DED wa Kyerwa ni tatizo kwa Watumishi

LAPSE RATE

Member
Oct 18, 2015
59
76
Wapendwa habari za muda huu?

Nimeona niandike uzi huu nikiwa na masikitiko kuhusu huyu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera aitwaye Shedrack Mhagama.

Huyu mheshimiwa amekuwa ni tatizo kwa watumishi wanaofanya kazi katika Halmashauri yake ambayo siyo kongwe sana.

Amehusika pakubwa sana kutenganisha ndoa za watumishi hasa kada ya walimu kwani amekuwa Munhu mtu, hataki kusikia mtumishi akimwambia anaomba uhamisho kwenda karibu na mwenza wake au kusogelea wazazi wake.

Watu wametoa machozi mbele yake lkn yy amekuwa akiwaambia hata walie kiasi gani hajali kwakuwa alipata cheo hicho kwa kukataa kuruhusu watu kuhama alipokuwa akifanya kazi kabla. Suala la kujiuliza ni je, kuhama ni mapenzi ya DED au ni haki ya mtumishi kwa mujibu wa vigezo vya sheria za utumishi wa umma?

Pia huyu Mkurugenzi hawajibiki vyema kwani watumishi wa Kyerwa wamekuwa hawapandi madaraja kwa mda mrefu kulinganisha na Halmashauri nyingine Kyerwa inakuwa the "worst ever" district council.

Inafahamika kuwa kwa muda mrefu watumishi hawajapanda vyeo nchi nzima ila kwa Kyerwa ni zaidi ya maeneo mengine. Unakuta hadi mtumishi aliyeajiriwa tangu 2012, 2013 bado hajawahi kupanda achilia mbali wa 2014, 2015, na kuendelea. Huu ni uzembe mkubwa unaoongozwa na huyu bwana sijui ni kwakuwa analindwa na ndugu zake.

Niombe mamlaka husika ziangalie kwa karibu madudu ya huyu bwana maana amekuwa kero kwa watumishi wake.
 
Lalamiko lake ni la kiutawala zaidi. Akiwasilisha huko litafanyiwa kazi hakuna shaka yoyote.
 
Back
Top Bottom