Shahada ya kwanza inatosha, Watanzania tusipoteze muda kusoma zaidi

Mimi ninadhani wenye uwezo mkubwa waendelezwe tena kwa pesa ya kodi zetu.
Tunahitaji academicians, scientists, researchers
Disemei wale wakulazimisha elimu la hasha wale wanaopata PhD at 40+, wale wajisomeshe wenyewe kama wanataka.

Ninasemes wale wanaopata Masters wakiwa 26-28 hata wakuvuta PhD wako chini ya 35 na wakiitumia elimu Yao hata kodi ilyowasomesha inarudi.
Haya ndiyo mawazo ya kiutu uzima! Mleta mada na wanaomkubali ni failure katika elimu wanajaribu kujiconsole tu.
 
Mambo mengine kama huyafahamu ni vizuri ukakaa kimya. Mtu unasema vitu ambavyo vinakuonyesha kabisa ulivyomfinya wa uelewo. Lengo la elimu sio kupata fedha pekee na wala sio kupata kazi ya kuajiriwa tu. Elimu kubwa, ubobezi na maarifa makubwa zaidi. Na maana hii ndio unapata wataramu wakubwa wanaoweza kukusaidia wewe kwa njia moja ama nyingine. Ndio elimu inayoweza kuzalisha walimu wa kukufundisha wewe hiyo degree unayoisema. Ndio utaramu unaofanya utafiti wa theories, principles na laws za maumbile ya asili ya dunia. Tatizo ulilonalo wewe unadhani watu wanasoma ili wapate pesa tu. Elimu ni zaidi ya hilo.
 
Uzi wako ni mzuri ila ulipokosea ni hapo mwisho kwamba "tusipoteze muda kusoma zaidi".
 
Enzi ya mwalimu elimu ilikua ndo kila kitu,ila kwa nyakati hizi pesa ndo elimu yenyewe kiwango cha juu cha pesa ndo degree yenyewe, wapo watu wanahitimu chuo cha usimami wa fedha tena masters lakina yupo kama fala Fulani ivi tunawatuma tu kitaa hata mia hana A/C zenyewe ni za urembo.namaliza kwa kusema ivi ELIMU NI KUWA NA PESA,
 
Elimu ina faida na manufaa sana endapo itamuongezea mhusika upeo, uwezo wa kuchambua mambo, maarifa na namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali.

Tatizo ni pale wanaoitafuta wanapoweka juhudi kwenye kupata cheti badala ya maarifa au kuelimika. Hapo ndio tofauti ya darasa la saba na PhD inapokosekana.
Mkuu nimekuelewa vizuri sana,umeelezea vizuri sana Kaka.
 
Ndg mimi nasoma Gombo sio biblia elimu ya Mungu tu ingetosha sana kutufanya kuwa mabwana wa maisha, lkn hii elimu ambayo ni Upuuzi inawafanya watu kuwa wa binafsi na kuwa watumwa wa maisha! Upendo hakuna imebaki kila mmoja kupambana na hali yake. Kma ningekua Muda wa kutosha ni kufunulia vitabu vya historia pale wanadamu alipoanza kuchanganya mambo ya Mungu na maarifa yao.View attachment 721870

Una habari akina Daniel, Musa na Paulo walikuwa wameelimika? Nimekuuliza jambo moja tu. Ni elimu ya aina gani inaitwa upuuzi? Bila elimu hata Biblia unafikiri ingeandikwa. Kusoma Gombo au chochote sio tija. Weka hoja mkuu.
 
Acha ufu wa akili. Lengo la elimu sio kupata hela na utajiri unaoutamani na utajiri wenyewe sifahamu kama unao. Lengo la elimu ni kutoa maarifa ya kila nyanja ya maisha. Bila elimu usingejua umuhimu wa kunawa mikono ukitoka uani. Acha kuleta mada za aibu aibu hapa.
 
Tatizo hatutumii elimu zetu, zaidi sana tunatumia vyeti. Kwa mantiki hiyo unaweza kuwa na PhD lakini huna la maana unaloweza kufanya.

Angalia tu saivi, PHD holders wengi wamejiingiza kwenye siasa, badala ya kujikita kwenye tafiti za kisayansi na uvumbuzi, wao wanapiga domo katika siasa.

Kwa Tanzania elimu ya darasani inasaidia kuongeza makabrasha ya vyeti, sio uwezo kifikra.
 
Ukishindwa kupata hela na kuendesha maisha /familia yako vizuri kwa degree yako moja basi elewa kwamba hata ukiwa na Masters /PhD maisha yatakusumbua sana. Na ukija kupata vijihela basi vitakuja too late ukiwa na miaka zaidi ya 50!

Wengi wenye pesa na maisha mazuri wana degree 1 kushuka chini mpaka primary education.

Na wengi ambao hupenda kusomasoma sana huwa wanaishia kuwa na stress /msongo wa mawazo na huishia maskini na kuanza kuiponda Serikali kwa kila kitu ambacho inafanya!

Angalia tu wadada /wazee /vijana wengi wa Kitanzania wanaofanya International trade na wenye kampuni ama biashara zilizokaa njema wengi wana Certificate /Diploma /one degree ama elimu isiyo maalum (elimu dunia)!

Tutumie elimu ndogo tulizonazo kutatua changamoto za kimaisha mapema!
Primitive thinking, typically Tanzanian mentality! Mmekakariri kuwa lengo la kusoma kusoma ni kupata kazi, hence fedha! Jaribu kutoka nje ya hilo box lenye ugoro uliojifungia! Elimu iko ili imwezeshe binadamu kupambana na mazingira yake na haina mwisho. Tunahitaji mabingwa kwenye kila area na fani. Tunahitaji ugunduzi mpya kila fani. Haya hayawezi kutokea bila watu kufanya research na kusoma! Afrika ina watu wengi kama wewe na ndio maana hatugundui chochote wala kuendelea mbele. Tumebaki kuokoteza vya wenzetu tu. Ptu! Mawazo yako yananuka.
 
Unatoa mifano ya akina Barkharesa, kama Barkharesa wako wangapi katika nchi? Education is for lebaration mentally and physically, not only to make you rich.
 
Mimi ninadhani wenye uwezo mkubwa waendelezwe tena kwa pesa ya kodi zetu.
Tunahitaji academicians, scientists, researchers
Sisemei i wale wakulazimisha elimu la hasha wale wanaopata PhD at 40+, wale wajisomeshe wenyewe kama wanataka.

Ninasemes wale wanaopata Masters wakiwa 26-28 hata wakivuta PhD wako chini ya 35 na wakiitumia elimu Yao hata kodi ilyowasomesha inarudi.
Sky Eclat elimu haina mwisho hence elimu haina umri! Jaribu kutembea duniani utabadilisha mawazo yako kwani naona kama unataka kutulisha mentality za kitanzania.
 
Elimu ya kibongo kusoma kindakindaki mwisho form 6.
Chuo ni madesa na viguruneti kwenda mbele mpaka unamaliza miaka mitatu na kijentromeni chako.

Unaingia mtaani kuuza juisi ya miwa ama kufungua goli la mtumba maana kufukuzia kazi unaweza poteza muda ambao ungeweza kumaliza degree ya masters bila mafanikio.
Kwa wale wenye akili za ziada wamekimbilia mashambani kulima vitunguu na matikiti.

Hii ndio bongo, sio marekani huko havard mtu kabla ya kumaliza degree kashakuwa na akili za kujitengenezea ubilionea.
 
Mimi najionea mtoa mada yupo sahihi. Kwa mana mimi nimeona matajiri wengi nibwafanya biashara hao wanaokuwa na elimu lazima wawe waajiriwa na mwisho wake wanaishia stress tu. Ila hata wamachinga wanauwezo wa kujikwamua kwa kiwango kikubwa sana kimaisha kushinda mwenye degree. Mimi ni mmoja wapo. Tanzania Bila elimu inawezekana kwa mana hata hao wenye elimu nyingi sanaa na standard wanafundisha tu twishen mtaani. Ambayo kila ada ya mtoto ni buku 5 kwa week.. Sasa ungelijuwa kuwa umesoma mtaji na ajira hakuna ni kheri ungefanya biashara tu.

Watu humu mnasema wengine wafanye biashara kwamba elimu hailipi na blah blah nyinginezo...nyinyi hizo biashara zinazowalipa mbona hatuzioni??? Mbona mnashinda kwenye JF na threads za kulalamika tuu? Sasa tofauti ni ipi? wasomi wanalalamika ajira hakuna...na wafanya biashara wanalalamika biashara ngumu sijui kodi kubwa..sasa unafuu uko wapi?? Sawa the so called wasomi wengi walikuwa na vyeti fake..Lakini hata wafanya biashara wengi walikwepa kodi..matokeo yake wengi wamefunga biashara! Hatuchekani!

Mimi nadhani kila mtu afanye anachoona kinamfaa tusipangiane maisha!
 
Una habari akina Daniel, Musa na Paulo walikuwa wameelimika? Nimekuuliza jambo moja tu. Ni elimu ya aina gani inaitwa upuuzi? Bila elimu hata Biblia unafikiri ingeandikwa. Kusoma Gombo au chochote sio tija. Weka hoja mkuu.
Elimu inayokwambia Mwanadamu alitokana na Nyani sindo hiyo hiyo inaendambali hadi degree? Mimi sijabahatika kusoma sana ila nilifundishwa hvyo maybe nikuulize na kina Daniel walifundishwa hvyo kumkana Mungu?
 
Hivi tuache kusoma kwa sababu kwenye elimu hakuna hela? Ee, si tunasoma tupate utajiri. Sasa bila elimu kubwa ya maarifa makubwa nani Angekutengenezea hiyo simu unayoitumia? Hiyo cm unayoitumia inamifumo mingi ambayo baadhi ya technoloji zake zilipatikana kwa maarifa makubwa ya elimu. Kama vitu hujui Kaa kimya endelea kula magimbi na bibi yako.
 
Back
Top Bottom