DED Monduli na TANESCO wamedhulumu taasisi za dini fidia ya ardhi

MWIBAPORI

Member
Feb 10, 2017
60
35
Hii imetokea katia kijiji cha Makuyuni tangu 2017 hadi leo ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Monduli amedhulumu taasisi za dini ya kiislam na kikristo na baadhi ya wananchi fidia ya ardhi yao baada ya TANESCO kupitisha umeme wa kilovolti 400 katika maeneo yao.

Makuyuni ni kijiji lakini ili DED huyu achukue hela za wananchi yeye na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha Kimanta walisema kijiji cha Makuyuni ni eneo la Halmashauri hivyo hiyo fidia anaichukua yeye.

Rais wetu tusaidie maana huu ni wizi na dhuluma kubwa ambayo wananchi wamefanyiwa.

Juhudi za kumwona na kuongea naye hazijazaa matunda na amekuwa akiwazungusha wananchi kwa kushirikiana na TANESCO Arusha na Afisa mipango miji wa manispaa ya Arusha aitwaye Deo.

DED anatumia mabavu na uvunjifu mkubwa wa sheria maana hana nyaraka zozote za kiserikali zinazoonyesha kama Makuyuni ni mji au mji mdogo kwani bado ni kijiji chenye vitongoji na siyo mitaa. Pia kijiji cha Makuyuni kinaongozwa na mwenyekiti wa kijiji pamoja na Mtendaji wa kijiji.

Na pia Rais wetu kipenzi tunakuomba sana utakapochagua wakurugenzi wa Halmashauri utuondolee huyu DED pale Monduli kwani amesababissha mateso makubwa kwa wananchi.

Zipo kesi zilizopelekwa mahakama kuu ambapo DED alishindwa na hakuweza kukata rufaa lakini bado anashindana na mahakama ili wahusika wasilipwe fidia kwa kuwarubuni TANESCO pamoja na afisa mipango miji wa Arusha.

Tunawasilisha kwa mara nyingine ombi letu kwako mh. rais ili utasaidie tupate haki yetu.
 
Tunamshukuru Mh Rais mama yetu kwa kumstaafisha Iddi Kimanta maana huu uovu waliufanya na huyu DED wakati huo Idd Kimanta alikuwa DC wa wilaya ya Monduli. Huyu DED ana kiburi sana kwa sababu ni kada wa chama
 
Hata hivyo siamini kama kuwa kada wa CCM ndicho kibali cha kuvunja sheria na kuwadhulumu wananchi uliopewa kuwaongoza
 
Wakati fidia ya maeneo ya wananchi waliopitiwa na umeme wa KV 400 inatangazwa na TANESCO mwaka 2017 huyu DED na wenzake pale wilayani akiwemo IDD KIMANTA walipanga mkusudi kuwadhulumu fidia wananchi waliokuwa wanamiliki kihalali maeneo yaliyokuwa yapitiwe na umeme.
Walitengeneza mazingira wakaanza kuwaambia wananchi wako eneo la ranchi, mara ushoroba mara ni eneo la halmashauri nk. Alipoona imeshindikana akawarubuni TANESCO ili wasitoe fidia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom