.

Umekaa sehemu,ghafla unajihisi uliwahi kukaa hapo katika hali hiyo hiyo uliyokaa kwa muda huo,hadi mavazi na aina ya ukaaji.

Unaongea na wenzako,ghafla unakumbuka uliwahi kuongea nao katika hali hiyohiyo na katika mazingira hayohayo.

Tatizo linakuja unapoanza kuvuta kumbukumbu ni lini,haukumbuki kamwe.
 
Mimi naona ni tofauti, nilikua naweza kukaa nikapata kama picha ya jinsi ntakavokua naishi mbele lakini mostly naona niko na mama pekee mpaka nakumbuka siku hiyo nimekaa najiuliza baba atakua wapi mbona hua simuoni kulikua na sauti ndani yangu ikanambia atakua amekufa nilishtuka na kweli alikuja kufa miaka miwili baadae nikawa najisemea bas nilichokua nakiona ni sahihi nikapgopa na kukataa hiyo hali nilikua nikikaa nikitulia kuna hali flan nazama kwenye fikra tokea nimekataa hiyo hainijii kabisa
Ulikataaje madam?
 
Back
Top Bottom