Debe la mpunga morogoro

Wasudi

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
226
223
Habari wakuu, nasikia kipindi cha mavuno mpunga hufikia hadi elfu tano kwa debe moja na gunia hufikia hadi elfu hamsini. Swali langu ni kwamba hili debe ukikoboa unatoa kg ngapi za mchele? Na hili gunia pia unaweza ukatoa kg ngapi? Naomba sana majibu yenu nataka kuingia ktk hii biashara ili niwe na takwimu sahihi.
 
debe moja la mpunga linatoa kilo 10,,,kwa maana hyo gunia moja la mpunga linatoaa kilo100,,lakin inategemeana na upimaji wako kama haupimi vizur,,gunia linaweza toa hata kilo 90
 
Ahsante mkuu maana nilikuwa nachanganyikiwa lengo langu ni kupata mchele tani 25 kwayo najua nijipange vp kwa hii duh mungu akulipe
 
debe moja la mpunga linatoa kilo 10,,,kwa maana hyo gunia moja la mpunga linatoaa kilo100,,lakin inategemeana na upimaji wako kama haupimi vizur,,gunia linaweza toa hata kilo 90
Mkuu hilo gunia la mpunga lenye kutoa kilo 100 ni Rumbesa au la kawaida lenye madebe 6?
 
Yes nazidi kupata maujuzi hapa jf zaidi darasa ahsanteni sana
 
Kwanza unatakiwa ujue gunia lina debe ngapi
Kuna magunia ya debe 7, 8 na kumi
Ila kwa hesabu yako ya gunia elfu 50 hiyo lazima itakuwa debe 7, ukikoboa gunia la debe 7 utapata kilo 55-60
 
Habari wakuu, nasikia kipindi cha mavuno mpunga hufikia hadi elfu tano kwa debe moja na gunia hufikia hadi elfu hamsini. Swali langu ni kwamba hili debe ukikoboa unatoa kg ngapi za mchele? Na hili gunia pia unaweza ukatoa kg ngapi? Naomba sana majibu yenu nataka kuingia ktk hii biashara ili niwe na takwimu sahihi.
Mm ni mkulima morogoro kama unataka kweli kuingia kwenye biashara hii nitafute wakati wa mavuno nikununulie mpunga kijijini kwetu na vijiji vya jirani
 
Habari wakuu, nasikia kipindi cha mavuno mpunga hufikia hadi elfu tano kwa debe moja na gunia hufikia hadi elfu hamsini. Swali langu ni kwamba hili debe ukikoboa unatoa kg ngapi za mchele? Na hili gunia pia unaweza ukatoa kg ngapi? Naomba sana majibu yenu nataka kuingia ktk hii biashara ili niwe na takwimu sahihi.
Ukikoboa mpunga, unapata mchere takiribani nusu ya mpunga ulio ukoboa!!! Kwa gunia la debe 8 ukikoboa utapata debe 4-5 za mchele!!!
Uzito unategemea na mpunga wenyewe ulikomaa kwa kiwango gani? Pia nadhani hata eneo kwa maana rutuba ya shamba ulipo toka
 
Yaah uzito wa mpunga unategemea na mbegu, zipo mbegu aina nyingi na zinatofautiana bei ya gunia
Kuhusu rutuba sio ishu sn ishu ni maji mpunga unahitaji maji yani shamba likiingia maji fresh mpunga unakuwa mzito na mzuri sn
Pia kuvunwa mpunga unatakiwa uvunwe kwa wakati usiwahi wala usichelewe sn
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom