DECI Nyingine yaja kivingine, kwa kutumia nembo ya Serikali

Ikwanja

JF-Expert Member
Jul 12, 2011
2,082
581
Wana JF, nimeona tushrikishane hii kitu maana naona imekaa kiutapeli tapeli mno. Hebo someni wenyewe halafu weny taarifa zaidi watujuze.

naweka link na attachment:

www.socialcompany.wen9.com

FINANCIAL SERVICES
Secure Online Application
WALIO MTANDAONI (7)


SOCIAL CREDIT COMPANY ni Taasisi ya kifedha inayohusika na utoaji mikoponafuu na isiyokua na riba kupitia mfuko maalum uitwao Social Credit & Loanskwa dhumuni la kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakubwa nchini Tanzania kwakuwapatia mikopo ya pesa kwa lengo la kumuinua kiuchumi mtanzania na kumleteamaendeleo ili aweze kujikimu kimaisha kwa dhana yakinifu kutaka kutokomezaumasikini.

Taasisi ya Social Credit Company imeanzishwa mwaka 2003 ikiwa kama tawi zawalisilojitegemea nakua kampuni binafsi iliyoingia ubia na Bank ya NBC (National Bank of Commerce) kwa makubaliano yamikataba ya muda. Social Credit Company imemaliza mikataba rasmi na Bank ya NBChivyo imeanza rasmi kujitegemea na kuunda mfuko huu wa Social Credit &Loans.


Social Credit Company imeanza hatua za kutaka kusambaza matawi yake mikoa yotenchini Tanzania ili kila mtanzania aweze kupata huduma za mikopo kwa ukaribu,kwasasa Social Credit Company ina matawi matatu makuu katika mikoa mitatu (3)Dar es salaam, Kigoma na Dodoma ina jumla ya wafanyakazi 45 katika matawi tajwakila mkoa.


MTANZANIA ATAWEZAJE KUPATA MKOPO?

Mikopo inatolewa kwa kila mtanzania bila ya kuwepo na ubaguzi wa aina yoyotehuduma zetu ni stahiki kwa kila mtanzania ambae ni mjasiriamali,mtumishi waserekalini au mfanyakazi wa kampuni binafsi wote wanastahili kujiunga na kuwawashirika wetu na tutawapatia mikopo.


Wakati tukiwa katika maandalizi ya kusambaza matawi yetu katika kipindi hikiinamlazimu mteja wetu ambae anahitaji mkopo kuweza kujiunga kwa kujaza fomu yamaombi ya mkopo na kujiunga kupitia Online katika tovuti hii kwa kujaza fomuyetu na kulipia ada ya ushirika kiasi cha Tshs. 38,500 (elfu thelathini na nanena mia tano) kupitia Mobile Banking Airtel Moneyna M-Pesa. Baada ya mteja kujaza fomu yetu nakulipia ada Tshs. 38,500 fomu yake itapokelewa pamoja na malipo yake baada yahapo maombi yake ya mkopo yataidhinishwa na atapatiwa mkopo wake wa pesa ndaniya masaa 24.

SIFA ZA KUJIUNGA UWE MSHIRIKA UPATE MKOPO

Sifa kuu za mwanachama anaetakiwa kujiunga aweze kupata mkopo nikama zifuatazo:-

(i) UWE MUAMINIFU
(ii) UWE NA AKILI TIMAMU
(iii) UWE NA UMRI KUANZIA MIAKA 18 AU ZAIDI
(iv) UWE MTANZANIA
(v) UWE NA KITAMBULISHO KIMOJA WAPO KATI YA HIVIMPIGA KURA, BANK, CHUO, LESENI YA BIASHARA, LESENI YA GARI au KITAMBULISHO CHAKAZI

KWANINI TUNATOA MIKOPO NAFUU YENYE MASHARTI RAHISI?

Watanzania wengi wanaweza kujiuliza kwanini Social Credit Company inatoa mikopokwa watanzania yenye masharti rahisi sana tofauti na asasi zingine walizozizoeakama bank na nyinginezo!? Sababu kuu ya kuweka masharti rahisi ni kutakakumsaidia kila mtanzania kuweza kupata mikopo bila kumuwekea vikwazo vigumuambavyo vitakatisha ndoto zake na kumfanya awe dhaifu katika maendeleo yake kwakukosa mkopo kutokana na vigezo vyetu kua vigumu ikiwa dhamira yetu kuu nikutaka kumsaidia kila mtanzania hivyo hakuna sababu yakuweka ugumu waupatikanaji wa mikopo.

KWANINI TUNATOA MIKOPO ISIYOKU NA RIBA?

Mikopo hii haina riba kutokana na faida kuu mbili tuzipatazo kutoka katikakampuni za simu pindi mteja anapojaza fomu na kulipia ada kwa tigopesa au mpesakuna asilimia fulani zinaingia katika kampuni yetu kupitia mitandao ya simuvodacom na tigo pindi mteja anapotuma pesa na pia ada zinazolipiwa na watejawetu baada ya kujaza fomu Tshs.38,500 inaingia katika mfuko wa Social CreditCompany hivyo tunafaidika kwa asilimia kubwa kipato kinajitosheleza bilakuchukua riba

MTEJA ATAUPOKEA MKOPO WAKE MUDA GANI? BAADA YA KUJAZA FOMU NA KULIPIAADA

Mikopo yetu haicheleweshwi kwa mteja wetu atakae jiunga kwa kujaza fomu na kulipiaada kiasi cha Tshs.38,500 atapatiwa mkopo wake wa pesa ndani ya muda muafaka

Social Company imeondoa urasimu ili kumuwezesha mteja wetu kupata mkopo wakendani ya masaa24 baada ya maombi yake ya mkopo kuidhinishwa.

MTEJA ANARUHUSIWA KUKOPA KUANZIA SHILINGI NGAPI?

Mteja anaruhusiwa kuomba mkopo kuanzia Tshs. 200,000 (LAKIMBILI) Mwisho wa kukopa ni Tshs. 10,000,000 (MILLIONKUMI)

MTEJA ATAPOKEA VIPI MKOPO WAKE BAADA YA KUJAZA FOMUNA KULIPIA ADA?

Katika fomu ya kujiunga kuna kipengele kinamtaka mteja ajaze njia itakayokuarahisi kwake kupokea mkopo wake kuna M-Pesa, Airtel Money au Bank inategemea nakiasi cha mkopo mteja atakae omba mkopo kuanzia Laki Mbili mpaka Million Tatumkopo wake utatumwa kupitia M-Pesa au Airtel Money. Kuanzia shilingi MillionNne mpaka Million Kumi mteja atatumiwa mkopo wake kwa njia ya Bank katikaakaunti yake. Hivyo mteja atatakiwa kujaza namba ya M-Pesa au Airtel Moneykatika fomu ili mkopo wake utumwe kwa njia ya Mobile Banking pia mteja anawezakuandika akaunti namba zake za Bank ili apokee pesa zake kupitia Bank. Marabaada ya mteja kujaza fomu na kulipia ada atapewa taarifa pindi tukishamtumiapesa zake.

KWANINI MTEJA ANAJIUNGA ONLINE KATIKA MTANDAO?

Tumeanzisha utaratibu huu wa kujiunga online kupitia katika mtandao kulinganana sababu kubwa ya upungufu au ukosefu wa matawi yetu kuto-enea katika mikoayote Tanzania hivyo tumemrahisishia kila mtanzania ambae yupo mkoani na hakunatawi letu na anahitaji kujiunga ili awe mshirika aweze kupata mkopo iwe njiarahisi kujiunga Online kupitia katika mtandao huu kwa kujaza fomu yetu nakulipia ada Tshs.38,500 kupitia M-PESA au AIRTEL MONEY na tutaipokea fomu yakena tutampatia mkopo bila tatizo.

MTEJA ANAE HITAJI KUFIKA KATIKA OFISI ZETUATATUPATAJE? (Mawasiliano)

Contacts Details

JAMUHURI STREET
SCC MNAZI MMOJA BRANCH
1st FLOOR
P.O.BOX 9282
MENEJA: +255 22 2135823begin_of_the_skype_highlighting +255 22 2135823 end_of_the_skype_highlighting
FAX: +255 22 2163448
Email: info@socialcompany.co.tz

AINA ZA MIKOPO TUNAYOITOA KWA WATEJA

1. BIASHARA
Mikopo ya biashara tunaitoa kwa wajasiriamali /wafanya biashara
2. MAENDELEO
Mkopo wa maendeleo unatolewa kwa wateja wote ambaowanahitaji kufanya maendeleo binafsi kama kujenga nyumba, kununua gari, kununuakiwanja au vitu vya samani aidha ukarabati wa nyumba
3. ELIMU
Mkopo wa elimu unatolewa kwa wanafunzi walio vyuonikwa dhumuni la kuwasaidia kulipia karo mashuleni au kwa mahitaji binafsi yaelimu

JINSI YA KUREJESHA MKOPO

Mteja mara baada ya kujiunga kwa kujaza fomu na kulipia ada tukampatia mkopoatatakiwa kukaa miezi miwili bila kufanya marejesho na baada ya hapo ndioatatakiwa kuanza kufanya malipo ya mkopo wake KWAMFANO: Mteja kajaza fomu leo Tarehe 3 mwezi wa 5 na akalipia adatukamtumia mkopo wake basi atatakiwa kuanza kurejesha mkopo kuanzia Tarehe 3mwezi wa 7. Miezi miwili atakaa bila kulipia na baada ya hapo mteja ataanza kuaanarejesha malipo ya mkopo wake kupitia namba zetu za malipo Airtel na Vodacomkupitia M-PESA na Airtel Money

NAMBA ZA KULIPIA ADA YA KUJIUNGA NA MAREJESHO YAMKOPO

Mteja akishajaza fomu atatakiwa kulipia Tshs. 38,500 Elfu Thelathini na nane namiatano kupitia Airtel Money katika namba: 0689 659 472au M-Pesa katika namba: 0753 327 661 ni muhimukulipia na pia kwa wateja wa tigopesa mnaweza kulipia toka Tigopesa kuja M-Pesaau Airtel Money katika hizo namba zetu za kampuni na pesa itatufikia pia kwamarejesho ya mkopo zinatumika namba hizo hizo



MAREJESHO YA MKOPO

Mteja atatakiwa kurejesha kiasi chochote kile cha pesa kuanzia Tshs. 100,000Laki moja kila mwezi mpaka deni lake litakapo kwisha haijalishi mteja atakuaanalipia shilingi ngapi ila kima cha chini kianzie Tshs. 100,000 mtejaanaruhusiwa kuwa analipia laki moja au zaidi ya laki moja kulingana na uwezowake kinachotakiwa aweze kukamilisha malipo ya mkopo wake na marejesho yoteyasivuke miezi 160.

JIUNGE SASA UPATE MKOPO WA HARAKA NA NAFUU

Kujiunga ni rahisi mtu yoyote anaruhusiwa kujiunga na atapatiwa mkopo.Unachotakiwa kufanya bofya katika Link / Kimvuli hapa chini kilichoandikwa JAZAFOMU HAPA utaiona fomu ya kujiunga ijaze fomu yote kisha itume kwetu baada yahapo unatakiwa kulipia ada Tshs. 38,500 kupitia M-PESA katika namba 0753 327661 au unaweza ukalipia kupitia Airtel Money katika namba 0689 659 472 pia kwawateja wa Tigo na Zantel mnaweza kulipia toka katika akaunti zenu kuja katikanamba hizo na tutapokea malipo yenu.

ANGALIZO: Ni muhimu kulipia Tshs.38,500 ilikuchangia mfuko wa Social Company na mikopo itatolewa kwa wale ambao watajazafomu na kulipia ada pekee

Mikopo inatolewa kwa kila mtanzania wajasiriamali na wasiokua wajasiriamali piawafanyakazi wa makampuni binafsi na watumishi serekalini wanaruhusiwa kujiungana watapatiwa mikopo.

Bofya katika hii Link ifuatayo iliyoandikwa JAZA FOMUHAPA uweze kujiunga kwa kuijaza fomu na ulipie ada Tshs.38,500 tukupatie mkopo.Baada ya kujaza fomu na kulipia ada utapokea mkopo wako ndani ya masaa24.

 
aiseeeeeeeee_serikali bado wamelala usingizi wa pono,...mpaka waamushwe...sio leo.
 
ndugu zangu hii ni desi mpyaa, mtandao wenyewe haueleweki, hatari tupu, kuweni makini watu hawana ofisi, wanataka kutumiwa hela kwa tigo pesa au mpesa si balaa
 
haya walimu kazi kwenu ninyi ndo target manake siku zote mmefulia. Mtalizwa mpaka basi!

Mama yangu ni mwalimu,
Naamini hapo ulipofika ni kwa mchango wa waalimu kama yeye, onesha ufahamu waliokufundisha kwa kutokuwaadhihaki kwa kutoa maneno ya fedheha dharau na ukatisha tamaa kiasi hiki!!!
 
huo utapeli tu...

Sidhani kama mtu na akili zake anaweza kuingizwa mkenge wa kitotto namna hiyo, ukisoma hapo utagundua mapungufu lukiki ya kuchekesha! btw, vijana naona wanachangamkia ajira siku hizi.
 
Mwee too bad eatv why did u verify that this coy exists for real?. Ona sasa nimeshajaza form ila hela ilikua nitume leo.
 
Pole sana. kitendo cha kujaza hiyo fomu tuu tayari umeshibiwa MamaBeata kwenye bank accounts zako na hata kwenye accounts za mitandao..maana umewapatia vielelezo vyote muhimu vinavyokuhusu wewe:A S-key:
Mwee too bad eatv why did u verify that this coy exists for real?. Ona sasa nimeshajaza form ila hela ilikua nitume leo.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mleta mada bila shaka hiyo ndo nimekuwa nikiiona hata kule fb, jamaa wanatumia jina la first ladies, kuvutia watu, hata mda huu ukifungua fb utawakuta, mara nyingi wanaweka tangazo lao hilo.
 
Back
Top Bottom