DECI,KAKOBE,KADHI Jinamizi kwa ccm uchaguzi 2010


U

Ubungoubungo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2008
Messages
2,508
Likes
18
Points
135
U

Ubungoubungo

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2008
2,508 18 135
Nilipita mtaani nikaona watu wanajadili, moja ya suala wanalojadili ni namna udini ulavyozidi kuigawanya tz, haswa wanaodhaniwa kuwa wanaonewa kuwa ni wakristo, na kwamba hawaiamini selikali ya kikwete kama ina dhamira chanya kwao. watu wengi imeonekana wana bifu na CCM kwahabari ya DECI kwasababu waliliwa pesa na mpaka leo hawajarudishiwa pesa zao, deci ilikuwa ni ya wakristo kwa asilimia 90, lakini hadi sasa selikali haijaingilia kati kurescue pesa au kuwagawia.

sakata la kakobe nalo, inaonekana wengi wanaona kama ni uvamizi dhidi ya wakristo hawa walokole (ambao kwasasa wana influence kubwa sana tz, wana umoja sana, makanisa yao ni makubwa sana na wanaweza kuamini chochote ambacho mchungaji wao anaweza kusema). hivyo ni dhahiri ccm haitapata kura hata moja kwa watu wote wa aina hii tz nzima, hata kama haiko wazi, iko mioyoni mwao, labda kazi ya ziada ifanyike kujisafisha.

mahakama ya kadhi ndo imemaliza kila kitu, wakristo woote, wanaamini kuwa mahakama ya kadhi ni tishio kwao, hawa kwasababu watoto wao wanaoleana na watu wa dini zingine, hivyo mahakama ya kadhi itawaadhiri wao pia. pia, wanaona kama nchi inataka kubadilishwa kuwa kama somalia, au nigeria ya kaskazini. the same issue kwenye OIC, ni msumari mzito. na kwa suala hili, hakika selikali ya CCM ina kazi kubwa kulieleza hili hadi watu walielewe, otherwise, hawatapata kura yao hata moja, tembelea makania yao uone response yao.

yapo mengi, ila tusijifanye kama hatuoni! haya mambo yapo, yanaguguma mioyoni mwa watu, na yanatendeka kimoyomoyo (achilia mbali the alleged uonevu kwa wakristo zanzibar). nafikiri CCM kama hawata address haya mambo, then chama chochte cha upinzani iwe CUF au CHADEMA, au chochote kile, kinaweza kuaddress, hata kwa kutoa elimu tu ya uraia, na wakakomba kura zote. naionea huruma sisiemu, kwasababu kuna dalili mwaka huu watapata shida kubwa sana katika uchaguzi, mlango wao wa ushindi unaonekana ni tundu la sindano kwa ngamia kupita. wasalam!.
 

Forum statistics

Threads 1,237,227
Members 475,501
Posts 29,282,165