DED, DC wampuuza Rais Magufuli; wafanya sherehe za kupongezana kinyume na agizo la rais

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
MARRY Tesha, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mwanza na Housian Kusiga, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la hilo wamekiuka agizo la Rais John Magufuli la kufanyika kwa sherehe za kupongezana pindi mtumishi wa umma anapoteuliwa kushika nyadhifa, anaandika Moses Mseti.

Machi mwaka huu, Rais Magufuli akiwaapisha wakuu wa mikoa jijini Dar e Salaam, aliwataka kutosherehekea kuteuliwa kwao na kwamba, wafanye hivyo siku wakitimuliwa.

Rais Magufuli pia aliwaagiza wakuu hao wa mikoa kuwekeza nguvu zao katika kuondoa tatizo sugu la madawati kwenye shule za umma, agizo ambalo muda wake ulikamilika Juni 30 mwaka huu huku Mkoa wa Mwanza ukikwama kufikia malengo hayo.

Sherehe za kumkaribisha mkuu huyo wa Wilaya ya Nyamagana na kumuaga aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Baraka Konisaga maarufu mtumishi wa Mungu, ziliandaliwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza chini ya kaimu mkurugenzi huyo.

Sherehe hizo zilizofanyika katika Hoteli ya New Mwanza ambapo zaidi ya watu 100 wakiwemo watumishi wa Jiji la Mwanza wakihudhuria ambapo kiasi cha zaidi ya Sh. 30 milioni zikitajwa kutumika.

Sherehe hizo zilizoanza saa 12 jioni hadi saa 4 usiku, waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari walitimliwa na kutakiwa kutoripoti habari hii.

Awali, waandishi walialikwa na baadhi ya viongozi hao wakiwemo wakuu wa wilaya kwa ajili ya kuripoti lakini baadaye ikaibuliwa hoja ya kwamba, inaweza kusababisha tatizo hasa kutokana na kutokamilika kwa fedha za ununuzi wa madawati.

Hosian Kusiga, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji hilo alipotafutwa kuzungumzia suala hilo amesema kuwa, fedha zilizotumika kuandaa sherehe hiyo hazikutoka katika mfuko wa serikali na kwamba, walichangishana baadhi ya watumishi wa jiji na taasisi mbalimbali.

“Wewe kama ulivyoona mwenye katika sherehe hiyo yalikuwepo makundi mbalimbali, ikiwemo Mwauwasa (Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira) mkoani Mwanza na sio fedha kutoka Jiji,” amesema Kusiga ambaye pia ni Ofisa Mipango wa Jiji.

Tesha, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana akizungumzia suala hilo amesema kuwa, fedha zilizotumika katika sherehe hiyo sio fedha za serikali.

“Pesa zilizotumika sio za serikali, unaniuliza fedha zilizochangwa eti kwanini hazijapelekwa kwenye madawati, mimi ningewakataza wasifanye sherehe, hivi wewe vipii… mbona sikuelewi,” amesema.
 
Unapenda sana habar za uchonganish sijui lengo lako huwa nini hasa? Na mnako elekea mtataka had fedha za harusi, send off ,kitchen party na ubatizo + kipaimara zikatengeneze madawati!! Achen tabia na mawazo za kikolon kiasi hicho uchumi wa nchi haujengwi kwa mawazo ya aina hii.
 
waandishi jaribuni kujikita katika habari zenye kuleta maendeleo na tija ja kwa jamii! Hizi habari ni mambo binafsi zaidi!

kimsingi Magufuli hakuwakataza sherehe, ila aliwashauri wasizifanye sherehe maana anytime mtu anaweza atumbuliwe, basi naafanye sherehe ingine ya kuachishwa!
 
Mkuu tatizo la hawa waandishi wa kibongo ni kununuliwa na kutumika.
 
Mkuu, basi wanunulike na waandike habari zenye tija kwa jamii....wamekalia kuandika fulani vile, fulani hivi...! badala ya kuleta habari za msingi, kuwa issue ipo hivi na inatakikana iwe vile kwa ustawi mzima wa jamii kwa ujumla...!

Wameweka sherehe, hawajaweka sherehe sisi wananchi wa nanjilinji inatusaidia nini?
 
...hawa lazima watatumbuliwa...kama kweli sherehe ilifanyika lazima watumbuliwe....mkuu anajiridhisha kwanza....by the way..huyo anayesema angewezaje kuzuia sherehe lazima waanze nae...maana angetaka angezuia....hizi mil.30 kwanini wasichangie madawati?...haya majipu haya....hawana sense of priority hawa....hata JPM alikataa kufanyiwa sherehe chamani na pesa zikafanya kazi nyingine..
 
MARRY Tesha, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mwanza na Housian Kusiga, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la hilo wamekiuka agizo la Rais John Magufuli la kufanyika kwa sherehe za kupongezana pindi mtumishi wa umma anapoteuliwa kushika nyadhifa, anaandika Moses Mseti.

Machi mwaka huu, Rais Magufuli akiwaapisha wakuu wa mikoa jijini Dar e Salaam, aliwataka kutosherehekea kuteuliwa kwao na kwamba, wafanye hivyo siku wakitimuliwa.

Rais Magufuli pia aliwaagiza wakuu hao wa mikoa kuwekeza nguvu zao katika kuondoa tatizo sugu la madawati kwenye shule za umma, agizo ambalo muda wake ulikamilika Juni 30 mwaka huu huku Mkoa wa Mwanza ukikwama kufikia malengo hayo.

Sherehe za kumkaribisha mkuu huyo wa Wilaya ya Nyamagana na kumuaga aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Baraka Konisaga maarufu mtumishi wa Mungu, ziliandaliwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza chini ya kaimu mkurugenzi huyo.

Sherehe hizo zilizofanyika katika Hoteli ya New Mwanza ambapo zaidi ya watu 100 wakiwemo watumishi wa Jiji la Mwanza wakihudhuria ambapo kiasi cha zaidi ya Sh. 30 milioni zikitajwa kutumika.

Sherehe hizo zilizoanza saa 12 jioni hadi saa 4 usiku, waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari walitimliwa na kutakiwa kutoripoti habari hii.

Awali, waandishi walialikwa na baadhi ya viongozi hao wakiwemo wakuu wa wilaya kwa ajili ya kuripoti lakini baadaye ikaibuliwa hoja ya kwamba, inaweza kusababisha tatizo hasa kutokana na kutokamilika kwa fedha za ununuzi wa madawati.

Hosian Kusiga, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji hilo alipotafutwa kuzungumzia suala hilo amesema kuwa, fedha zilizotumika kuandaa sherehe hiyo hazikutoka katika mfuko wa serikali na kwamba, walichangishana baadhi ya watumishi wa jiji na taasisi mbalimbali.

“Wewe kama ulivyoona mwenye katika sherehe hiyo yalikuwepo makundi mbalimbali, ikiwemo Mwauwasa (Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira) mkoani Mwanza na sio fedha kutoka Jiji,” amesema Kusiga ambaye pia ni Ofisa Mipango wa Jiji.

Tesha, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana akizungumzia suala hilo amesema kuwa, fedha zilizotumika katika sherehe hiyo sio fedha za serikali.

“Pesa zilizotumika sio za serikali, unaniuliza fedha zilizochangwa eti kwanini hazijapelekwa kwenye madawati, mimi ningewakataza wasifanye sherehe, hivi wewe vipii… mbona sikuelewi,” amesema.

Huko ccm hakuna hata mmoja anayeyasimamia maneno yake,yeye mwenyewe alipiga marufuku mikutano na shughuli zote za kisiasa nchini hadi 2020,na policcm wakaanza utekelezaji wa agizo lake kwa kupiga marufuku na kuwatawanya kwa mabomu na maji ya kuwasha wale wote walioonekana kwenda kinyume na agizo la Rais.

Lakini kwa masikitiko makubwa,amejisaliti na kulikana katazo lake na hivi ninavyondika haya,chama chake kipo katika hatua ya mwisho ya kulisaliti agizo la Rais la kuzuia shughuli za kisiasa.Sasa kwa msaada wa policcm,nao wamejisaliti na kuzikana "taarifa zao za kiintelejensia"walizokuwa wanazitumia kuzima shughuli za kisiasa za wapinzani,na leo hii bila aibu,policcm wamesema "hawajawahi kuzuia shughuli za kisiasa isipokuwa walizuia bendera!!!

Kama mkuu wa kaya ameisaliti kauli yake mwenyewe na sasa anajiandaa kuhudhuria shughuli za kisiasa za chama chake,iweje hao walioamua kufuata nyayo zake za kujisaliti na kukana maagizo yake waonekane wasaliti? kwa kufanya sherehe ya kujipongeza?
 
Kuna sherehe za muhimu na nyingine hazina hâta umuhimu, madawati hawajafikia malengo alafu wanatumbua milioni zote hizo eti kupongezana!! Kwani wangeshikana mikono na kuhutubiana huku wakinywa maji wangepungukiwa nini? Hiyo michango wangeonesha mfano kwa kuahirisha starehe ili kuwezesha mambo muhimu,sisi tunajibana ili kununua madawati wasidhani hatujui kusherehekea. It was WRONG,HAIKUWA WAKATI SAHIHI KUSHEREHEKEA KABLA YA VITA VYA KUONDOA AIBU YA WANAFUNZI KUKAA CHINI. Mwandishi yuko sahihi kulieleza hili hatakama hawatoshughulikiwa wajue hatujapenda uchuro wao
 
...hawa lazima watatumbuliwa...kama kweli sherehe ilifanyika lazima watumbuliwe....mkuu anajiridhisha kwanza....by the way..huyo anayesema angewezaje kuzuia sherehe lazima waanze nae...maana angetaka angezuia....hizi mil.30 kwanini wasichangie madawati?...haya majipu haya....hawana sense of priority hawa....hata JPM alikataa kufanyiwa sherehe chamani na pesa zikafanya kazi nyingine..
kweli mkuu nani naona dalili zote za kutumbuliwa hawa wahusika,ajabu wakishatumbuliwa utawaona hawa vijana wa buku saba wanaomshambulia mtoa mada wakija jukwaani kwa mwendokasi kumpongeza Pombe!
 
Marry Tesha, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mwanza na Housian Kusiga, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la hilo wamekiuka agizo la Rais John Magufuli la kufanyika kwa sherehe za kupongezana pindi mtumishi wa umma anapoteuliwa kushika nyadhifa.

Rais Magufuli pia aliwaagiza wakuu hao wa mikoa kuwekeza nguvu zao katika kuondoa tatizo sugu la madawati kwenye shule za umma, agizo ambalo muda wake ulikamilika Juni 30 mwaka huu huku Mkoa wa Mwanza ukikwama kufikia malengo hayo.

Sherehe za kumkaribisha mkuu huyo wa Wilaya ya Nyamagana na kumuaga aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Baraka Konisaga maarufu mtumishi wa Mungu, ziliandaliwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza chini ya kaimu mkurugenzi huyo.

Sherehe hizo zilizofanyika katika Hoteli ya New Mwanza ambapo zaidi ya watu 100 wakiwemo watumishi wa Jiji la Mwanza wakihudhuria ambapo kiasi cha zaidi ya Sh. 30 milioni zikitajwa kutumika.

Sherehe hizo zilizoanza saa 12 jioni hadi saa 4 usiku, waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari walitimliwa na kutakiwa kutoripoti habari hii.

Awali, waandishi walialikwa na baadhi ya viongozi hao wakiwemo wakuu wa wilaya kwa ajili ya kuripoti lakini baadaye ikaibuliwa hoja ya kwamba, inaweza kusababisha tatizo hasa kutokana na kutokamilika kwa fedha za ununuzi wa madawati.

Hosian Kusiga, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji hilo alipotafutwa kuzungumzia suala hilo amesema kuwa, fedha zilizotumika kuandaa sherehe hiyo hazikutoka katika mfuko wa serikali na kwamba, walichangishana baadhi ya watumishi wa jiji na taasisi mbalimbali.

“Wewe kama ulivyoona mwenye katika sherehe hiyo yalikuwepo makundi mbalimbali, ikiwemo Mwauwasa (Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira) mkoani Mwanza na sio fedha kutoka Jiji,” amesema Kusiga ambaye pia ni Ofisa Mipango wa Jiji.

Tesha, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana akizungumzia suala hilo amesema kuwa, fedha zilizotumika katika sherehe hiyo sio fedha za serikali.

“Pesa zilizotumika sio za serikali, unaniuliza fedha zilizochangwa eti kwanini hazijapelekwa kwenye madawati, mimi ningewakataza wasifanye sherehe, hivi wewe vipii… mbona sikuelewi,” amesema.

Chanzo; MwanaHALISI.
 
Back
Top Bottom