DED aliyebainika kuiba fedha za Umma avuliwa madaraka

Mathias Byabato

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,020
691
Jamani hii adhabu kweli inatosha?!



amka2.gif
MKURUGENZI wa Halamshauri ya Wilaya ya Karagwe, Consolatha Kamuhabwa, amevuliwa wadhifa huo na kubaki katika kazi yake ya awali ya kitaaluma na sasa amehamishiwa kituo kingine cha kazi katika ofisi ya mkoa wa Arusha.


Hatua hiyo inakuja baada ya tume iliyokuwa ikiwachunguza wafanyakazi wa halmashauri hiyo, waliokuwa wakikabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na ubadhirifu wa fedha za sekondari, kukamilisha uchunguzi wake.


Akisoma waraka uliotoka katika ofisi ya Waziri ya Mkuu Tamisemi, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Fabian Massawe, katika kikao cha dharula cha Baraza la Madiwani, jana, alisema kuwa mwaka 2010 watumishi 10 wa halmashauri hiyo walikumbwa na kashfa ya kutumia madaraka vibaya na ubadhirifu wa fedha za umma, hivyo tume iliundwa kubaini ukweli huo.


Alisema wakati uchunguzi ukiendelea, iliamriwa kuwa watumishi hao wapumzishwe ili kupisha uchunguzi huku ofisi ya kamanda wa polisi mkoani Kagera nayo ikiagizwa na serikali kufanya uchunguzi pia ili watumishi watakaobainika kuwa na makosa waweze kufikishwa mahakamani.


Kanali Massawe alisema kuwa baada ya uchunguzi wa tume na polisi kukamilika, serikali imemchukulia hatua ambapo Christian, ambaye anadaiwa kuiingizia hasara kwa kuibia halmashauri sh milioni 46 za kutengeneza barabara kwa kushirikiana na mkandarasi na kushiriki katika upotevu wa sh milioni moja za kutengeneza makaravati.


Wengine ni Henerico Batinoluho, ofisa elimu msingi ambaye anakabiliwa na kosa la kumdanganya mwajiri wake kuwa na shahada ya uzamili wakati si kweli na Froliana Buberwa, ofisa tabibu katika kituo cha afya Mulongo anayekabiliwa na kosa la kumwibia mwajiri chakula cha wagonjwa chenye thamani ya sh laki moja.


Aliwataja wengine kuwa ni Mwalimu Fransisca Ishengoma wa Shule ya Msingi Kitengule anayekabiliwa na kosa la kumwibia mwajiri na kumsababishia hasara ya sh milioni 3.2 na Metson Bartazal aliyekuwa mtunza stoo.


Katika orodha hiyo pia yuko Nkwenda anayekabiliwa na kosa la kumwibia mwajiri na kumsababishia hasara ya sh laki nne kwa kutoa chakula pungufu kwa wagonjwa ambapo serikali imemwagiza katabu tawala wa mkoa wa Kagera, kuwafikisha watumishi hao watano mahakamani ili wachukuliwe hatu za kisheria.


Wengine ambao wamechukuliwa hatua za kinidhamu ni Kalumuna Nkalage aliyekuwa katibu wa bodi ya utumishi wa halmashauri hiyo, Dk. Thomas Rutachu, ambaye ni mganga mkuu, Dauda Hassan, fundi mkuu na Mkude Mwakiluma aliyekuwa akihusika na
malipo.

CHANZO HAPA



 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli nae juzi jioni walimsweka ndani. Ni ubadhilifu wa mali za umma. Yeye Alikwapua mashine ya maji kwa k ushirikiana na mwenyekiti wa halmashauri wa zamani then akabanwa ikarudi na alivyo **** akamwandikia appreciation letter yule mwizi na hapo RC akapanda mori na kumsweka yeye na mwizi mwenzie. Hawa wote ni manyokaa wa mamvi lakini.
 
Hapo kuna jipya lipi? kama wezi wa EPA wanabembelezwa kurejesha fedha za wizi sembuse huyo DED
 
Kwa Karagwe:
Ushahidi ukipatikana kwamba mhusika alisababisha hasara au wizi wa fedha za umma ni wazi kwamba lazima afunguliwe kesi ya wezi, arudishe fedha husika (off course with discounting rate; PV=(1/1+r).P! Kama kuwa uhakika wa huo wezi hakuna kumwamisha sehemu nyingine kwa sababu ataendeleza tatizo huko!
Kama wamemwamishia sehemu nyingi basi hizo hela zilitumika kwenye kampeni na hawa watu na kafara tu!

Monduli: Wizi huu ni wa siku nyingi na aliyekuwa anawezesha hili ni EL! Sasa baada ya uchaguzi wa 2010, tofauti yake na aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri ya Monduli ulijitokeza baada ya juhudi za EL kushindwa kuzuia nguvu za wananchi hasa wa pale Makuyuni ya kumwangusha dikteta wao (Daudi Pelo) katika uchaguzi mkuu, ambaye ni mwizi aliyetengenezwa na EL mwenyewe kwa mikono yake, tofauti zilijitokeza na hapa EL na Pelo wakawa paka na mbwa koko!
My take in this: EL is the engineer of this problem kwa vile naye alihusika - anawakomoa hawa watu wasiokuwa watiifu kwake, na usitegemee hawasaidie hata kama angekuwa na uwezo ambao nina wasiwasi kwa sasa kutokana na mambo kumzidi yeye mwenyewe!
 
Tungeanza na EPA,richmond,meremeta nk tungeona wapo serious lakini kwa staili hiyo tunaona ni kuwaonea dagaa tu huku mapapa wakiwa mitaani na zaidi ya yote wakiwa wafadhili wa ccm
 
Wakuonewa ataonewa lakini haki itapatikana...Tatizo siasa za kukomoana ndizo zinazoharibu halmashauri nyingi kwa maagizo ya viongozi fulani wa chama....mf ofisa elimu wa msingi yeye aliajiriwa kwa degree na alieleza kua masters yake aliifanyia nje ya nchi na kuonesha documents zote ila transcript tu ndo hajaichukua lakini nae kakumbwa na hilo panga...kwanza alipewa kazi ya uofisa elimu wa msingi kwa degree km iweje masters ambayo hakuiombea ndo wamshtaki nayo na kwanini wasimwambie akafate hicho cheti if that is a case?
 
Back
Top Bottom