DED sitamani kuona wananchi wakilalamikia miradi

JAMHURI

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
449
60
Kiteto iliyopo Mkoani Manyara, imekuwa na mabadiliko makubwa na kwa haraka kwa miaka miwili na nusu, kutokana na aina ya uongozi uliopo.

Hili limeshuhudiwa na wananchi wenyewe na wakati mwingine wanediriki kuyasema hayo mabadiliko.

Kwa miaka mitano iliyopita, Kiteto ilizungumzwa vibaya, kwa kuitwa majina ya kila aina kutokana na yaliyokuwa yanajitokeza.

Kiteto iliitwa Cossovo, Darful, Somalia ni kutokana na mgogoro uliokuwa umeibuka kati ya wakulima na wafugaji.

Katika mgogoro huo watu walijeruhiana na hata kuuana wakigombea ardhi jambo ambalo lilisababisha maendeleo kusimama.

Viongozi mbalimbali waliofika akiwemo aliyekuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Simon Sirro aliyekuwa kitengo cha Opetesheni za Polisi ambaye kwa sasa ni IGP Tanzaniana wengine wengine wengi.

Pamoja na mambo mengine Suluhu ya matatizo haya ilitokana na kubadilishwa kwa viongozi mbalimbali karibia ngazo zote.

Kwa sasa viongozi waliopo wanafanya kazi za maendekeo tofauti na awali ambao walifikiri kutatua mgogoro kuliko maendeleo ya wananchi.

Katika kipindi cha miaka miwili na nusu sasa Kiteto inazungumzwa yenye maendeleo kwani kila ufikapo kwa wananchi badala ya kuzungumzia migogoro sasa wanazungumzia Shule, Maji, na hata Afya.

Ukifika Kara ya Sunya utaelezwa Habari ya ujenzi wa Kituo cha Afya kilichoboreshwa kwa 400 mil, Matui Ujenzi na wa utanuzi wa Kituo cha Afya umeanza.

Kumeanzishwa Sekondari mbili za A leval Kiteto na Engusero kwa pamoja, limejengwa jengo la Halm la 4.3 bil.

Soko la Wilaya lililokuwa limepata ajali ya kuungua limeezekwa, mitaro ya maji katika barabarani za miji inaendelea tena kwa kiwango cha hali ya juu.

Hospitali ya Kiteto imezungushiwa uzio (ukuta), na kuchimbwa kisima cha maji ujenzi wa tanki Duka la dawa ndani ya Hosp.

Ujenzi wa madarasa katika shuke za msingi na Sekondari, haya yote kwa pamoja yametajwa kuzungumzwa na wananchi wenyewe wa Kiteto.

Visima vya maji zaidi ya 12 kwa wakati mmoja vimechimbwa ili kuondoa adha ya maji, kani awali Wilaya ilikuwana na uqezo wa kujimudi kwa 36% tu kuhudumia wananchi wake, viko katika ujenzi wa miundombinu

Hili kwa muungwana yoyote ni jambo jema niseme tu lililobaki ni kwa wananchi wenyewe kuendekea kutoa ushirikiano kwa viongozi wao

Na pia kulinda miradi hiyo iwe endekevu, hii italeta tija kubwa kwa wananchi katika ustawi wa maendeleo yao.

Itaendelea..
 
Attachments

  • FB_IMG_1534449107680.jpg
    FB_IMG_1534449107680.jpg
    55.3 KB · Views: 27
Viongozi waendelee kutimiza majukumu yao. Kama vituo vya afya, visima, jengo la halmashauri na soko vimewasahaulisha ugomvi wanakiteto basi juhudi zaidi ziongezwe.
 
Viongozi wakubwa ndiyo ilikuwa Chanzo cha matatizo, Kumiliki Ardhi Kubwa uko kiteto, ikapelekea wafugaji kukosa malisho ya mifugo yao. wengi Ardhi wamenyang'anywa,
 
Viongozi waendelee kutimiza majukumu yao. Kama vituo vya afya, visima, jengo la halmashauri na soko vimewasahaulisha ugomvi wanakiteto basi juhudi zaidi ziongezwe.
Aa wapi!
Ile ya kuwahamisha,kubomoa makazi,kuwasambaratisha na kuwafukarisha wakazi wa KISIMA na kuwabwaga PORI-KWA-PORI ni maamuzi ya haohao viongozi.
KISIMA ipo kata ya AMEI.Matumizi ya ardhi ni sehemu ya KILIMO. Tayari watu walikuwa wamejipanga kujenga shule.
PORI-KWA-PORI ipo Kata ya KIMANA--takribani kilomita 15 magharibi.
Watu watoke P.k.P waingie maporini kulima na hakuna ulinzi!
Ndiyo useme 'hali ni shwari'
DECISION MAKING IS AN ART.
 
Back
Top Bottom