Shahada ya kwanza inatosha, Watanzania tusipoteze muda kusoma zaidi

Elimu inayokwambia Mwanadamu alitokana na Nyani sindo hiyo hiyo inaendambali hadi degree? Mimi sijabahatika kusoma sana ila nilifundishwa hvyo maybe nikuulize na kina Daniel walifundishwa hvyo kumkana Mungu?

Hapo ndio unapochanganya mambo sasa. Hapa tunajadili hii hii elimu ya aeiou na hesabu za 123456....huo mjadala wa theology tunaweza kuuanzishia uzi mwingine.

Nnachokushauri, usitazame kila kitu katika mtazamo wa aina moja.
 
Tatizo hatutumii elimu zetu, zaidi sana tunatumia vyeti. Kwa mantiki hiyo unaweza kuwa na PhD lakini huna la maana unaloweza kufanya.

Angalia tu saivi, PHD holders wengi wamejiingiza kwenye siasa, badala ya kujikita kwenye tafiti za kisayansi na uvumbuzi, wao wanapiga domo katika siasa.

Kwa Tanzania elimu ya darasani inasaidia kuongeza makabrasha ya vyeti, sio uwezo kifikra.
Watu wengi humu wanashindwa kutofautisha mbio za vyeti na kuelimika.. Hata ukiwa na mtt mkazanie akaelimike..asiweke effort kwenye grades tu.. Ukiona mtt anakazana na gardes ukimuuliza swali kwa mfumo au lugha tofauti hawezi ujue hakuna elimu hapo..

Taasisi za elimu..ikiwemo familia..zinakujengea uwezo wa kutafsiri taarifa(facts) kusuit your daily needs.. Kama haifanyi hivyo basi ujue hakuna kuelimika hapo.

Watanzania wengi tunakimbizana na vyeti.. Yaani tunatafuta kujiaminisha uelewa wetu kwa kipande cha karatasi (certificate) elimu ni practice ya knowledge kama huwezi unachojua ni nadharia tu hakuna kitu hapo.

Pia kwa taifa tunahitaji managers , researchers and technicians... Kila mti anataka degree nani afanye?! Hz degree za nit engine inawapa kazo mpaka wakutane na vijana wa uswahilini ambao pia wamepata elimu kivyao..ila wao wameitfasiri kwa vitendo since day 1 ndio maana japo wanajua kidogo bado wanaweza kuitumia yote.

Lakini pia ukiacha hayo..lazima kuwe na kikomo cha kutafuta hiyo elimu Mpya uanze kuitumia ulikwisha kuipata... Huwezi ukaendelea tu kutafuta elimu kila siku.. Sema inatosha haya maarifa niliyopata yanapaswa kutumika sasa .ili ufanye kitu. Sasa wewe unatafutaga tu elimu ...unadhani waliotumia ceteris paribus walikuwa wajinga.. Lazima ifike kipindi ukonclude... Uache kupekenyua.
 
Hapo ndio unapochanganya mambo sasa. Hapa tunajadili hii hii elimu ya aeiou na hesabu za 123456....huo mjadala wa theology tunaweza kuuanzishia uzi mwingine.

Nnachokushauri, usitazame kila kitu katika mtazamo wa aina moja.
Kwani ndg kilichokuwa kinazungumziwa si Elimu na mafanikio ama mi sikuelewa vzri?
 
Mkuu kwenye hizi technolojia kubwa unazoziona kwenye nyanja mbalimbali, mfano. kwenye tiba, vyombo vya usafiri kama ndege, na vitu kama simu ya kisasa unayotumia kuna PhD za watu zimelala humo. Kwa hiyo kadri unavyoendelea kufurahia maendeleo hayo ya kiteknolojia, jua kuna watu wamesugua vichwa barabara.
 
Kwani ndg kilichokuwa kinazungumziwa si Elimu na mafanikio ama mi sikuelewa vzri?

Ndio hicho na hasa kiwango cha elimu. Hapo ndio ulipokuja na kusema hii elimu ni upuuzi kwa mujibu wa Biblia. Nikakukumbusha mbona Biblia inasema mshike sana Elimu usimuache aende zake?
Ukasema inapinga uwepo wa Mungu. Hapo ndio nikaona tutaharibu mada na lengo la mleta uzi.

Tujikite kwenye hoja, mafanikio na kiwango cha elimu. Na Je vina uhusiano na utajiri?
 
Kosa kubwa lilifanyika watu kudhani kusoma sana ni sawa na kuwa na hela sana.
Elimu ni muhimu lakini huko ilikoanzia haikuwa na msisitizo wa kumfanya aliyesoma kuwa tajiri.
 
Ndio hicho na hasa kiwango cha elimu. Hapo ndio ulipokuja na kusema hii elimu ni upuuzi kwa mujibu wa Biblia. Nikakukumbusha mbona Biblia inasema mshike sana Elimu usimuache aende zake?
Ukasema inapinga uwepo wa Mungu. Hapo ndio nikaona tutaharibu mada na lengo la mleta uzi.

Tujikite kwenye hoja, mafanikio na kiwango cha elimu. Na Je vina uhusiano na utajiri?
1wakorinto 1-20 Yu wapi mwenye hekima?
Yu wap mwandish?
Yu wapi mleta hoja wa zamani hizi?
Je! Mungu hakuifanya hekima ya Dunia kuwa ni upumbavu? 21 Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waminio kwa upuuzi wa lile neno linalohubiriwa. Rafiki tusaidiane hapa nini Mungu alimanisha?
 
Mkuu, hauwezi hata kutofautisha hekima na Elimu? Hekima haiji kwa kwenda shule. Unaweza kusoma na usiwe nayo, hali kadhalika sio ajabu kumkuta asiyesoma ana hekima.

Kwenye vifungu ulivyoleta sijaona elimu ikisemwa ina tatizo wala upuuzi
 
Watu humu mnasema wengine wafanye biashara kwamba elimu hailipi na blah blah nyinginezo...nyinyi hizo biashara zinazowalipa mbona hatuzioni??? Mbona mnashinda kwenye JF na threads za kulalamika tuu? Sasa tofauti ni ipi? wasomi wanalalamika ajira hakuna...na wafanya biashara wanalalamika biashara ngumu sijui kodi kubwa..sasa unafuu uko wapi?? Sawa the so called wasomi wengi walikuwa na vyeti fake..Lakini hata wafanya biashara wengi walikwepa kodi..matokeo yake wengi wamefunga biashara! Hatuchekani!

Mimi nadhani kila mtu afanye anachoona kinamfaa tusipangiane maisha!
Nikisoma mawazo ya watu hapa wanasema elimu haina maana, Tanzania bila elimu inawezekana! Dah unaona kabisa Afrika tuna safari ndefu sana... Watu hawajajua point kuu ya elimu ni ipi, eti ni kujipatia fedha!
Point ya elimu ni kumuwezesha binadamu kuelewa mazingira na ulimwengu vizuri,kisha kutengeneza mifumo mizuri itakayomuwezesha kuishi maisha bora, kuanzia kwenye matibabu, mawasiliano, uzalishaji chakula, utawala na mengine kibao... Mtu anasema eti Bakresa na wengine hawajasoma na ni matajiri hivyo etio kusoma hakuna umuhimu...hOpeless kabisa!
Bakressa ana wakemia, wahasibu na wachumi na wasomi wengine ambao ndio uti wa mgongo wa kampuni zake... Sasa kama wabongo hawataki kusoma aki import wahindi kutoka nje watamlaumu?????
 
Wakenya wamejazana nafasi za juu huku sie tunatolea mfano Bakhresa hajasoma na ni tajiri, au mtu anajwambia sijui Bil Gates hakusoma na ni tajiri.

Hao wote wameajiri wasomi na wataalam wa hali ya juu.
 
Mkuu, hauwezi hata kutofautisha hekima na Elimu? Hekima haiji kwa kwenda shule. Unaweza kusoma na usiwe nayo, hali kadhalika sio ajabu kumkuta asiyesoma ana hekima.

Kwenye vifungu ulivyoleta sijaona elimu ikisemwa ina tatizo wala upuuzi
Tatizo lako kaka unachukua neno moja tu na kulitolea ufafanuzi, je anapozungumzia Mwandish? Pia kwa Dunia yaleo ili uwe na Hekima usome kwa leo hakuna mchungungaji alie chini ya 4m4! Naomba unipe tafsir ya Mungu alichokisema hapo kma sivyo bas kubaliana na mimi.
 
Inaonekana tunaongelea vitu viwili tofauti. Napinga na ntaendelea kupinga kwamba Biblia inaita Elimu upuuzi. Kama hilo ni tatizo basi nna tatizo.
 
Pesa ni kipimo cha maarifa,
Unapesa unamaarfa huna pesa huna maarifa, kias cha pesa unazomiliki au kipato chako ni sawa na maarifa ulionayo!
Elimu huongeza maarifa hivyo ni siri mojawapo ya utajiri
Kusoma sana jambo ambalo hutalitumia kukuletea pesa ni kupoteza mda wako
 
Back
Top Bottom